Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,142
- 18,769
Hali ya siasa za Tanzania ni ya kutisha sana, na vyama vyote vya siasa vina hatia, CCM kama chama tawala na vyama vya upinzani. Imefikia mahali ambapo kuna chuki, ubabe, kukomoana, kusalitiana, kutukanana, kudharauliana na hata kuuana, sio tu kati ya chama tawala na vyama vya upinzani, bali pia ndani ya vyama vyenyewe, CCM na vyama vya upinzani.
Imefikia wakati wanasiasa wanapoongea unaona wazi maneno ya chukii, ubabe dharau nk dhidi ya wanasiasa ndani ya chama chao wenyewe au kuelekezwa kwa watu wa chama kingine, ambao ni Watanzania kama wao, na wote wanadai wapo katika siasa kwa ajili ya maslahi ya Watanzania.
Cha kusikitisha zaidi, ni kwamba Watanzania tumekubali kama vipofu kuongozwa na watu wa namna hii, na hata kushangilia na kushabikia pale wanapofanya au kutamka mambo ambayo yanaendeleza chuki na mengine mabaya kati yetu. Hivi tumerogwa na nini hadi kufikia hapa tulipo? Ile Tanzania ya watu wenye kupendana, walioitana "ndugu', waliosifika duniani kote kwa amani na umoja, imeenda wapi? Imefikia mahali tunaruhusu hawa wanasiasa wasababishe chuki kati yetu na wanandoa wetu, ndugu zetu wa ukoo, wapenzi wetu, jirani zetu, rafiki zetu na wala hilo hatulioni!
Watanzania ni lazima tufikie mahali tuamke, na kutambua kwamba wanasiasa wa vyama vyote nchini wameamua kuwa viongozi wenye akili iliyotawaliwa na chuki, ubabe nk katika kuendesha siasa zao. Hakuna siasa tena Tanzania, ni vurugu tupu zilizojaa ulevi tu wa kutaka kuhodhi madaraka kwa njia yeyote ile. Kinachoendelea sio tena wanasiasa kujinadi kwa ubora wa sera zao, bali ni wanasiasa kujinadi kwa kuonyesha ni jinsi gani wanasiasa fulani ndani ya chama chao au chama kingine wanapaswa kudharauliwa, kuchukiwa, kubezwa na ikiwezekana hata kuuliwa!
Enzi za nyuma hata tuliimba "Sisi tunataka kuwasha mwenge, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo mahali ambapo pana chuki, heshima ambapo pamejaa dharau". Je ndicho wanasiasa wetu wanafanya? Tutaimbaje mwenge umulike hata nje ya mipaka yetu na kuleta mambo haya wakati hapa kwetu hayapo na wala hatuyajali tena? Karibu viongozi wetu wote wa siasa katika ngazi zote, kila wakifungua midomo yao utakachosikia ni dharau na chuki. Tumaini gani hilo wanalotupa?
Kuna vitabu vya dini vimeandika juu ya sifa za watu katika nyakati fulani, kuwa watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, watukanaji, wasio na utakatifu; wasio na ubinadamu, wasiopenda kusuluhishwa, wachonganishi, walafi, wakatili, wasiopenda mema; wasaliti, wasiojali kitu, waliojaa majivuno. KIla nikisoma maneno haya naona kama yaliandikwa kwa ajili ya wanasiasa wa Tanzania. Na haya nayaona katika wanasiasa wote wa Tanzania, kuanzia CCM, Chadema, NCCR, TLP nk, kuanzia viongozi wa juu hadi wa chini.
Hivi kweli Watanzania tumekuwa vipofu kiasi kwamba hatuoni haya katika wanasiasa wetu? Kwa nini tunakubali kuwa mashabiki wasio na akili kwa ajili ya watu wa namna hii ambao kwa unafiki wanajifanya wako katika nafasi zao kwa ajili ya kututumikia?
Watanzania wenzangu, tunahitaji mambadiliko makubwa katika nchi yetu. Tunahitaji msukumo mkubwa wa kuwakataa hawa wanasiasa wote ambao sio tu wanazidi kuwa vipofu wa kutuongoza sisi tuliokubali kuwa vipofu kama wao, bali wanaiangamiza nchi yetu. Tunahitaji tuake chini na kuwaonyesha kwamba hatutaki tena watu wa namna hii kujiita viongozi wetu. Tunahitaji kurudisha udugu wetu na amani ambayo ndizo zilikuwa sifa zetu kuu.