Siasa za Tanzania na Televisheni ya Taifa-TBC

BJEVI

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
1,359
251
Wana jf ni wazi kuwa demokrasia TZ itadhoofishwa na inaendelea kudhoofishwa daima na chombo tunachokiita TBC.


UPENDELEO WA WAZI NDO DHIMA YAO HASA LINAPOKUJA SUALA LA KAMPENI mfano mzuri ni IGUNGA.

Kwa kuwa chombo hiki kinaendeshwa kwa kodi za wananchi ni halali kufanya haya???
 
Chombo kile(TBC) hakiwezi kuendeshwa kwa uweledi being fair and free kutokana na nafasi za kuteulliwa za uongozi wa juu,kila anayeenda pale jambo la kwanza anafikiria kumfurahisha/ridhisha aliyemteua. Nafasi za kuteuliwa ktk idara nyingi za serikali ndo mwanzo wa mafindo findo unayoyaona, mathalani,,angalia mkuu wa tume ya uchaguzi, mkuu wa polisi (IGP), wakurugenzi n.k
 
Hata taarifa ya habari inayoihusu Chadema huwa imechakachuliwa, hawapendi kuisema vizuri Chadema. Ikiwa ccm imefanya madudu kwenye kampeni huwa hawatangazi yao.
 
TB CCM wagonjwa hao achana nao, vilaza hatakai c kwa TV tu. katiba ijika watajua wanawajibika kwa nani maana kwa sasa wana-dhana ya kuwa wawajibika kwa CCM wapuuzi wapuuzie tu
 
Hiyo chanel imepoteza sifa za kuwa chanel ya taifa kwani inaupendeleo wa wazi sana sijui watajificha wapi siku nuru itakapoliangaza taifa hili, hawajifunzi hata yanayotokea nchi za jirani!!!!
 
Mbona hakuna jipya hapa maoni ni yale yale kila siku.
Hivi hamjui kuwa TBC ni chombo cha serikali. Na serikali inaundwa na CCM?
 
Mkuu hulazimishwi kuangalia TBC vituo vya television viko vingi sana mazee
 
Mkuu hulazimishwi kuangalia TBC vituo vya television viko vingi sana mazee
Hivi wee unaona ni sawa mtu aache kuangalia TV ya Taifa kwasababu tuu halazimishwi? ana haki ya kuhoji kwasababu TBC ni chombo cha Kitaifa na kinatumia kodi hata za watu wasio wanaCCM, ni muhimu TBC wabadirike hii siyo Taasisi ya CCM.
 
Wana jf ni wazi kuwa demokrasia TZ itadhoofishwa na inaendelea kudhoofishwa daima na chombo tunachokiita TBC.


UPENDELEO WA WAZI NDO DHIMA YAO HASA LINAPOKUJA SUALA LA KAMPENI mfano mzuri ni IGUNGA.

Kwa kuwa chombo hiki kinaendeshwa kwa kodi za wananchi ni halali kufanya haya???


Mkuu hili si swali. Ni wazi kabisa kuwa inapofika wakati wa Kampeni CCM inatumia vyombo vvya habari vya serikali na wapinzani hawatumii kama CCM wanavyotumia. Je ni halali au si halali, hili si swali, ila ni hali halisi. Kwa hiyo opposition ijifunze kupambana katika hali kama hii....

TBC ni mfano mzuri wa ahli ya sasa ya Tanzania. Professional mzuri kama Tido anafanya kazi kubwa na kuleta mabadiliko makubwa, mtu kama makamba anakuja kumfukuza. kwa ufupi si sehemu ya professionalism.
 
Hata siku moja vyama vya upinzani na wanaharakati kwa ujumla wao wasitegemee fadhila za mama wa kambo.

Taasisi zote za umma zinaitikia amri ya mteuzi wao lakufanya nikuweka mikakati ya kuanzisha vyombo vyao vya habari nadhani uwezo wanao na sapoti kutoka kwa wadau wao wataipata.
 
Cjapenda jinsii TBC inavyotumiwa kwa kupendelea chama tawala na ukiangalia kwa yanayojili kule Igunga taarifa zao ni kutoka CCM na CUF tu basi...cjui bana lkn wajue ya kwamba kituo kile kinaendeshwa na kodi za watz wote bila kujali itikadi zao za vyama na cdhani kama wako tayari kubadilika....any way time will tell.
 
TBC ni sawa sawa na kipindi cha kibonde Clauds FM,so usitegemee hata siku moja watakiongelea vibaya CHADEMA wakitoa habari zao basi utaona ni za viongozi wa chadema kukamatwa na hata gazeti la Tanzania Daima na Mwanahalisi marufuku kulisoma pale kwenye uchambuzi wa magazeti
 
Tbc haina habari nyingine zaidi ya kusifia ccm,kuna habari nyingine wao hawaonyeshi kabsa,nyingi zikiwa zinahusu upinzani
si channel ya kutegemea kupata habari zilizo fair
 
Mara ntingi inatokea endapo aliyeteuliwa hafiti kwenye ile position huwa lazima ajikombe.
 
Katiba mpya ndio suluhisho la kila kitu. Tuisimamie kwa nguvu zetu zote ili tuitawale nchi yetu wenyewe kwa matakwa yetu na si ya hawa dhalimu wachache
 
Back
Top Bottom