Siasa Za Zanzibar Zinaongoza Kwa Udanganyifu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa Za Zanzibar Zinaongoza Kwa Udanganyifu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Aug 30, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  SALIM SAID SALIM,
  UDANGANYIFU ni moja ya njia zinazomsaidia mtu, hasa akiwa katika matatizo, kujiliwaza, kumpunguzia usumbufu na hata kumpa furaha kwa muda na kujiona amefanikiwa na baadaye ndio huelewa ameharibikiwa kutokana na kudanganya.
  Tabia ya kudanganya au kusema uwongo si jambo baya na unaweza kusema ni haki ya msingi ya binadamu. Kila mtu anayo haki ya kusema uongo na kuuamini uongo anaoubuni. Lilio muhimu ni kwa yeye kukaa na uongo wake peke yake na huwa kosa pale anapoueneza huo uwongo anaouamini kwa wengine na kuwataka wauamini.
  Mara nyingi ninapozitafakari kauli za watu mbali mali wa Zanzibar, viongozi na wale wanaoitwa ‘pangu pakavu’, huona uongo umestawi na kupaliliwa. Upo wakati hukaa nikasema kama yatafanyika mashindano ya Olimpiki ya kusema uongo, basi washiriki wengine watalazimika kugombea medali za fedha na shaba kwani uwezekano wa Mzanzibari kuchukua medali ya dhahabu ni kubwa.
  Katika medani ya siasa na hasa katika masuala ya uchaguzi, uongo umekithiri na una sura ya kusikitisha na kutisha. Karibu kila unalolisikia basi huwa kinyume chake, yaani kauli hzo hua za udanganyifu. Hata wana wa taaluma ya habari nao ametumbukia katika utamaduni huu wa uwongo kutokana na uzito wa pochi anazopewa, iwe kutoka kwa walio madarakani au wa kambi ya upinzani.
  Pande zote mbili zina vitimbakwiri vyao ambavyo hubadilisha maneno na kueleza ya uwongo ili kuwafurahisha wanaowapa mshiko, iwe SMZ, CCM au CUF. Wengine husukumwa tu na utashi wao wa kupenda chama fulani.
  Kila baada ya siku chache, Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, amekuwa akisema kila Mzanzibari mwenye haki ya kupata kitambulisho atapewa na kila mwenye haki ya kupiga kura ataandikishwa katika daftari la kudumu. Lakini hakuna linalofanyika na mamia ya watu wanaendelea kusumbuliwa na kwa kuwekewa vikwazo vya kila aina.
  Wapo wanaokataliwa kupewa hizo fomu, wapo wanaokwenda kwa masheha na kuambiwa kwa vile ameshateremsha bendera ameshafunga ofisi na wengine kila siku huambiwa njoo kesho, kama afanyavyo kuku kwa vifaranga vinavyotaka kunyonya!
  Wapo wanaokataliwa kupewa hizo fomu, wapo wanaokwenda kwa masheha na kuambiwa kwa vile ameshateremsha bendera ameshafunga ofisi na wengine kila siku huambiwa njoo kesho, kama afanyavyo kuku kwa vifaranga vinavyotaka kunyonya!
  Hapa ungelitarjia waandishi kuhoji kwa nini kauli ya Rais inawekewa vikwazo na masheha. Badala yake unasikia habari za eti vitambulisho vimeanza kutolewa badala ya kuuliza kwa nini waliosababisha vurugu hii kwa kuwanyima watu haki yao ya vitambulisho na kujiandikisha hawawajibishwi kisheia? Hawakukosea wale wanaosema taaluma ya habari imevamiwa na akina adisadi (mafisadi). Tukumbuke kuwa kpotosha habari ni ufisadi.
  Mkurugenzi wa Vitambulisho, Mohammed Juma, naye anasema mamia ya watu hawaendi kuchukua vitambulisho vyao. Lakini ukweli ni kuwa wananchi wengi waliokwenda kuchukua vitambulisho wamejikuta wanapewa msururu wa masharti, ikiwa ni pamoja na kwenda kupata barua ya sheha na kutakiwa waandike barua kueleza kwa nini imewachukua muda kwenda kuvichukua vitambulisho. Kama hivi si vikwazo ni kitu gani?
  Hapa pana udanganyifu wa aina fulani, au Mkurugenzi ambaye aliwahi kuwalalamikia masheha haielewi kinachoendelea.
  Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Juma Tindwa, naye amekuja na yake mpya. Anasema suala la vitambulisho si la kisiasa. Sijui anamdanganya nani, kwani hivi vitambulisho imefanywa leseni ya kupata haki ya kupiga kura na kama uchaguzi hauna uhusiano na siasa ni jambo gani lenye uhusiano na siasa…kukimbiza mwenge?
  Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Khatibu Mwinchande, naye anasema kwa mujibu wa takwimu, Zanzibar inaongoza kwa watu wengi kujiandikisha na kupiga kura kusini mwa jangwa la Sahara. Upo ukweli wa kauli hii, lakini hauwi ukweli kama ukweli wote unaolizunguka suala hili haukuelezwa. Nao ni pamoja na udanganyifu uliofichwa kwenye mabano.
  Nao ni kwamba idadi ya watu wanaojiandikisha na kupiga kura Visiwani ni zaidi ya asilimia 90 ya makisio ni kwa sababu wapo wengi wanaopiga kura mbili au tatu.
  Ni kawaida wakati wa uchaguzi kuona magari yanabeba makundi ya vijana wakizunguka kituo baada ya kituo kupiga kura.
  Kwa mujibu wa ripoti ya ZEC ya uchaguzi wa mwaka 2005 walikuwapo watu zaidi ya 5,000 waliojiandikisha kupiga kura zaidi ya mara moja. Kinachoshangaza ni hata mmoja wao hakushitakiwa na orodha ya watu hawa waliovunja sheria haikuchapishwa.
  Na ofisa wa ZEC na vyombo vya dola bado wanapaswa kueleza kwa nini wanalindwa. Ni kawaida kama ilivyoshuhudiwa katika majimbo ya Kwahani Kitope na Unguja, kwa idadi ya wapiga kura kuzidi kwa zaidi ya asilimia 50 ya watu waliojiandikisha.
  Vile vile Zanzibar katika uchaguzi wa mwaka 2005 palikuwa na vituo vya wapiga kura ambavyo ZEC ilisema haikuwa na taarifa navyo. Nani aliendesha vituo hivyo na wapi walipata karatasi za kura na vifaa vyengine vya uchaguzi ni kielelezo chenye kuonyesha kwa nini idadi ya watu wanaopiga kura Zanzibar huzidi asilimia 95 ya matarajio. Tusishau pia kuwa Zanzibar inashuhudia mamia ya wapiga kura mamluki wakiletwa kutoka Bara na yapo maeneo yanayotumika kama kambi za kuwaweka na kuwahifadhi hawa wapiga kura mamluki. Nani anawaleta ni sula la mjadala.
  Kwa kweli mtindo wa kutoa kauli ambazo hazina ukweli hausaidii kutatua matatizo ya Zanzibar na badala yake inayaongeza.
  Wakati tunaelekea uchaguzi wa mwaka 2010 ni vizuri ikaeleweka kua udanganyifu hautasaidia.
  Viongozi waliopo madarakani na wa upinzani wanapaswa kujenga utamaduni wa kusema na kukubali ukweli.
  Utashi wa kisiasa usiwe sababu ya kubuni uwongo na kutaka wengine waukubali na wauamini. Ni vizuri kila mmoja wetu akajidanganya mwenyewe na sio wengine.
  Waandishi wa habari nao waelewe atumizi mabaya ya kalamu zao yataiponza Zanzibar na wakija kuhukumiwa siku za mbele kwa kuchangia kuharibu hali ya kisiasa Zanzibar wasije kulalamika. Wajue kisima wanachochimba siku moja watatatumbukia wenyewe na hatakuwepo mtu wa kuwaokoa.


  SOURCE:TANZANIA DAIMA.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hebu fikiria tu pale mwanasiasa anasimama jukwaani anawahutubia wananchi na kuwaambia kuwa Chama kimefanikiwa kutekeleza ilani yake kwa asilimia 100, halafu wananchi hao wanapiga makofi na kushangilia huku njaa zinawauma ni uongo kiasi gani, tokea wanadanganywa wakijiona na huku na wao wanajidanganya wenyewe eti wakiamini kuwa ni kweli ilani imetekelezwa kwa asilimia mia moja.
  Halafu cha ajabu zaidi SMZ haijawahi kukubali kushindwa, kukosea, kusahau, kughafilika, kupitikiwa, bahatimbaya n.k misamiati hii haimo katika kamusi za SMZ,siku zote wao wapo 100% right, wakikosolewa au kuelekezwa wanakuja juu na kukataa kila kitu na kutafuta sababu za kiongo ongo kuhalalisha makosa yao. Hakuna na wala sikumbuki kiongozi wa SMZ au waziri kusimama na kusema pahala kuwa hapa tumekosea, tumeghafilika,tumeshindwa n.k
  Mwandishi mmoja wa TVZ alitoa taarifa juu ya hali ya uchafu ya wodi ya watoto ya Hospitali ya Mnazimoja kiasi ya kusababisha wadudu aina ya mende kuzaliana na kuenea mpaka vitanda vya wagonjwa, mama yangu we! kilichomtokea mwandishi yule anajuwa Mungu, laiti kama angekua ni "mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa" wangelim-Samuel Sitta, sema manusra ni mtoto wa kigogo tu, na licha ya hivyo alihamishwa TVZ na kupelekwa Idra ya Habari Maelezo kuandikia gazeti na sura yake mpaka leo haionekani kwenye TV.
  Hata aliyewahi kuwa mwandishi wa TVZ, Marine Hassan, alikiona cha mtema kuni alipohoji tu msimamo wa SMZ kukataa udhamini wa kampuni za ulevi katka michezo wakati huo huo serikali ikipokea misaada mengine kutoka kampuni hizo katika mambo yasiyokuwa ya michezo na huku ulevi ukiuzwa na kutangazwa katka maeneo mbali mbali, Waziri Issa Moh'd Issa(RIP) wakati huo si tu alimjibu alivyotaka yeye bali pia alihakikisha kuwa sura ya Marine Hassan haionekani tena TVZ na kweli ikawa hivyo.
  Kwahiyo kwa uwongo tu siasa za Zanzibar hazijambo.
   
 3. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mambo ya zanzibar ni kuzungumkuti kitupu. hakuna haki wala sheria mbele ya siasa. wazi ni dhahiri kabisa na unafanywa mchana kweupeeeeeee.
   
Loading...