Siasa za Umeme: Kwa vile Umeme wa Stigler's utatosha na ziada kuuza nje. Je, TANESCO kusaini PPA mpya 6 toka kwa 6 IPPs, sio ufisadi mpya wa kisasa?

CHA MSINGI MKATABA UWE OPEN WANAUZIWA UNIT 1 KWA SHILINGI NGAPI SIYO KUTULETEA MAMBO RICHMOND NA IPTL HAPA>>unit 1 ISIZIDI sh 100

NA KULE RUFIJI WANACHIMBACHIMBA TU
NUCLEAR NDIO SOLUTION PEKEE YA UMEME HAO MABEBERU WANATUMIA HALAFU WANAZUGIA KWENYE UPEPO NA MAJI KUTUDANGANYA SISI WAAFRICA
 
Mkuu Paschal, hao wote ni wazalishaji wadogo sana huwezi walinganisha na IPTL, RICHMOND etc. Baadhi yao MillardAyo amewarusha Sana kwenye mtandao wake. Tanesco inachofanya ni kujaribu kuwa boost watanzania wabunifu walioanza kuunganisha mitambo yao kwenye maporomoko locally na ku supply vijiji vya jirani tena bure mwanzoni.

JPM aliposikia akaamuru wawezeshwe na waingizwe kwenye mpango maalum ili kuwawezesha baadae kufika level za juu zaidi. Hii imefanyika kati ya 2017 - 2019. Ukifatilia kwa ukaribu hizo kampuni zote ni za wazawa tena wa huko ndani ndani. Hili ni jambo la kuishukuru Tanesco na serikali badala ya kulaumu au kutilia shaka.

Hapo hakuna kampuni ya mchina,mhindi wala mzungu hata mmoja. Hao ni wabunifu wa humu humu Tanesco inajaribu kuwainua. Hujiulizi kampuni sita Total supply ni 19.6 MW ?
Majibu ya Pascal yapo hapa,Welldone!!
 
Tutofautishe installed/capacity au generated energy capacity na delivered energy capacity. Umeme unaozalishwa siyo wote unamfikia mlaji/mteja. Lazima ujue kuna capacity factor ina husika hapo. Yaani capacity factor ni uwiano wa matumizi na uzalishaji wa umeme kwa muda maalumu waweza kuwa kwa mwezi ama mwaka. Vyanzo/miradi ya umeme ina capacity factor tofauti. Umeme wa Maji ukiwa na capacity factor ya juu.
Ninaona aidha uko confused au unataka kwa makusudi ku confuse watu kwa lugha hiyo ya capacity factor, installed capacity, generated energy capacity, delivered energy capacity and so on. Nadhani lengo lako ni ku justify tanesco kununua umeme huo wa wamachinga na kuja kutuuzia sisi badala ya wamachinga hao kutuuzia sisi mojamkwa moja hiyo bidhaa yao ya umeme.

Nimejaribu kutumia lugha nyepesi kurlezea logic ya biashara hiyo. Nitatoa ufafanuzi na mifano rahisi kama ifuatavyo;

1. Chukulia grid ya taifa kama ni lori la tani 10. Yaani lori hili lina uwezo wa kubeba mzigo wa tani 10. Hivyo installed capacity ya lori hili ni tani 10. Wateja waliopatikana jumla ya mzigo wao wanaotaka kuusafirisha ni tani 8 tu. Hivyo litasafirisha tani nane kwa operating expense hiyo hiyo kama lingesafirisha tani 10 hususani idadi ya lita za diseal nk. Delivery capacity ya tani 8 au hata tani 1 linayo. Sasa itakuwa ni uendawazimu kwa mmiliki wa lori hilo la tani kumi kukodisha bajaji sita kutoka watu binafsi kumsaidia kusafirisha mzigo huo wa tani 8 wa wateja wake. Yaani lori hilo na bajaji hizo 6 zitumike kusafirisha mzigo huo.

2. Ukiacha umeme wa jua kuchaji mabetri (solar electricity), umeme huzalishwa na mashine zinazoitwa power generators ambazo hutumia (kuwaka) aidha mafuta ya petroli, diseal, gas, makaa ya mawe, nguvu za atomic au nguvu za upepo. Kila mashine ya hizi generators ina uwezo wake wa kiasi cha umeme itakaoutoa pale itakapowashwa (installed capacity) kama hilo lori la tani 10. Chukulia generator yako ya nyumbani yenye capacity ya 5,000 kw. Ukiiwasha umeme inaotoa unawezo wa kuwasha jiko lako la umeme, taa zako zote za nyumbani, fridge zako za nyumbani, washing machine yako, water heaters za bafuni kwako, microwave yako, tv zako zote, computer zako zote nyumbani na pasi yako zote kwa wakati mmoja. Kama utawasha taa chache tu fridge moja na tv moja tu, umeme mwingi utakaokuwa unazalishwa na hiyo generator yako ukiwa umeiwasha ndiyo tunaouita uko iddle. Yaani kwenye grid yetu ya taifa hadi sasa ina umeme wa 550 MW ambao uko iddle hatuutumii. Sababu kubwa hatuutumii ni kwamba bei ya kilowatt hour moja ya tanaesco ni kubwa sana kuliko nchi zote duniani. Hii imetokana na ufisadi wa miaka mingi katika shirika hili.

3. Kahama imekuwa ikipata umeme wa kutosha kutoka mgodi wa.almasi wa William Diamonds kabla hata tanesco haijazaliwa. Sasa hivi inapata umeme wa kumwagwa kutoka grid ya taifa ya tanesco. Sasa eti kuna jamaa anazalisha 10Mw za umeme wa solar ambao atakuwa anawauzia wanakahama kupitia tanesco! Yaani tanesco mnatuona sisi ni wajinga sana? Kuzalisha 10MW za umeme wa solar unahitaji solar panel 10,000 zenye capacity ya 100 watts kila moja na betri 60,000 za 300A au panel 5,000 zenye capacity ya 200W kila moja na betri 30,000 za 300Amps. Kiasi hicho cha ma solar panels na ma betri ku occupy eneo lote la mji wa kahama na pasitoshe. Huyo jamaa hana kiasi hicho cha ma panels na ma betri. Halafu what for and why all this expense?

4. Tanesco ina off grid power plants kwenye maeneo mengi tu nchini ambayo aidha hayajafikiwa na grid ya taifa au yako kwa ajili ya standby operation during national grid cut off. Off- grid power plants hizi hutumia diseal fired generating engines zenye capacity mbali mbali. Kwa mfano uwezo wa off grid power plant ya Mwanza iliyoko Nyakato ni MW 60, ya Kigoma ni 6.25MW from 5 generating units, Kasulu 2.5MW from 2 units. Plants za aina hii zipo pia kule Biharamulo, Mafia, Ludewa, Mpanda, Bukoba in case of the Uganda grid cut off, Liwale, Sumbawanga, Tunduru na Namtumbo. Hakuna sehemu ambako tanesco inahitaji huo umeme wa hao IPP sita.
 
Hii mada imekaa kitaalamu, ila nimeshangaa huko juu nimeona mtu mmoja anadai ya kuwa uhitaji utaalamu kung'amua kadhia hii.

Mabadiliko na mahitaji hayamsubirii mtu, bali kujiandaa ndiyo jambo bora zaidi. Hapa ingekuwa ni hoja ya msingi kujadili uwezo wa hizi kampuni ndogo,je zina uwezo au (Hili wahusika watalifanyia kazi).

Kwa nchi yetu ni ngumu au itachukua muda mrefu sana Umeme wa gridi ya Taifa kuwafikia watu wote na hii si lazima sana, ndiyo maana kuna wakati kununua Umeme kwa nchi jirani au kwa kampuni huwa ni gharama ndogo sana kuliko sisi kupeleka umeme wa gridi sehemu husika. Mathalani kwa eneo la Wilaya ya Kalambo kwa kipindi kile ilikuwa ni gharama sana kupeleka umeme wa gridi kuliko kununua umeme toka Zambia. Ndiyo maana tulikuwa tunanunua Umeme toka huko.

Lakini pia hivyo vyanzo vingine vinaweza kutumika kama "Stand by".

Nina mengi ya kuandika juu ya kadhia hii, ila nisiwachoshe sana, nakomea hapa.
 
Mkuu Paschal, hao wote ni wazalishaji wadogo sana huwezi walinganisha na IPTL, RICHMOND etc. Baadhi yao MillardAyo amewarusha Sana kwenye mtandao wake. Tanesco inachofanya ni kujaribu kuwa boost watanzania wabunifu walioanza kuunganisha mitambo yao kwenye maporomoko locally na ku supply vijiji vya jirani tena bure mwanzoni.

JPM aliposikia akaamuru wawezeshwe na waingizwe kwenye mpango maalum ili kuwawezesha baadae kufika level za juu zaidi. Hii imefanyika kati ya 2017 - 2019. Ukifatilia kwa ukaribu hizo kampuni zote ni za wazawa tena wa huko ndani ndani. Hili ni jambo la kuishukuru Tanesco na serikali badala ya kulaumu au kutilia shaka.

Hapo hakuna kampuni ya mchina,mhindi wala mzungu hata mmoja. Hao ni wabunifu wa humu humu Tanesco inajaribu kuwainua. Hujiulizi kampuni sita Total supply ni 19.6 MW ?
Mimi binafsi nimekuelewa.
 
Wanabodi,

Kwa vile hii ni mada technical, yaani ni mada ya kitaalam, naomba kuanza bandiko hili kwa elimu kidogo kwa members wenzangu ambao sio wataalam wa mambo ya power na energy.

Watu wanadhani siasa ni kusimama tuu majukwaani na kupiga domo, issues yoyote yenye impact kubwa kwa taifa ni siasa, hivyo hivyo zozote zinazohusu utilities, maji, umeme, gesi, mafuta, na public transport ni siasa, na kwa nchi zinazotegemea mkate kama chakula kikuu, issue yoyote. ya mkate ni siasa! kuna nchi inayotegemea mkate kama chakula chake kikuu, bei ya mkate ilipanda kwa thumuni tuu!, wananchi waliingia barabarani na serikali ilipinduliwa!. Hivyo issues za Umeme sio habari mchanganyiko ni siasa!

Kwa vile tumeelezwa umeme wa Stigler ukikamilika utatosha na ziada kuuzwa nje!, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani Desemba 14, 2020 akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa Mradi mkubwa wa kufua umeme wa Megawati 2115 kwa njia ya maji wa Julius Nyerere, amesema inatarajiwa kwa mwaka 2023 mahitaji ya umeme Nchini yakaongezeka kwa zaidi ya mara mbili mpaka kufikia megawati 2,770.

"Leo hii mahitaji kwa siku ni megawati 1,177.20. Kukamilika kwa mradi huu wa Julius Nyerere kutaongeza megawati 3,973 ambazo zitatumika katika shuguli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii hivyo tunahitaji umeme wa kutosha, utakaobaki tutawauzia majirani zetu" amesema Dkt. Kalemani.

Leo asubuhi, nimesoma mahali kuwa Tanesco imesaini mikataba mipya 6 ya PPA (Power Purchase Agreements) koka kwa wazalishaji binafsi IPPs (Independent Power Producers ) wapya 6, ili kununua megawati 19.16 na kuziingiza kwenye gridi ya taifa, ndani ya miezi 18 ijayo, Jee huu sio aina mpya ya ufisadi mpya wa kisasa kama ulivyokuwa ufisadi wa Richmond, Dowans na IPTL?!.

Hebu kwanza jisomee story yenyewe

TANZANIA: TANESCO to buy 19.16 MW of green electricity from six IPPs

By Inès Magoum - Published on December 14 2020 / Modified on December 14 2020

abriendomundo/Shutterstock" data-src="/proxy.php?image=https%3A%2F%2Fwww.afrik21.africa%2Fwp-content%2Fuploads%2F2020%2F12%2Fshutterstock_1464805487-800x400.jpg&hash=051e3b0f7fda1d5f598545cf47a53447" data-lb-sidebar-href="" data-lb-caption-extra-html="" data-single-image="1"> TANZANIE : la Tanesco va acheter 19,16 MW d’électricité verte à six IPP<img src=abriendomundo/Shutterstock" title="TANZANIE : la Tanesco va acheter 19,16 MW d’électricité verte à six IPPabriendomundo/Shutterstock" width="" height="" />

Six Independent Power Producers (IPPs) have just concluded power purchase agreements with the Tanzania Electric Supply Company (TANESCO). These private companies are developing renewable energy projects in Tanzania with a total capacity of 19.16 MW.​

The state-owned Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) is signing power purchase agreements (PPAs) with six independent power producers (IPPs) that are developing several renewable energy projects in Tanzania. TANESCO agrees to purchase 19.16 MW of electricity, under the supervision of the Energy and Water Regulatory Authority (EWURA) of Tanzania.

Among the selected IPPs is Nishati Lutheran Investment, which is implementing a 36-kW hydropower project at the Ijangala Falls in Makete. Similarly, Madope Hydro is implementing the 1.7 MW Madope Hydroelectric Project on the Madope River. Luponde Hydro is also signing a PPA with Tanesco for its Luponde hydroelectric project (9 kW) on the Luhololo River in Njombe. Lung’ali Natural Resources, which is implementing the Maguta hydroelectric project (1.2 MW) on the Lukosi River Falls in Kilolo, will sell its production to the utility.

Commercial operation in 18 months​

The other IPP selected is NextGen Solawazi which is working on a 5 MW hydropower project in the Kigoma Special Economic Zone. SSI Energy Tanzania, which is currently building a 10 MWp solar power plant in Kahama, will also sell its production to Tanesco. According to the public company, the six private companies will have to start marketing their production within 18 months.

In the meantime, TANESCO is developing other electricity projects in Tanzania. In this way, TANESCO is supporting the Tanzanian government’s policy of achieving a 75% electrification rate by 2035. Among its projects is the construction of the Rumakali and Ruhudji hydroelectric power plants which will have capacities of 222 MW and 358 MW respectively. In July 2020, TANESCO selected Multiconsult Norge AS, a Norwegian engineering consulting firm, to provide consulting services for the two projects.

My Take:
Japo mimi ni mwandishi wa habari, na sasa nimeisha staafu rasmi, lakini kwa vile kazi ya uandishi iko kwenye damu, hivyo ikitokea habari inahitaji ufuatiliaji, mimi nitaiweka tuu humu jf, wahariri watakao iona it's newsworthy, watatuma waandishi wao kuifuatilia, au waandishi watakaona ni habari, wataifuatilia, mimi nitakuwa nimetimiza wajibu wangu kwa jamii, ila ikitokea kweli ukawa ni ufisadi mwingine, utakuja kujulikana mwaka 2025 kabla ya uchaguzi ujao, nitakachokifanya ni kuwakumbusha tuu kuwa tulinusa, tukasikia harufu, tukauliza, na hayo ndio matokeo, ila pia, sio kila unaposikia harufu ya ufisadi ni ufisadi, harufu nyingine ni harufu tuu na hakuna ufisadi wowote, vitu vingine ni ukosefu tuu wa transparency, kama zile Bilioni 1.5 kwenye ripoti fulani ya CAG, watu wakadhani ni ufisadi, ikaja kukutikana hakuna ufisadi wowote.

Maswali ni haya.
  1. Kwanza maendeleo yoyote ya ujenzi wa mioundo mbinu wa umeme wa maji, ni maendeleo, endelevu, hivyo wakati Watanzania tukiusubiri huu umeme wa Stigler kuingizwa kwenye gridi ya Taifa, hakuna ubaya kwa Tanesco kuendelea kununua umeme toka kwa wazalishaji binafsi waliopo, kwa vile kuna wazalishaji wengi na mikataba imesimamishwa, kwa nini Tanesco wasiendelee nao na badala yake wanasani mikataba na wazalishaji wapya?. What is so special na hawa wapya, wakati wa zamani wapo, mikataba imesitishwa na wengine wametushitaki kwa kuvunja mikataba yao?
  2. Kama umeme wa Stigler, unatosha, hizi PPA's 6 mpya zinazosainiwa sasa ni za nini?.
  3. Kule nyuma tulivunja mkataba wa Dowans kwa tuhuma za ufisadi wa kulipishwa capacity charge kubwa na Tanesco kununua umeme wa bei juu toka kwa hawa IPPs na kuuza kwa bei ya chini!, Jee this time kwenye hii mikataba mipya jee Tanesco wananunua kwa bei gani per unit na kuuza kwa bei gani, tusije kuwa tunatwanga maji kwenye kinu?
  4. Baada ya kuvunjwa kwa mkataba wa Dowans, tulishitakiwa, tukashindwa kesi, tukadaiwa fidia iliyotwa Tozo ya Dowans, waheshimiwa wetu kule Bunge, wakajiapisha kwa maneno kama "over my dead body!" hatulipi! did you know what happened?....we paid every single cent kimya kimya na umeme ukapandishwa bei, Watanzania wote kwa ujumla wetu, tukafidia. Kitu cha ajabu sana katika hili, kampuni ile ile ya Dowans tuliovunja nayo mkataba, ikajibadili jina kujiita Simbion, mitambo ile ile, capacity charge ile ile, na mkataba ule ule, ikaingia tena mkataba na Tanesco, na tukakawa tunawalipa hadi JPM alipoingia, akaukataa ujinga huu, ndipo mkataba wa Simbion ukasitishwa na mpaka sasa kesi iko mahakamani, sijui tumefikia wapi! Kawa haya ndio mambo ya Tanesco na hizi PPA's zake, vipi hizi PPA's sita mpya are they clean?, transparent?.
  5. Kuna wakati kule nyuma, Tanesco ilikuwa inaelemewa na madeni ya umeme wa hawa PPA's na situation ya Tanesco kwa sasa ikoje hadi kuendelea kununua umeme kwa hawa wazalishaji binafsi, ili Tanesco ipate faida ni lazima inunue kwa bei ya jini na kuuza kwa bei ya juu, sasa kama Tanesco haina uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha, kwa nini hao wazalishaji binafsi wasiruhusiwe kuuza umeme wao direct kwa watumia kwa bei ya chini, wananchi ndio wafaidike?.
  6. Japo tunaelezwa Stigler ikikamilika Tanzania tutakuwa na umeme wa kutosha na ziada kuuza nje. Hawa jamaa wanasema "In the meantime, TANESCO is developing other electricity projects in Tanzania. In this way, TANESCO is supporting the Tanzanian government’s policy of achieving a 75% electrification rate by 2035", wakimaanisha huo mwaka 2035, Tanzania ndio tutafikisha 75% ya mahitaji yetu ya umeme!, sasa nani anasema kweli?, jee ni kweli tutajitosheleza na ziada kuuza nje, au tutajitosheleza kwa mahitaji ya sasa kwasabu bado hajaweza ku electrify nchi nzima, hivyo hiyo ziada tutakayouza nje, tutauza huku baadhi ya vijiji vyetu havina umeme kwasababu hatuna miondombinu ya kutosha ku i electrify nchi nzima?. Which is which?.

Paskali
Update
Habari yenyewe

TANESCO yasaini mkataba wa kununua umeme kwa wazalishaji wadogo​

KUSAINI MKATABA KATI YA TANESCO NA WAWEKEZAJI WADOGO

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeingia mkataba wa kununua umeme kutoka kwa wazalishaji wadogo wa kampuni sita binafsi, utakaoingia moja kwa moja kwenye kwenye gridi ya Taifa na kutumika katika maeneo mbalimbali Nchini.

Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini mikataba kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Meneja Mwandamizi Uwekezaji, Mhandisi Costa Rubagumya alisema wawekezaji hao wamekidhi vigezo kwa mujibu wa kanuni zilizoidhinishwa na EWURA.

"Kwa mujibu wa kanuni zinazosimamia uendelezaji wa miradi midogo ya kuzalisha umeme, inaitaka TANESCO kuingia mikataba na wazalishaji umeme wadogo kwenye maeneo ambayo gridi ya Taifa bado haijafika", alisema Mhandisi Rubagumya.

Aliainisha vigezo vingine ni maeneo ambayo yanatatizo la umeme mdogo ili kuimarisha ubora wa umeme na kigezo kingine ni maeneo ya usambazaji umeme ambapo njia za umeme za TANESCO ni ndefu hivyo kusababisha upotevu wa umeme.

Mhandisi Costa alizitaja kampuni hizo kuwa ni, Kahama Solar Power Project MW 10.0, Kigoma Solar Power MW 5.0, Nishati Lutheran (DKK) Investment Ltd MW 0.36.

Makampuni mengine ni, Madope Hydropower MW 1.7, Luponde Hydropower MW 0.9 na Maguta Hydropower MW 1.2.

Wakizungumza Kwa niaba ya Wazalishaji wadogo wa umeme, Padre Luciano Mpoma na Nicholas Richardson wameishukuru Serikali kupitia TANESCO kwa kukubali kufanya nao biashara ya umeme.

Waliongeza kuwa safari ilikuwa ni ndefu lakini hatimaye wamekuwa na furaha kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha nishati ya umeme inamgusa kila mwananchi.

Makampuni hayo yanatakiwa kuanza kuiuzia TANESCO umeme ndani ya miezi 18 kuanzia leo Disemba 08, 2020.

Update 2.
Mchango very constructive
Uwe na Akili na wewe. Kuna sehemu Grid ya Taifa haijafka,,maana yake wanaweka umeme wa jenereta sehemu ambazo hakuna muunganiko na gridi ya Taifa.,,na hapo baadae wataunganishwa na grid
 
Stiglers Gorge haijazalisha umeme na watu wanataka umeme leo. Tutajadiliana tena mambao haya huko mbeleni tukishakuwa na umeme wa ziada, ila kwa sasa hivi tuna upungufu wa mahitaji.
 
Nadhani lengo lako ni ku justify tanesco kununua umeme huo wa wamachinga na kuja kutuuzia sisi badala ya wamachinga hao kutuuzia sisi mojamkwa moja hiyo bidhaa yao ya umeme.
Kwa taarifa yako uuzaji wa umeme kutoka kwa hao unawaita 'wamachinga' unaongozwa na kanuni maalumu zilizowekwa na muangalizi wa mambo haya, EWURA. Hata Tanesco bei yao ya umeme inaratibiwa/ridhiwa na EWURA. Suala la bei ya umeme ama kutoka kwa hao unaowaita 'wamachinga' ama TANESCO siyo suala la kusumbua 'akili' kiasi cha kuanza kuulizana bei ya umeme ya pande hizi mbili!

Hivyo litasafirisha tani nane kwa operating expense hiyo hiyo kama lingesafirisha tani 10 hususani idadi ya lita za diseal nk
Nadhani hapa ndipo tunapoanza kupishana!!
===
Yaani lita za mafuta ya diesel zitakazotumika kusafirisha mzigo wa tani 10 kutoka (mfano) Dar kwenda Mbeya ni sawa na kiasi hicho kwa kusafilisha mzigo wa tani nane! Kwa taarifa yako ni kuwa gari likiwa limebeba mzigo mzito huwa linalazimika kutembea kwenye gia kubwa. Gia kubwa hufyonza mafuta zaidi, ili injini iwe na uwezo wa kuhimili mzigo huo. Gari likiwa na mzigo mdogo mara nyingi linatembelea kwenye gia ndogo kwani injini haihitaji nguvu kubwa hivyo haifyonzi mafuta mengi.

Mapungufu haya uliyoyaonyesha katika hili yana ua kabisa morali ya kuamini kuwa unatosha kabisa kufafanua suala lilipo mezani bila 'upendeleo'!

Kwa maelezo hayo hapo juu, nadhani wanaJF wataamua wenyewe ni nani wanamuona "... aidha yuko confused au anataka kwa makusudi ku confuse watu kwa lugha hiyo...."
 
No mimi sioni tatizo la TANESCO kwa kuingia mikataba kwa wazalishaji wadodo wa ndani kuwauzia umeme hata kidogo. Umeme wa maji mara njingi huwa rahisi kuliko wa mafuta, kinachotakiwa kulinda hapo ni mikataba imekaaje iwapo TANESCO wataweza kupata umeme wa kutosha toka kwenye vyanzo vyao. Now here comes back to capacity charges. Najua TANESCO wameingia kwenye migogoro mingi kwa kuingiliwa na wanasiasa sio wao wenyewe. Na hili ni uzembe wa TANESCO yenyewe kwa kuwa na poor strategic plan na kuacha mianya ya wanasiasa kujichomeka kwenye mambo yao. Nahisi watanielewa.
 
Wanabodi,

Kwa vile hii ni mada technical, yaani ni mada ya kitaalam, naomba kuanza bandiko hili kwa elimu kidogo kwa members wenzangu ambao sio wataalam wa mambo ya power na energy.

Watu wanadhani siasa ni kusimama tuu majukwaani na kupiga domo, issues yoyote yenye impact kubwa kwa taifa ni siasa, hivyo hivyo zozote zinazohusu utilities, maji, umeme, gesi, mafuta, na public transport ni siasa, na kwa nchi zinazotegemea mkate kama chakula kikuu, issue yoyote. ya mkate ni siasa! kuna nchi inayotegemea mkate kama chakula chake kikuu, bei ya mkate ilipanda kwa thumuni tuu!, wananchi waliingia barabarani na serikali ilipinduliwa!. Hivyo issues za Umeme sio habari mchanganyiko ni siasa!

Kwa vile tumeelezwa umeme wa Stigler ukikamilika utatosha na ziada kuuzwa nje!, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani Desemba 14, 2020 akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa Mradi mkubwa wa kufua umeme wa Megawati 2115 kwa njia ya maji wa Julius Nyerere, amesema inatarajiwa kwa mwaka 2023 mahitaji ya umeme Nchini yakaongezeka kwa zaidi ya mara mbili mpaka kufikia megawati 2,770.

"Leo hii mahitaji kwa siku ni megawati 1,177.20. Kukamilika kwa mradi huu wa Julius Nyerere kutaongeza megawati 3,973 ambazo zitatumika katika shuguli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii hivyo tunahitaji umeme wa kutosha, utakaobaki tutawauzia majirani zetu" amesema Dkt. Kalemani.

Leo asubuhi, nimesoma mahali kuwa Tanesco imesaini mikataba mipya 6 ya PPA (Power Purchase Agreements) koka kwa wazalishaji binafsi IPPs (Independent Power Producers ) wapya 6, ili kununua megawati 19.16 na kuziingiza kwenye gridi ya taifa, ndani ya miezi 18 ijayo, Jee huu sio aina mpya ya ufisadi mpya wa kisasa kama ulivyokuwa ufisadi wa Richmond, Dowans na IPTL?!.

Hebu kwanza jisomee story yenyewe

TANZANIA: TANESCO to buy 19.16 MW of green electricity from six IPPs

By Inès Magoum - Published on December 14 2020 / Modified on December 14 2020

abriendomundo/Shutterstock" data-src="/proxy.php?image=https%3A%2F%2Fwww.afrik21.africa%2Fwp-content%2Fuploads%2F2020%2F12%2Fshutterstock_1464805487-800x400.jpg&hash=051e3b0f7fda1d5f598545cf47a53447" data-lb-sidebar-href="" data-lb-caption-extra-html="" data-single-image="1"> TANZANIE : la Tanesco va acheter 19,16 MW d’électricité verte à six IPP<img src=abriendomundo/Shutterstock" title="TANZANIE : la Tanesco va acheter 19,16 MW d’électricité verte à six IPPabriendomundo/Shutterstock" width="" height="" />

Six Independent Power Producers (IPPs) have just concluded power purchase agreements with the Tanzania Electric Supply Company (TANESCO). These private companies are developing renewable energy projects in Tanzania with a total capacity of 19.16 MW.​

The state-owned Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) is signing power purchase agreements (PPAs) with six independent power producers (IPPs) that are developing several renewable energy projects in Tanzania. TANESCO agrees to purchase 19.16 MW of electricity, under the supervision of the Energy and Water Regulatory Authority (EWURA) of Tanzania.

Among the selected IPPs is Nishati Lutheran Investment, which is implementing a 36-kW hydropower project at the Ijangala Falls in Makete. Similarly, Madope Hydro is implementing the 1.7 MW Madope Hydroelectric Project on the Madope River. Luponde Hydro is also signing a PPA with Tanesco for its Luponde hydroelectric project (9 kW) on the Luhololo River in Njombe. Lung’ali Natural Resources, which is implementing the Maguta hydroelectric project (1.2 MW) on the Lukosi River Falls in Kilolo, will sell its production to the utility.

Commercial operation in 18 months​

The other IPP selected is NextGen Solawazi which is working on a 5 MW hydropower project in the Kigoma Special Economic Zone. SSI Energy Tanzania, which is currently building a 10 MWp solar power plant in Kahama, will also sell its production to Tanesco. According to the public company, the six private companies will have to start marketing their production within 18 months.

In the meantime, TANESCO is developing other electricity projects in Tanzania. In this way, TANESCO is supporting the Tanzanian government’s policy of achieving a 75% electrification rate by 2035. Among its projects is the construction of the Rumakali and Ruhudji hydroelectric power plants which will have capacities of 222 MW and 358 MW respectively. In July 2020, TANESCO selected Multiconsult Norge AS, a Norwegian engineering consulting firm, to provide consulting services for the two projects.

My Take:
Japo mimi ni mwandishi wa habari, na sasa nimeisha staafu rasmi, lakini kwa vile kazi ya uandishi iko kwenye damu, hivyo ikitokea habari inahitaji ufuatiliaji, mimi nitaiweka tuu humu jf, wahariri watakao iona it's newsworthy, watatuma waandishi wao kuifuatilia, au waandishi watakaona ni habari, wataifuatilia, mimi nitakuwa nimetimiza wajibu wangu kwa jamii, ila ikitokea kweli ukawa ni ufisadi mwingine, utakuja kujulikana mwaka 2025 kabla ya uchaguzi ujao, nitakachokifanya ni kuwakumbusha tuu kuwa tulinusa, tukasikia harufu, tukauliza, na hayo ndio matokeo, ila pia, sio kila unaposikia harufu ya ufisadi ni ufisadi, harufu nyingine ni harufu tuu na hakuna ufisadi wowote, vitu vingine ni ukosefu tuu wa transparency, kama zile Bilioni 1.5 kwenye ripoti fulani ya CAG, watu wakadhani ni ufisadi, ikaja kukutikana hakuna ufisadi wowote.

Maswali ni haya.
  1. Kwanza maendeleo yoyote ya ujenzi wa mioundo mbinu wa umeme wa maji, ni maendeleo, endelevu, hivyo wakati Watanzania tukiusubiri huu umeme wa Stigler kuingizwa kwenye gridi ya Taifa, hakuna ubaya kwa Tanesco kuendelea kununua umeme toka kwa wazalishaji binafsi waliopo, kwa vile kuna wazalishaji wengi na mikataba imesimamishwa, kwa nini Tanesco wasiendelee nao na badala yake wanasani mikataba na wazalishaji wapya?. What is so special na hawa wapya, wakati wa zamani wapo, mikataba imesitishwa na wengine wametushitaki kwa kuvunja mikataba yao?
  2. Kama umeme wa Stigler, unatosha, hizi PPA's 6 mpya zinazosainiwa sasa ni za nini?.
  3. Kule nyuma tulivunja mkataba wa Dowans kwa tuhuma za ufisadi wa kulipishwa capacity charge kubwa na Tanesco kununua umeme wa bei juu toka kwa hawa IPPs na kuuza kwa bei ya chini!, Jee this time kwenye hii mikataba mipya jee Tanesco wananunua kwa bei gani per unit na kuuza kwa bei gani, tusije kuwa tunatwanga maji kwenye kinu?
  4. Baada ya kuvunjwa kwa mkataba wa Dowans, tulishitakiwa, tukashindwa kesi, tukadaiwa fidia iliyotwa Tozo ya Dowans, waheshimiwa wetu kule Bunge, wakajiapisha kwa maneno kama "over my dead body!" hatulipi! did you know what happened?....we paid every single cent kimya kimya na umeme ukapandishwa bei, Watanzania wote kwa ujumla wetu, tukafidia. Kitu cha ajabu sana katika hili, kampuni ile ile ya Dowans tuliovunja nayo mkataba, ikajibadili jina kujiita Simbion, mitambo ile ile, capacity charge ile ile, na mkataba ule ule, ikaingia tena mkataba na Tanesco, na tukakawa tunawalipa hadi JPM alipoingia, akaukataa ujinga huu, ndipo mkataba wa Simbion ukasitishwa na mpaka sasa kesi iko mahakamani, sijui tumefikia wapi! Kawa haya ndio mambo ya Tanesco na hizi PPA's zake, vipi hizi PPA's sita mpya are they clean?, transparent?.
  5. Kuna wakati kule nyuma, Tanesco ilikuwa inaelemewa na madeni ya umeme wa hawa PPA's na situation ya Tanesco kwa sasa ikoje hadi kuendelea kununua umeme kwa hawa wazalishaji binafsi, ili Tanesco ipate faida ni lazima inunue kwa bei ya jini na kuuza kwa bei ya juu, sasa kama Tanesco haina uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha, kwa nini hao wazalishaji binafsi wasiruhusiwe kuuza umeme wao direct kwa watumia kwa bei ya chini, wananchi ndio wafaidike?.
  6. Japo tunaelezwa Stigler ikikamilika Tanzania tutakuwa na umeme wa kutosha na ziada kuuza nje. Hawa jamaa wanasema "In the meantime, TANESCO is developing other electricity projects in Tanzania. In this way, TANESCO is supporting the Tanzanian government’s policy of achieving a 75% electrification rate by 2035", wakimaanisha huo mwaka 2035, Tanzania ndio tutafikisha 75% ya mahitaji yetu ya umeme!, sasa nani anasema kweli?, jee ni kweli tutajitosheleza na ziada kuuza nje, au tutajitosheleza kwa mahitaji ya sasa kwasabu bado hajaweza ku electrify nchi nzima, hivyo hiyo ziada tutakayouza nje, tutauza huku baadhi ya vijiji vyetu havina umeme kwasababu hatuna miondombinu ya kutosha ku i electrify nchi nzima?. Which is which?.

Paskali
Update
Habari yenyewe

TANESCO yasaini mkataba wa kununua umeme kwa wazalishaji wadogo​

KUSAINI MKATABA KATI YA TANESCO NA WAWEKEZAJI WADOGO

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeingia mkataba wa kununua umeme kutoka kwa wazalishaji wadogo wa kampuni sita binafsi, utakaoingia moja kwa moja kwenye kwenye gridi ya Taifa na kutumika katika maeneo mbalimbali Nchini.

Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini mikataba kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Meneja Mwandamizi Uwekezaji, Mhandisi Costa Rubagumya alisema wawekezaji hao wamekidhi vigezo kwa mujibu wa kanuni zilizoidhinishwa na EWURA.

"Kwa mujibu wa kanuni zinazosimamia uendelezaji wa miradi midogo ya kuzalisha umeme, inaitaka TANESCO kuingia mikataba na wazalishaji umeme wadogo kwenye maeneo ambayo gridi ya Taifa bado haijafika", alisema Mhandisi Rubagumya.

Aliainisha vigezo vingine ni maeneo ambayo yanatatizo la umeme mdogo ili kuimarisha ubora wa umeme na kigezo kingine ni maeneo ya usambazaji umeme ambapo njia za umeme za TANESCO ni ndefu hivyo kusababisha upotevu wa umeme.

Mhandisi Costa alizitaja kampuni hizo kuwa ni, Kahama Solar Power Project MW 10.0, Kigoma Solar Power MW 5.0, Nishati Lutheran (DKK) Investment Ltd MW 0.36.

Makampuni mengine ni, Madope Hydropower MW 1.7, Luponde Hydropower MW 0.9 na Maguta Hydropower MW 1.2.

Wakizungumza Kwa niaba ya Wazalishaji wadogo wa umeme, Padre Luciano Mpoma na Nicholas Richardson wameishukuru Serikali kupitia TANESCO kwa kukubali kufanya nao biashara ya umeme.

Waliongeza kuwa safari ilikuwa ni ndefu lakini hatimaye wamekuwa na furaha kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha nishati ya umeme inamgusa kila mwananchi.

Makampuni hayo yanatakiwa kuanza kuiuzia TANESCO umeme ndani ya miezi 18 kuanzia leo Disemba 08, 2020.

Update 2.
Mchango very constructive
Paskali, Ujinga wa Tanesco ni kung'ang'ania solar. Solar is a stupid alternative. Ni umeme unaozalishwa mchana tu! Kwa 10 MW huwezi nieleza kwamba utakuwa na storage yake kwa miaka 10. Kinachowashawishi saana ni rushwa. Ukiangalia kazi zote za solar TANESCO na REA wao huwapa makampuni binafsi maana ni kazi ambazo wao wenyewe hawawezi kuzifanya, hapo wana 10% yao.

Kuna kampuni kama CAMCO wanaojiita clean energy wamewashika utadhani ni taasisi ya serikali na kumejaa usanii tu! Inatia uchungu lakini sijui kuna nini hadi Kalemani na TANESCO hawasikii. Kalemani anaweza kuwa na immunity ya Chato lakini kwa kiwango kikubwa kabisa naweza kusema kuna ufisadi nyuma yake.
 
Bado nasisitiza uamuzi wa TANESCO ni safi kwasababu kubwa moja hii ku encourage private operators kusaidia uzalishaji wa power. Niliwahi kukaa kidogo Europe, nilishangaa nyumba tuliokuwa tukiishi mwenyenyumba alikuwa ameweka solar pannel zake nyingi sana juu ya mapaa ya nyumba zetu. Nikapata wasaa wa kuonge nae inakuwaje ana solar pannels nyingi vile na zinamsaidiaje?. Akaniambia zinamsaidia sana hasa kipindi cha kiangazi kwani kipindi hicho yeye huuza umeme kwa shirika lao la umeme. Kwahiyo kipindi hicho analipwa yeye badala ya yeye kilipia umeme. Hili nalo tulitazame hivi badala ya kuwa wagumu kuelewa na kuangalia the darkest part of TANESCO.
 
Mhandisi Costa alizitaja kampuni hizo kuwa ni, Kahama Solar Power Project MW 10.0, Kigoma Solar Power MW 5.0, Nishati Lutheran (DKK) Investment Ltd MW 0.36.

Makampuni mengine ni, Madope Hydropower MW 1.7, Luponde Hydropower MW 0.9 na Maguta Hydropower MW 1.2.

Wakizungumza Kwa niaba ya Wazalishaji wadogo wa umeme, Padre Luciano Mpoma na Nicholas Richardson wameishukuru Serikali kupitia TANESCO kwa kukubali kufanya nao biashara ya umeme.

Tuliambiwa Taasisi za dini zisijihusishe na siasa, hapa naona taratibu Yesu akiwekwa kando (...Padre Luciano Mpoma na Nicholas Richardson wameishukuru Serikali kupitia TANESCO kwa kukubali kufanya nao biashara ya umeme).

Labda sadaka hailipi
 
Paskali bila kupunguza ladha ya uzi wako, nilishangaa na kuchanganyikiwa kusikia kuwa huu mradi wa umeme wa SG hauko kwenye miradi ya umeme inayofahamika na TANESCO!
Hivi katika nchi yetu hii kuna Umeme wa SG ndugu yangu si kila jambo unatakiwa uchangie kama hujui jambo kaa kimya ufiche ukilaza wako.
 
Kwa taarifa yako uuzaji wa umeme kutoka kwa hao unawaita 'wamachinga' unaongozwa na kanuni maalumu zilizowekwa na muangalizi wa mambo haya, EWURA. Hata Tanesco bei yao ya umeme inaratibiwa/ridhiwa na EWURA. Suala la bei ya umeme ama kutoka kwa hao unaowaita 'wamachinga' ama TANESCO siyo suala la kusumbua 'akili' kiasi cha kuanza kuulizana bei ya umeme ya pande hizi mbili!

Nadhani hapa ndipo tunapoanza kupishana!!
===
Yaani lita za mafuta ya diesel zitakazotumika kusafirisha mzigo wa tani 10 kutoka (mfano) Dar kwenda Mbeya ni sawa na kiasi hicho kwa kusafilisha mzigo wa tani nane! Kwa taarifa yako ni kuwa gari likiwa limebeba mzigo mzito huwa linalazimika kutembea kwenye gia kubwa. Gia kubwa hufyonza mafuta zaidi, ili injini iwe na uwezo wa kuhimili mzigo huo. Gari likiwa na mzigo mdogo mara nyingi linatembelea kwenye gia ndogo kwani injini haihitaji nguvu kubwa hivyo haifyonzi mafuta mengi.

Mapungufu haya uliyoyaonyesha katika hili yana ua kabisa morali ya kuamini kuwa unatosha kabisa kufafanua suala lilipo mezani bila 'upendeleo'!

Kwa maelezo hayo hapo juu, nadhani wanaJF wataamua wenyewe ni nani wanamuona "... aidha yuko confused au anataka kwa makusudi ku confuse watu kwa lugha hiyo...."
Logic thinking inatakiwa izingatie ukweli. Siyo kweli kwamba ukiwasha generator lako la nyumbani litatumia mafuta machache kama utazima vifaa vyako vyote vya nyumbani na kubakiza taa chache za watts 5 kila moja. Siyo ukweli kwamba basi lako lenye uwezo wa kubeba abiria 60 kutoka Dar hadi Mwanza litatumia mafuta machache kama utabeba abiria 30. Kwamba kama linatumia mafuta ya lita 200 likiwa limebeba abiria 60 kwa hiyo likiwa limebeba abiria 30 litatumia mafuta ya lita 100; ni logics za vilaza wa hisabati za shule ya msingi watakaokuambia kuwa kilo moja ya mawe ni nzito kuliko kilo moja ya pamba.

Lengo letu hapa si kwa wana Jf kuamua. Lengo letu ni kuijulisha serikali kuhusu ufisadi katika shirika letu la umeme. Wameanza IPPs ndogo ndogo 6. Wataendelea na zingine na zingine, hatujui mwisho wake. Hata zile IPPs kubwa kubwa zitakuja. Tunarejea huko huko kwenye maumivu tuliyoyapata kutoka kwa IPPs za akina Songas, Simbion, Dowans, Rugemalila na yule singasinga.

Tunachosema ni kuwa shirika letu la umeme linaingia mikataba na IPPs hizi tukiwa:

1. Tuna umeme wa ziada wa kiasi cha 550MW zilizo iddle kwenye grid yetu ya taifa.

2. Tuna off grid standby power plants zenye diseal fired generators za kisasa kwenye maeneo yote Tanzania, zilizo na capacity ya jumla ya MW sisizopungua 200MW.

3. Tunaendelea na ujenzi wa hydro power plants huko Rusumo (180 MW), Kikongwe - Ruvuma (300 MW), Songwe - Mbeya (180 MW) na Julius Nyerere - Morogoro (2,115). Hydro power plants ambazo kwa ujumla wake zitatoa MW 2,775 zinatarajiwa kukamilika ndani ya miaka 2 ijayo na kuingizwa kwenye grid ya taifa. Hivyo tuki assume kwamba ndani ya miaka 2 ijayo kama matumizi yetu ya umeme yatabaki kama yalivyo sasa, grid yetu ya taifa itakuwa na umeme wa ziada ulio iddle wa kiasi cha MW 550 + 2,775 = 3,325 MW. Ni umeme mwingi sana ambao utakuwa hauna wateja na utakuwa umekaa tu iddle.

Tunachosema ni kuwa shirika letu la umeme linachotakiwa kufanya ni kuhangaika kupata soko la kuuza huo umeme ulio iddle. Na soko kuu ni kwa sisi watanzania. Watuuzie kwa bei ndogo. Wakipunguza sana bei zao, umeme huo utauzika hapa hapa nchini. Wangaliweza hata kutupa bure kuliko kuuacha iddle.

Tatizo kubwa ni kwamba wafanyakazi wa tanesco hujigawia umeme bure. Ndiyo maana hawajui machungu ya bei zao za umeme. It is high time now wafanyakazi wa tanesco watakiwe kulipa umeme wanaotumia majumbani kwao. Mbona madaktari na manesi wakiugua hawajitibu bure? Mbona walimu watoto wao walikuwa hawasomi bure? (kabla ya jpm kusomesha watoto wote bure). Mbona wafanyakazi wa mamlaka ya kodi wanalipa kodi? (sina uhakika kama wanalipa). Mbona mapolisi wanaokamata watu nao hukamatwa? Mbona maaskari wa magereza nao hufungwa magerezani? Kwa nini hawa wafanyakazi wa tanesco wajigawie umeme uliotokana na jasho (kodi) letu wote wao wanajichotea bure? Halafu wanatuletea figisu figisu wa umachinga kwenye umeme wetu.

Serikali ichukue hatua dhidi ya wahusika katika mikataba hiyo ya kifisadi ndani ya tanesco. Sasa ni muda muafaka bei ya umeme ianze kupunguzwa. Kupunguza kwa bei ya umeme itachochea sana ukuaji wa uchumi wa nchi yetu. Nina uhakika bei ya umeme ikipunguzwa hadi kuwa TSh 50 kwa unit, kasi ya kuongezeka kwa ukuaji wa uchumi wa nchi yetu itakuwa kubwa sana na kutuwezesha kuwa nchi ya uchumi wa kati wa juu (high middle income country) ifikapo 2025 kama ilivyolengwa kwenye ilani ya uchaguzi ya ccm ya 2020 - 2025.
 
2. Tuna off grid standby power plants zenye diseal fired generators za kisasa kwenye maeneo yote Tanzania, zilizo na capacity ya jumla ya MW sisizopungua 200MW.
Asante kwa ufafanuzi wako na pia kumradhi kwa kuchelewa kujibu bandiko lako. Nimelisoma lote. Kikubwa hapa, mengine 'gentlemanly' tukubaliane kutokukubaliana.

Hata hivyo, msingi wa hoja yangu ya kuunga mkono TANESCO kuingia mikataba hiyo sita ni kuwa hatua hiyo, kama nilivyoeleza awali, inaambata na utekelezaji wa maelekezo yaliyo katika sera ya Nishati nchini ya mwaka 2015. Maelezo ambayo ni kuongeza matumizi ya nishati jadidifu ( renewable energy) katika matumizi ya jumla ya nishati nchi. Tanesco wana tekeleza sera hiyo ambayo kama nchi tuliikubali kuifuata.

Pia nimeishaeleza kuwa Tanzania imeridhia utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu(sustainable development goals i.e. SDGs). SDGs hizi zinahusisha lengo namba saba linalohimiza kuongeza matumizi ya nishati jadidifu.

Faida za matumizi ya nishati jadidifu zimeelezwa ikiwemo kupunguza athari hasi ya mabadiliko ya tabia nchi yaani kwa kupunguza gesi za ukaa hewani zinazoongeza joto duniani. Na athari za mabadiliko hasi ya tabia nchi yameishaonekana. Gesi za ukaa uharakisha sana mabadiliko haya hasi ya tabia nchi. Na chanzo kikuu cha gesi hizi ni matumizi ya nishati ya ukaa yaani " fossil fuel" kwa lugha ya kimombo. Fossil fuels moja wapo ni mafuta ya dizeli, ambayo umeeleza kuwa bado Tanzania tunazalisha umeme wa 200 MW( takwimu hii sikuwa nayo) kwa kutumia mafuta haya. Kwa sera na malengo tuliyokubali kuyafuata juu ya matumizi ya nishati jadidifu, hizi 200 MW inabidi ziondolewe kwenye ukokotoaji wa matumizi ya Nishati nchini. Tanesco wameanza kupunguza 19 MW ( kama ulivyoeleza) kutoka hiyo 200 MW kwa kuingia mikataba sita ya uzalishaji wa nishati jadidifu. Kwa taarifa yako tu, tunafikiria sasa kupata umeme kutoka kwenye gesi ya Hydrogen kwa kuchakata maji endapo upembuzi yakinifu utaonyesha kuwa Tanzania ipo kwenye nafasi ya kufaidika na teknolojia hiyo. Teknolojia hii inaangukia kwenye teknolojia za nishati jadidifu. Kwa hiyo andaa mashambulizi yako sawa sawa!

Sasa, Mkuu, kwa kuhitimisha, kama hukubaliani na kinachofanywa na serikali kupitia TANESCO juu ya uongezaji wa matumizi ya nishati jadidifu, basi kwa ustaarabu na utaratibu makini unatakiwa uanze kampeni ya kwanza kubadilisha sera ya nishati ya mwaka 2015 ili iakisi matakwa yako ya kupinga matumizi ya nishati jadidifu; pili uanze mkakati wa kuishawishi serikali ijitoe kwenye utekelezaji wa SDGs. Mimi nakuahidi kuwa nitakupinga kwa nguvu zote usifanikiwe mpango wako huo kwa sababu faida za matumizi ya nishati jadidifu ni kubwa sana kwa ustawi endelevu wa uwepo wa binadamu duniani.
 
Mkuu Kuna Mambo mengi sana mmekaririshwa tu, mfano Katiba mpya,sijui tume huru ya uchaguzi,demokrasia etc. Matatizo ya nchi za Africa karibu zote hasa za watu weusi ni yaleyale. Matatizo ya watu weusi waliobakia nje ya Afrika ni yaleyale karibu nchi zote kuanzia USA, Brazil,Papua New Guinea,Jamaica etc. Turudi Afrika mashariki. Mnadai Kenya Wana tume huru na katiba mpya mbona kabla ya uchaguzi uliopita kiongozi wa tume ya uchaguzi aliokotwa kafa na kidole gumba cha kutumika kwenye mfumo wa fingerprint kimekatwa!?.. Africa ni umafia tu. Ndo maana wengine tunaamini kwenye watu sio vyama. Hata uweke katiba ipi,tume ipi, mfumo upi as long as ni hizi nchi zetu za watu weusi kama kiongozi aliyepo sio mkali Mambo ni yaleyale. Mimi hutakaa uniaminishe eti Chadema ikiingia madarakani maisha ya watanzania yatabadilika. NEVER. WHY!??.. Hulka ya wanaoongoza ni ile (Selfish,roho mbaya,njaa,asili ya umaskini,majivuno, ulimbukeni nk) na wanaoongozwa hivyo hivyo(njaa,umaskini, ujinga, kukosa Elimu,kupenda ngono,kuzaana hovyo nk). Hata ije CDM,CUF,ACT,CHAUMA as long as viongozi ni weusi na wanaoongozwa ni weusi NO CHANGES. So, wengine tunamuona angalau JPM ana moyo wa kukemea na kumaanisha. Sasa kumuamini au kutomuamini inabaki kwa mtu binafsi. Kama dini vile.
Pamoja na juhudi za kumwimbia mapambio, Jiwe kaenda zake akiwa amelowa damu mwili mzima na kabeba mzigo wa manung'uniko na laana kutoka binadamu, watz wenzie.
Kama huo ukandamizaji na unyanyasaji, ndio moyo wa kukemea na kumaanisha uliyotaka kutuaminisha, basi mtazamo wako UTAENDELEA kutia shaka sana. AMEN
 
Back
Top Bottom