Siasa za utoaji PhD za Open University of Tanzania

Andrew123

JF-Expert Member
Jun 2, 2012
8,281
10,794
Nimeshangazwa sana na Utoaji wa PhD wa Chuo hiki kikongwe hapa Tanzania (1992-2016). Kwanza aina ya tafiti wanazofanya zinaniacha mdomo wazi kwa mfano Mahafali ya 16 December 2015 mtunukiwaji aliandika "thesis" inaitwa "DETERMINANTS OF SUSTAINABLE FARMERS ORGANIZATIONS IN TANZANIA" na akapewa PhD kilainiii namna hii tutatoboa kweli? Sasa kimbembe kimekuja kwenye Shahada ya Heshima ya jana ndo nimechoka vigezo vilivyotumika kumpatia "mtunukiwaji" eti KUTEMBELEWA NA MARAIS WA DUNIA hivyo anastahili kupewa daah! Inasikitisha. Tafakari.
 
mpeni na mzee Maembe PhD ya heshima maana naona anaweweseka tu baada ya kukosa uteuzi wa Ngosha
 
Phd skuiz zinavyotolewa nikama tuzo za KILI.
Kama unatoa mikataba kiholela na watu wanajibebea maliasili kama madini,wanyama na mbuga,magogo,ardhi,viwanda,samaki,gesi nk kiholela,lazima viongozi wadunia watiririke kukufata ili nchi na watu wao wafaidi.
ajabu nipale watuwako wanapokutunuku kwa kuwezesha hayo kutokea.
Nimewahi fika mbuguni mererani inapotoka
tanzanite yote ya dunia hii!!?! Unaweza kulia kwa maisha yalivyo magumu. Hata walimu wakipangiwa kwenda kufundisha kule hugoma jumla.tunachukuliwa madini na kuachiwa ukame,njaa na umaskini.
Shame on us!! Vizazi vijavyo vitatulaani saaana.
 
nchi yangu Tanzania ni ya ajabu sana maana tulidhani Wasomi watatusaidia kumbe hata nao wameangukia mifukoni mwa wanasiasa!! Tutegemee nini kwa wasomi wa PhD walioteuliwa kwenye uwaziri na ukatibu mkuu/naibu? Watatuvusha? Open University mmetia aibu
 
sijawahi kusikia Open University wamefanya jambo la maana, kwa hiyo hata hili sishangai
 
Yes title haivutii lkn research yake ilikuwa imeleta tija gani ktk mapinduzi ya kilimo!
Kipi kilikiwa innovative ktk hiyo thesis, sidhani kama tunahaki ya kubeza just title na kumake solid conclusion kuwa hapo hamna kitu!
Ikiwa ni kuhukumu hiyo thesis weka abstract yote watu waangalie nini kilizingatiwa! Kweli title ipo shallow kama ya undergraduate lkn huwezi jua content hadi usome abstract!
 
nchi yangu Tanzania ni ya ajabu sana maana tulidhani Wasomi watatusaidia kumbe hata nao wameangukia mifukoni mwa wanasiasa!! Tutegemee nini kwa wasomi wa PhD walioteuliwa kwenye uwaziri na ukatibu mkuu/naibu? Watatuvusha? Open University mmetia aibu
Hata Australia China walimpa JK degree za heshima!
Hakuna sababu ya kukiandama chuo hiki kwa kumpa JK degree ya heshima!
Hakuna mtu mmoja anaweza kuisaidia Tanzania, hii ni nchi yetu wote!
Hata kama wangekuja wasomi wote wa dunia kutuongoza bado wasingeweza kuifanya Tanzania iwe na maendeleo iwapo wananchi watakuwa passive!
Wewe Andrea ukisubiri Magufuli au waziri x ndio afanye hayo mabadiliko Utakuwa unasubiri kama fisi! Tufanye kazi kama mchwa, tulipe kodi na tusimamie haki na uwajibikaji kila mtu katika nafasi yake, hapo waziri msomi atasaidia! Nje ya hapo unasubiri miujiza tu!
 
Acheni wivu....Kikwete ni mtu mwenye bahati kubwa...yuko tofauti na nyinyi...kumuonea wivu kwenu hakubadili kitu chochote. Na chuo cha Open sio cha kwanza kumpa hiyo shahada ya heshima. Na pia sababu uliyotumia ya Kikwete kupewa shahada ya heshima sijui umeitoa wapi, lakini sio ambayo ilitajwa na chuo husika kilichotoa hiyo shahada.

Kitu kingine, Kikwete hana haja ya kufanya siasa kwa sasa. Hana mpango wa kugombea urais au nafasi yoyote ile. Ni mtu mpuuzi tu ndiye atadhani Kikwete anafanya siasa kwa sasa.
 
Yes title haivutii lkn research yake ilikuwa imeleta tija gani ktk mapinduzi ya kilimo!
Kipi kilikiwa innovative ktk hiyo thesis, sidhani kama tunahaki ya kubeza just title na kumake solid conclusion kuwa hapo hamna kitu!
Ikiwa ni kuhukumu hiyo thesis weka abstract yote watu waangalie nini kilizingatiwa! Kweli title ipo shallow kama ya undergraduate lkn huwezi jua content hadi usome abstract!
Ndio maana tunasema ukiwa UKAWA sharti elimu yako iwe ya hapa na pale otherwise huwezi kuvumilia upuuzi wao. Badala mtoa post angetuletea objectives za hiyo thesis...Yeye anatuletea title. Title ni nembo tu, lakini haina maana kubwa kama mtoa post na akili zake za hapa na pale anavyodhani.

Kuleta title na kuhitimisha study ilikuwa ya hovyo ni sawa na ku-judge kitabu kwa kutazama cover lake tu.
 
Wewe ni ccm mwanamabadiriko hawezi andika sweeping statements kama hizo. Nani akusanye kosi kama serikali yenyewe ndio inaiba fedha ya kodi
 
Back
Top Bottom