Siasa za UCHUMI au UCHUMI wa kiSIASA??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa za UCHUMI au UCHUMI wa kiSIASA???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fikirikwanza, Jun 25, 2012.

 1. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ndugu WanaJF, Nalima pamba kwa nguvu zote baada ya kuambiwa kuwa bei ya pamba itakuwa TZS 1500/-kwa kilo. Zao linastawi, ninakopa kuweka mbolea na dawa kuua wadudu. Pamba yangu inapendeza sana.

  Inafika wakati wa kuuza pamba, serikali ile ile inashuhudia nauza pamba kwa TZS 500/- tu, haina jibu hata kidogo. DC alinihimiza nilime pamba kila kaya heka 2 kwenda juu, sasa simwoni tena DC wa RC wala aliyewatuma kazi, sio hata yule tarishi wa katikati waziri wa kilimo au biashara.

  Je hii ni siasa ya uchumi au uchumi wa siasa?? huu uchumi wa siasa utatufikisha wapi?? nani awajibike kwa hadaa hii kwa wananchi na hasara hii kwa familia??? Mbunge wangu naye ni mwoga bungeni anapitisha kila kitu isipokuwa makato ya kodi kwenye mshahara wake.

  Kijijini kura tumpe CCM tena???? Akiambulia sufuri atupige mabomu??? Tukibisha tumebisha liwalo na liwe hongereni sana Shy CCM 4 CDM 7; hapo ndo mwanzo wa kuachana na CCM bila vurugu.

  Nawasilisha
   
Loading...