Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,997
- 20,329
Kwa Afrika nchi zote zinaongozwa kidikteta kwa karibu 51%, zingatieni kuwa madikteta wasomi ni hatari kuliko madikteta wapumbavu.
Dikteta msomi hutawala huku umma ukilia moyoni wakati machoni ukichekelea, madikteta wapumbavu hutawala huku umma ukicheka moyoni wakati machoni ukilia.
Utawala wowote wa kidikteta ni adui wa mawazo kinzani, yaani vyama vya siasa havina nafasi kwenye tawala za kidikteta, hii ni duniani kote.
Angalizo langu upinzani Afrika ujitathimini na kubuni njia mpya za kupambana na tawala za aina hii, kitendo cha kuruhusu baadhi ya mambo yanayotafsiriwa kuwa ni udikteta yakapita mbele ya umma bila kupingwa kisawasawa ni kuipa nguvu serikali inayoongozwa utawala wa kiimla.
Upinzani Afrika unazo njia tatu.
KWANZA: Kulazimisha upingaji wa uimla huu kwa njia ya maandamano,
Hapa matokeo yanaweza kuwa mawili.
1. Kuuwa kwa waandamanaji lakini mwisho serikali ikakubali kulegeza msimamo au ikatia mkazo, hili tumeliona Burundi na Uganda na kwingineko. Njia hii imeshapitwa na wakati.
2. Kuogopa kwa serikali na kulegeza msimamo bila kumwaga damu, hili tumeliona Tunisia, Bukinafaso, Misri, nk.
MBILI: Kubadili njia ya siasa kwa kutumia muundo wa chambuzi za hali ya nchi. Chambuzi hizi ziwekwe kwenye muundo wa hotuba za kitaifa za kila mwezi na zinatakiwa kufanywa na viongozi wa juu kwakutumia vyombo vya habari, Hapa lazima vyama vya siasa viwekeze nguvu kubwa kwenye ujasusi ili kupata habari sahihi na stahiki, mfano afya, elimu, nishati nk...
Na kisha kila mwezi kutakuwa na hotuba ya saa moja ya kiongozi mkuu wa chama ama katibu mkuu nk ilimradi awakilishe chama taifa. Hii inaweza kukumbana na kikwazo katika vyombo vya habari ambavyo vingi vinaweza kutishiwa ama kufungiwa kabisa.
Utaratibu huu huendeshwa na nchi nyingi duniani hasa zile zilizopevuka kifikra na kisiasa.
TATU: Kutumia udhaifu wa chama tawala, mfano mpasuko wa chama tawala ama makosa ya serikali yake. Njia hii ndio hutumiwa na vyama vingi Afrika kutokana na kuwa vyama vingi vina itikadi zisizofahamika kwa wanachama wao, hii ikiwemo Tanzania kwa miaka yote na ndio iliyovipa mafanikio na umaarufu vyama vya upinza, ambapo kwa muono wangu awamu hii ya tano kwakiwango fulani ccm imeonyesha kuizuia njia yetu, kwakuwa wakifanya kosa wanatumia vyombo vya habari kuziba makosa hayo mapema kwakutumia kitu kiitwacho "kutumbua majipu". Zingatieni jamii zetu za Afrika zinapenda siasa za urembo ama za rangirangi (decorated politics) na ccm wanafaulu hilo.
Zipo agenda ambazo kwa kisayansi ni za umma, mfano ufisadi hii ni agenda ya umma kwa Afrika, hivyo akitokea mtawala akawarubuni wananchi kuwa anapambana nao hata kwa geresha tu watamuunga mkono, na kwakuwa tawala za kidikteta kote duniani hudhibiti vyombo vya habari hivyo geresha ya vita dhidi ya ufisadi hutangazwa kwa nguvu zote.
Kisiasa akitokea mtu yeyote mwenye uelewa mzuri akapinga aina ya vita hivyo inavyopambanwa atapingwa na umma kwakuwa hana uungwaji mkono kwa wingi.
Binafsi kwa Tanzania kitendo cha upinzani nikiwemo mimi kukosoa utawala huu hasa aina ya utumbuaji majipu wa serikali ya Magufuli ni tendo la ushujaa na utii wa itikadi, lakini hausaidii siasa za Upinzani kwakuwa nguvu ya kutetea ni ndogo tofauti na nguvu ya kutangaza utumbuaji huo inayofanywa na serikali, Serikali imedhibiti vyombo vya habari vyote vikabaki kuhubiri majipu tu kila kona, na kwamantiki ya sayansi ya siasa, Suala la Majipu limefanikiwa kutengenezwa kuwa "agenda ya umma", hivyo kulipinga ni kujimaliza kisiasa, Werevu wachache tunatambua kuwa chama tawala kinarubuni umma, lakini Wananchi wengi wenye uelewa mdogo wanatushangaa wakati huo propaganda ya utumbuaji inashika kasi.
Licha ya hali mbaya ya maisha inayoendelea kuwakumba lakini ni ukweli kuwa jamii kubwa ya waafrika huwa haistuki mpaka ianze kufa kwa njaa ndipo huamka, Sukari bei juu, nk
Hii ni siasa hivyo mchezo upo upande mmoja.... Tujisahihishe...
2020 ni kesho tu sio mbali.