Siasa za Tanzania, unaweza ukacheka, ukadondoka ukazimia kisha ukafa!

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,429
Yaani kuna watu walisema Mzee Kikwete ni dhaifu, fastjet, na kila aina ya lawama. Kila aliemtetea akaitwa mchumia tumbo na kila jina baya. Alivyostaafu watu wale wale wakaanza kumsifu.

Mara Mzee Kikwete, akaingia bungeni juzi juzi, waliomponda hapo awali kwa juhudi zao zote, wakaimba kwa nguvu zao zote na sauti nzito. Tumekumisi! Tumekumisi! X100! Kikwete fadhwahikatu' fi twabasam!

Mara juzi tena watu wale wale wakaibuka kwa shangwe bungeni. Haieleweki vizuri furaha yote ile ilitokana na nini. Mara wimbo ukaanza. Tunaimaniiii na kikweteee! Oya oya oya!x 300

Mara kamati ya makinikia inatoka. Mara watu wale wale wanasisitiza Mzee Kikwete awe miongoni mwa watakaoshitakiwa. Mara Mh.Rais Magufuli anaagiza kuwa Mzee Kikwete aachwe apumzike , Mara watu wale wale wanakazania ni lazima ashitakiwe. Hatimaye round nyingine mtanange unaanza.

Ukifuatilia siasa za nchi hii na ukiwa na kumbukumbu nzuri unaweza ukacheka kama mwendawazimu.
 
Bungeni wanasutana umbea tu...mle asilimia kubwa ya watu wanaopatikana wana elimu ya kujua kusoma na kuandika tu. Wanaojua zaidi ya hapo wapo wachache sana...hivyo kusababisha kutoonekana ktk kuchangia michango yenye maslahi kwa umma. Bunge lingevunjwa tu, warudi mtaani tufanye uchaguzi upya
 
Hata hao wasomi pia hawana msaada wowote kwa taifa
 
Back
Top Bottom