Siasa za Tanzania za vyama vyote zimefikia hali mbaya sana ya chuki, ubabe, kukomoana, kusalitiana, kutukanana, kudharauliana na hata kuuana!

Hizo ni hisia zako kwa Chadema Chadema kinahitaji mabadiliko kodogo sana haswa upande wa uzoefu wa kidiplomasia
Nyanja zingine Chadema kiko sawa na kama kuhusu visasi sidhani kama chadema kitalipiza kisasi ila kitaacha sheria zichukue mkondo wake
Mbona kwenye chama chenu ukitofautiana na mkubwa unatimuliwa bila hata kuhojiwa.? We kweli we hujielewi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana, lakini tumefikia mahali ambapo, Chadema hata wakirekebisha wakashinda, CCM hawatakubali kuacha uadui na Chadema. Kwa hiyo Chadema watakuwa wameshinda lakini Tanzania kama nchi haijashinda. Ndio maana nikasema toa CCM, toa Chadema toa utitiri wa hivi vyama vyote yeboyebo vya siasa, tuanze upya.

Unajua hii mentality ndio ikimweka Macron madarakani kule Ufaransa? Na huenda ndio maana CCM wanaogopa sana mgombea huru - kwa kuwa ana uwezo wa kushindwa kwa kuonyesha mapungufu ya CCM na upinzani na watu wenye akili wakamwelewa na kuachana na hivi vyama vilivypo.
Sisi kama Watanzania CCM imekuwepo kwa miongo mingi tunaijua vizuri tunasema hivi Asante ccm lakini tumekuchoka sana sana tuache tuichague Chadema nayo tuiangalie itatufikisha wapi sasa kama ccm ikijifanya kama inahati miliki ya kuongoza Nchi kwa nguvu ndipo inapoharibu kwa mfano ccm inatumia milioni 400 za walipakodi kununua Diwani wa Chadema mmoja
 
Sio wote wabaya.
Hili pia ni jambo ovu sana kuwachanganya wabaya na wazuri kapu pamoja.
Hata kama kweli wote ni waovu chagua basi aliye muovu kidogo ukilinganisha na wenzake.
Mkuu, unapaswa kuelewa jinsi ya kushughulika na tatzizo katika system. Hapo unakuwa unashughulika na "mentality" ya system, sio mtu moja mmoja. Ndio maana hata watu humwambia Magufuli tengeneza system sio kushughulika na kutumbua mtu mmoja mmoja kila siku - utumbuaji hautaisha. Hebu niambie, utaanzaje kuwatoa wabaya ndani ya CCM au Chadema? Utasababisha mgogoro mkubwa hata zaidi. Ona kilichotokea CCM walipoanza kushughulika na Membe, Kinana, Makamba nk. Na Chadema kuwafukuza Wabunge "wasaliti"? Je hayo yanajenga au kubomoa?

Hapa tunafanya mambo kisayansi - siasa za Tanzania zinahitaji system upgrade, sio kurekebisha sehemu moja moja. Hiyo ni kazi kubwa na siyo effective. Embe likioza sehemu sehemu, utakuwa salama zaidi kutokula funza kwa kulitupa lote, sio kula sehemu unazodhani hazina funza, kwa kuwa funza wakiwa sehemu nzuri za embe wanaonekana kama nyama ya embe!
 
Chadema Ndio waasisi wa matusi, dharau, kiburi wakiongozwa na wanasheria wao

Jiwe ndio kapandikiza chuki ndani ya nchi hii maana sio kiongozi kwa maana ya kiongozi bali mlevi madaraka.
 
Hali ya siasa za Tanzania ni ya kutisha sana, na vyama vyote vya siasa vina hatia, CCM kama chama tawala na vyama vya upinzani. Imefikia mahali ambapo kuna chuki, ubabe, kukomoana, kusalitiana, kutukanana, kudharauliana na hata kuuana, sio tu kati ya chama tawala na vyama vya upinzani, bali pia ndani ya vyama vyenyewe, CCM na vyama vya upinzani.

Imefikia wakati wanasiasa wanapoongea unaona wazi maneno ya chukii, ubabe dharau nk dhidi ya wanasiasa ndani ya chama chao wenyewe au kuelekezwa kwa watu wa chama kingine, ambao ni Watanzania kama wao, na wote wanadai wapo katika siasa kwa ajili ya maslahi ya Watanzania.

Cha kusikitisha zaidi, ni kwamba Watanzania tumekubali kama vipofu kuongozwa na watu wa namna hii, na hata kushangilia na kushabikia pale wanapofanya au kutamka mambo ambayo yanaendeleza chuki na mengine mabaya kati yetu. Hivi tumerogwa na nini hadi kufikia hapa tulipo? Ile Tanzania ya watu wenye kupendana, walioitana "ndugu', waliosifika duniani kote kwa amani na umoja, imeenda wapi? Imefikia mahali tunaruhusu hawa wanasiasa wasababishe chuki kati yetu na wanandoa wetu, ndugu zetu wa ukoo, wapenzi wetu, jirani zetu, rafiki zetu na wala hilo hatulioni!

Watanzania ni lazima tufikie mahali tuamke, na kutambua kwamba wanasiasa wa vyama vyote nchini wameamua kuwa viongozi wenye akili iliyotawaliwa na chuki, ubabe nk katika kuendesha siasa zao. Hakuna siasa tena Tanzania, ni vurugu tupu zilizojaa ulevi tu wa kutaka kuhodhi madaraka kwa njia yeyote ile. Kinachoendelea sio tena wanasiasa kujinadi kwa ubora wa sera zao, bali ni wanasiasa kujinadi kwa kuonyesha ni jinsi gani wanasiasa fulani ndani ya chama chao au chama kingine wanapaswa kudharauliwa, kuchukiwa, kubezwa na ikiwezekana hata kuuliwa!

Enzi za nyuma hata tuliimba "Sisi tunataka kuwasha mwenge, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo mahali ambapo pana chuki, heshima ambapo pamejaa dharau". Je ndicho wanasiasa wetu wanafanya? Tutaimbaje mwenge umulike hata nje ya mipaka yetu na kuleta mambo haya wakati hapa kwetu hayapo na wala hatuyajali tena? Karibu viongozi wetu wote wa siasa katika ngazi zote, kila wakifungua midomo yao utakachosikia ni dharau na chuki. Tumaini gani hilo wanalotupa?

Kuna vitabu vya dini vimeandika juu ya sifa za watu katika nyakati fulani, kuwa watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, watukanaji, wasio na utakatifu; wasio na ubinadamu, wasiopenda kusuluhishwa, wachonganishi, walafi, wakatili, wasiopenda mema; wasaliti, wasiojali kitu, waliojaa majivuno. KIla nikisoma maneno haya naona kama yaliandikwa kwa ajili ya wanasiasa wa Tanzania. Na haya nayaona katika wanasiasa wote wa Tanzania, kuanzia CCM, Chadema, NCCR, TLP nk, kuanzia viongozi wa juu hadi wa chini.

Hivi kweli Watanzania tumekuwa vipofu kiasi kwamba hatuoni haya katika wanasiasa wetu? Kwa nini tunakubali kuwa mashabiki wasio na akili kwa ajili ya watu wa namna hii ambao kwa unafiki wanajifanya wako katika nafasi zao kwa ajili ya kututumikia?

Watanzania wenzangu, tunahitaji mambadiliko makubwa katika nchi yetu. Tunahitaji msukumo mkubwa wa kuwakataa hawa wanasiasa wote ambao sio tu wanazidi kuwa vipofu wa kutuongoza sisi tuliokubali kuwa vipofu kama wao, bali wanaiangamiza nchi yetu. Tunahitaji tuake chini na kuwaonyesha kwamba hatutaki tena watu wa namna hii kujiita viongozi wetu. Tunahitaji kurudisha udugu wetu na amani ambayo ndizo zilikuwa sifa zetu kuu.
Kutoka hapa tulipo panahitaji Reformation ktk System ya Siasa za nchi yetu!! Siasa ya nchi yetu imekosa mvuto kbsa!! Raila odinga ni rafiki wa Kenyatta Ila kwetu mbowe ni adui wa JPM!! Duuuh,, Pengine mgombea huru asiye na Chama labda linaweza Kuwa ni suruhu kwa hii Siasa ya nchi yetu!!! But the situation is worse!!

Yap! Na mimi naona tunahitaji mgombea huru kuwa raisi ili atuunganishe wote bila kujali vyama!
 
Hali ya siasa za Tanzania ni ya kutisha sana, na vyama vyote vya siasa vina hatia, CCM kama chama tawala na vyama vya upinzani. Imefikia mahali ambapo kuna chuki, ubabe, kukomoana, kusalitiana, kutukanana, kudharauliana na hata kuuana, sio tu kati ya chama tawala na vyama vya upinzani, bali pia ndani ya vyama vyenyewe, CCM na vyama vya upinzani.

Imefikia wakati wanasiasa wanapoongea unaona wazi maneno ya chukii, ubabe dharau nk dhidi ya wanasiasa ndani ya chama chao wenyewe au kuelekezwa kwa watu wa chama kingine, ambao ni Watanzania kama wao, na wote wanadai wapo katika siasa kwa ajili ya maslahi ya Watanzania.

Cha kusikitisha zaidi, ni kwamba Watanzania tumekubali kama vipofu kuongozwa na watu wa namna hii, na hata kushangilia na kushabikia pale wanapofanya au kutamka mambo ambayo yanaendeleza chuki na mengine mabaya kati yetu. Hivi tumerogwa na nini hadi kufikia hapa tulipo? Ile Tanzania ya watu wenye kupendana, walioitana "ndugu', waliosifika duniani kote kwa amani na umoja, imeenda wapi? Imefikia mahali tunaruhusu hawa wanasiasa wasababishe chuki kati yetu na wanandoa wetu, ndugu zetu wa ukoo, wapenzi wetu, jirani zetu, rafiki zetu na wala hilo hatulioni!

Watanzania ni lazima tufikie mahali tuamke, na kutambua kwamba wanasiasa wa vyama vyote nchini wameamua kuwa viongozi wenye akili iliyotawaliwa na chuki, ubabe nk katika kuendesha siasa zao. Hakuna siasa tena Tanzania, ni vurugu tupu zilizojaa ulevi tu wa kutaka kuhodhi madaraka kwa njia yeyote ile. Kinachoendelea sio tena wanasiasa kujinadi kwa ubora wa sera zao, bali ni wanasiasa kujinadi kwa kuonyesha ni jinsi gani wanasiasa fulani ndani ya chama chao au chama kingine wanapaswa kudharauliwa, kuchukiwa, kubezwa na ikiwezekana hata kuuliwa!

Enzi za nyuma hata tuliimba "Sisi tunataka kuwasha mwenge, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo mahali ambapo pana chuki, heshima ambapo pamejaa dharau". Je ndicho wanasiasa wetu wanafanya? Tutaimbaje mwenge umulike hata nje ya mipaka yetu na kuleta mambo haya wakati hapa kwetu hayapo na wala hatuyajali tena? Karibu viongozi wetu wote wa siasa katika ngazi zote, kila wakifungua midomo yao utakachosikia ni dharau na chuki. Tumaini gani hilo wanalotupa?

Kuna vitabu vya dini vimeandika juu ya sifa za watu katika nyakati fulani, kuwa watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, watukanaji, wasio na utakatifu; wasio na ubinadamu, wasiopenda kusuluhishwa, wachonganishi, walafi, wakatili, wasiopenda mema; wasaliti, wasiojali kitu, waliojaa majivuno. KIla nikisoma maneno haya naona kama yaliandikwa kwa ajili ya wanasiasa wa Tanzania. Na haya nayaona katika wanasiasa wote wa Tanzania, kuanzia CCM, Chadema, NCCR, TLP nk, kuanzia viongozi wa juu hadi wa chini.

Hivi kweli Watanzania tumekuwa vipofu kiasi kwamba hatuoni haya katika wanasiasa wetu? Kwa nini tunakubali kuwa mashabiki wasio na akili kwa ajili ya watu wa namna hii ambao kwa unafiki wanajifanya wako katika nafasi zao kwa ajili ya kututumikia?

Watanzania wenzangu, tunahitaji mambadiliko makubwa katika nchi yetu. Tunahitaji msukumo mkubwa wa kuwakataa hawa wanasiasa wote ambao sio tu wanazidi kuwa vipofu wa kutuongoza sisi tuliokubali kuwa vipofu kama wao, bali wanaiangamiza nchi yetu. Tunahitaji tuake chini na kuwaonyesha kwamba hatutaki tena watu wa namna hii kujiita viongozi wetu. Tunahitaji kurudisha udugu wetu na amani ambayo ndizo zilikuwa sifa zetu kuu.
Unadhani nini chanzo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unadhani nini chanzo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mmh, sijakuelewa Mkuu. Chanzo cha chuki? Ubinafsi tu. Na zaidi ni tasnii ya siasa kuingiliwa na watu wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, watukanaji, wasio na utakatifu; wasio na ubinadamu, wasiopenda kusuluhishwa, wachonganishi, walafi, wakatili, wasiopenda mema; wasaliti, wasiojali kitu, waliojaa majivuno
 
Back
Top Bottom