Siasa za "wafu" na "vipofu" zikikoma tunaweza kujiuliza maswali kama haya

winnerian

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
335
530
"Je! Unafikiri China inasubiri kuwekeza katika miundombinu yake ya dijiti au utafiti na maendeleo? Ninawaahidi, hawasubiri," Bwana Biden alisema katika hotuba yake Jumatano.
Bwana Biden alisema Uchina na ulimwengu wote "wanakimbia mbele yetu katika uwekezaji walionao siku za usoni".


"Do you think China is waiting around to invest in its digital infrastructure or research and development? I promise you, they are not waiting," Mr. Biden said in a speech on Wednesday.
Mr. Biden said China and the rest of the world "are racing ahead of us in the investments they have in the future".

Unaweza kusema tukiacha kutawaliwa na kuongozwa na vichwa vilivyooza kwa rushwa na ulafi basi tutapata maendeleo ya kweli na hakika. Kazi keleleni tu na kujipendekeza kwingi ilimradi upate cheo madaraka na mwisho uchumie tumbo na kizazi chake cha baadae kisichokuwa na uhakika wa kumudu yote uliyoibia wengine kwa kutumia dhamana uliyopewa.
 
Si useme tu kua unamsema Nikki wa pili
Ni nani huyo?
Unaweza kusema tukiacha kutawaliwa na kuongozwa na vichwa vilivyooza kwa rushwa na ulafi basi tutapata maendeleo ya kweli na hakika.
Hata hili sina hakika nalo mkuu 'winnerian.'

Tunaweza kabisa kuwa na viongozi na kutawaliwa na vichwa visivyokuwa na sifa kama hizo ulizotaja, lakini bado tukawa tunakwama.

Je, unaonaje kama tukiongozwa na vichwa vinavyoamini waTanzania hawana uwezo wa kujiletea maendeleo bila ya kuwakimbilia na kujisalimisha kwa jirani?

Unadhani hapo pana matumaini kweli?
 
Acha tuendelee kuwa soko la bidhaa za wengine, haijalishi hali itakuwaje lakini maisha lazima yataendelea!
 
Back
Top Bottom