Siasa za Tanzania ni kwa Wasomi au Matajiri?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Wasomi wengi sasa wapo katika Siasa za Tanzania,Matajiri pia,na nguvu kisiasa hutegemea uwezo wa mhusika.Je Siasa za Tanzania zimejikita kwa Watu wa aina hiyo?
 
Nilikuwa najiuliza siku nyingi hata mpaka sasa sijapata jibu yakinifu la kwanini wasomi wetu wengi (wanazuoni) wanaobahatika kubaki hapa nchini wanajiingiza kwenye siasa?. Kwani kwenye siasa kuna nini mpaka wasomi hata wale ambao bado wapo kwenye fani zao wanalilia kila siku kuingia kwenye siasa? Jamani nisaidieni kwa hili ili baadae tuweze kuinusuru nchi yetu.
 
nilikuwa najiuliza siku nyingi hata mpaka sasa sijapata jibu yakinifu la kwanini wasomi wetu wengi (wanazuoni) wanaobahatika kubaki hapa nchini wanajiingiza kwenye siasa?. Kwani kwenye siasa kuna nini mpaka wasomi hata wale ambao bado wapo kwenye fani zao wanalilia kila siku kuingia kwenye siasa? Jamani nisaidieni kwa hili ili baadae tuweze kuinusuru nchi yetu.

wasomi wa leo si wale wa zamani, kule kwenye fani kunahitaji akili zaidi na vitendo kwa sana.huku kwenye siasa ni mdomo tu.
 
Hakuna kazi ya maana ila kuna pesa nyingi sana na misamaha mingi ya kodi ya kibiashara,pia ukhdhulumu viwanja na mashamba kesi zinaisha kiaina.
 
wasomi hawana thamani tena kwa muono wa wanasiasa, elimu yao haitumiwi, ndio maana wanakimbilia kwenye siasa ambako kuna mshiko bila kujishughulisha.
 
Nilikuwa najiuliza siku nyingi hata mpaka sasa sijapata jibu yakinifu la kwanini wasomi wetu wengi (wanazuoni) wanaobahatika kubaki hapa nchini wanajiingiza kwenye siasa?. Kwani kwenye siasa kuna nini mpaka wasomi hata wale ambao bado wapo kwenye fani zao wanalilia kila siku kuingia kwenye siasa? Jamani nisaidieni kwa hili ili baadae tuweze kuinusuru nchi yetu.

duh mpaka leo ujajua kwenye siasa kuna nini au ni unafiki umekujaa.....kwani mpaka watoto wadogo wanajua siasa inalipa vya kutosha
 
Wamegundua kuwa siasa ndiyo inayolipa siku hizi hapa Bongo. Taaluma haziheshimiwi tena
kwani kila kitu kinafanywa na wanasiasa. Mungu ibariki Tanzania
 
kwa sababu hata ukidevelop theories haziwezi work out kwa kuwa hakuna political will...

wanafunzi wanapokuuliza sasa kwa nini mambo hayaendi?

na wewe ni mtu mzima unakosa jibu...

inabidi usonge golini....ndicho walichofanya kina kaguta na kagame...
 
hizi thread za namna hii naona zimekuwa nyingi hapa JF, kwanza tatizo sio kwanini wasomi? tatizo ni hao wasomi wanaitumiaje elimu yao kwenye siasa ya nchi yao? kwenye siasa kunaweza kusiwe na maslahi na bado wasomi wakapakimbilia kwa sababu tu ya uzalendo wa kutumikia wenzao, kinyume chake ni sahihi kwa sababu ya uvivu na ubinafsi.
 
mshahara wenyewe ndio huu,nani hataki milioni saba kila mwezi,mkopo milioni tisini,posho kibao
 
Simple logic, jifanye una masters yako ya ualimu uliyopata pale UDSM na unafundisha pale Ilboro high school, unalipwa shilingi 450000 kwa mwezi, unatembea kwa miguu au unapanda daladala kwenda kazini na kurudi, halafu unaishi nyumba ya vyumba vitatu ambayo umepanga na unajilipia kodi mwenyewe kwa kuwa serikali haina uwezo wa kukulipia kodi. Inatokea siku unakutana na rafiki yako aliyefeli darasa la saba au form four, akaamua kuingia kwenye biashara na baadaye siasa. Anakwamba analipwa 12,000,000/= kwa mwezi na anadrive shangingi lake, pia anaishi kwenye hekalu ambalo amejenga kwa hela ya mkopo aliyopewa bungeni, wewe utaona sababu gani ya kuendelea kuwa kwenye profession yako?
Msomi wa Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika hana thamani kabisa mbele ya mwanasiasa. Kwa hiyo namna nzuri ya msomi naye kufaidi keki ya taifa ni kuingia huko wanakofaidi wengine.
 
Kwa sababu alichokisoma katika fani yake akielewi, ndio maana anaona akapige domo ili ajipatie pesa kirahisi. inashangaza kuona Prof.
mwenye fani ya Medicine anaenda kujiunga na siasa na kukaa bar kusia fani yake, wakati ilitakiwa muda huo aupoteze katika mahabara
kufanya utafiti wa dawa kwani uwezo wa kuvumbua dawa tanzania upo kutokana mahitaji mengi kuhusu utafiti wa dawa upo.
Utafiti na uvumbuzi ni kitu kinachoitaji muda mwingi sana. na hao Maprof. wetu sio wavumilivu kwa hilo.
 
Nilikuwa najiuliza siku nyingi hata mpaka sasa sijapata jibu yakinifu la kwanini wasomi wetu wengi (wanazuoni) wanaobahatika kubaki hapa nchini wanajiingiza kwenye siasa?. Kwani kwenye siasa kuna nini mpaka wasomi hata wale ambao bado wapo kwenye fani zao wanalilia kila siku kuingia kwenye siasa? Jamani nisaidieni kwa hili ili baadae tuweze kuinusuru nchi yetu.

Ndugu yangu Wilson, ni maslahi manono tu, hakuna kingine
Jaribu kufikiri katika mstari huu: Daktari ambaye ni specialist, awapo zamu ya masaa 24, say kwenye kitengo cha wajawazito na uzazi, ambaye anafanya zaidi ya operesheni 15 kwa masaa hayo, bila kulala, na wakati mwingine kula mara mbili ama moja kwa siku kwa kukosa muda, mwisho wa siku analipwa 10,000 Tsh, tena kwa hospitali kubwa kama Muhimbili. Kisha compare na mwanasiasa huyu ambaye kwa kukaa bungeni, na kugonga meza, kwa siku moja (masaa 8 at top) anaingiza Tsh 150,000 nje ya mshahara. Wakati yule daktari mshahara wake baada ya makato ni tsh 800,000, huyu mwanasiasa anakunja kiulaini >12mil. Wakati huyu daktari atasota kutafuta mkopo wa ki-bito chake na asipate maana hakopesheki, mwanasiasa anapatiwa Mil 90 tena hatatakiwa kuzilipa zote. Sasa hata ukiwa na uzalendo wa aina gani kweli utabakia kwenye fani yako,..kwanini usiende nawewe kujaribu bahati kama sio kusepa kabisa ili ukatoe huduma kwa watakaokuthamini?..sad as it looks, mtaalamu huyu atatakiwa kutoa huduma tu maana ni wito..mwanasiasa anasahau kuwa kazi ya uwakilishi ndo wito wa kwanza duniani..maana umetumwa na watu,..tena maskini..
 
Back
Top Bottom