Mtuflani Official
JF-Expert Member
- Dec 31, 2019
- 1,936
- 4,347
MTV Base Africa leo wametangaza kusitisha tuzo za MAMAs ambazo zilikua zifanyike 20 mwezi huu nchini Uganda.
Ikumbukwe tarehe 14 mwezi wa kwanza Uganda ilikua na uchaguzi wa Urais ambako Museveni alishinda lakini watu walidai uchaguzi haukua wa haki.
Dj maarufu duniani ambaye ni Dj Khaled na mwanamuziki alipangwa kuwa mshereheshaji wa hizi tuzo.
Cha ajabu Dj Khaled alijaribu kupost ujumbe kupitia twitter kutangaza hizo tuzo lakini wananchi wa Uganda walimjibu kwa kupost picha za watu waliouawa katika kipindi cha uchaguzi. Hii ilifanya Dj Khaled kufuta ule ujumbe na pia kufuta video zinahusiana na tuzo hizo kwenye mitandao yake ya kijamii.
Kuna mzungu anaitwa Jeffrey Smith huko twitter. Huku wengine tunamkumbuka kipindi cha kampeni za Tanzania 2020 alipokua akimshabikia Tundu Lissu huku akimpinga sana Magufuli. Jeffrey Smith alikua mstari wa mbele kupinga MAMAs kufanyika Uganda.