Siasa za Tanzania na kufuru ya ufananisho wa mbinguni

mkwapuaji

Member
Jan 6, 2012
46
95
Wana jamvi habarini za muda huu...
Naomba niweke dukuduku langu kwa siasa za Tanzania za sasa ambazo zimeanza kunifanya nijitathmini kiimani.
Kama wengi mnafuatilia mtaona kuna kauli nyingi za kumnenea kiongozi wetu mambo asiyoyanena ama yatakayomfanya aikufuru imani yake. Hii ni hasa baada ya kuona cheo cha makamu wa Mungu kumbe kiko Tanzania kiasi kuona kuna mahusiano baina ya siasa zetu na mbinguni.

Sijaelewa mtu kumwita Mwenyezi Mungu Baba na kusema fulani ni baba mdogo yaani yeye ni mdogo wake Mungu kweli? Na inakuwaje anaenda kuombewa kama huwa anaombewa au iweje ahudhurie nyumba za ibada angali angeweza wasiliana na ndugu yake tu.
Mbaya zaidi mtu mwengine anadiriki kusema huyu ndiye mwakilishi wa mwenyezi Mungu ...... Yaani mpaka nakereka kwa kufuru wanayomtendesha huyu kiongozi.

Kitabu cha imani yangu kinasema zitiini mamlaka zilizowekwa lakini hazikusema wenye mamlaka ni wadogo zake Mungu ama ni wawakilishi wa Mungu bali wanayafanya yale yampendezayo Mungu kwa kuwa ama wameteuliwa au wamechaguliwa na watu naye akishasema sauti ya watu ni sauti ya Mungu. Hivyo basi tunapaswa kumweshimu kiongozi wetu na kumuunga mkono lakini hatupaswi kumfananisha na Mungu kwani Mungu alikuwako, yupo na atakuwako dahari na dahari wewe na miaka yako kadhaa ulimwengu huu ni kiasi gani cha nafasi unaichukua katika umri wa mwenyezi Mungu mpaka ufananishwe naye?......
 
dafity

JF-Expert Member
Aug 16, 2008
1,771
2,000
Neno BABA maana yake MLEZI. Sio lazima afanye ngono na mama yako.

Kusema MWAKILISHI WA MUNGU hakuna kosa. Kwani ukitoa Sadaka anapokea Mungu? Basi huyo anayepokea na kuzitumia ndio mwakilishi wake. Tuliza akili
Wana jamvi habarini za muda huu...
Naomba niweke dukuduku langu kwa siasa za Tanzania za sasa ambazo zimeanza kunifanya nijitathmini kiimani.
Kama wengi mnafuatilia mtaona kuna kauli nyingi za kumnenea kiongozi wetu mambo asiyoyanena ama yatakayomfanya aikufuru imani yake. Hii ni hasa baada ya kuona cheo cha makamu wa Mungu kumbe kiko Tanzania kiasi kuona kuna mahusiano baina ya siasa zetu na mbinguni.

Sijaelewa mtu kumwita Mwenyezi Mungu Baba na kusema fulani ni baba mdogo yaani yeye ni mdogo wake Mungu kweli? Na inakuwaje anaenda kuombewa kama huwa anaombewa au iweje ahudhurie nyumba za ibada angali angeweza wasiliana na ndugu yake tu.
Mbaya zaidi mtu mwengine anadiriki kusema huyu ndiye mwakilishi wa mwenyezi Mungu ...... Yaani mpaka nakereka kwa kufuru wanayomtendesha huyu kiongozi.

Kitabu cha imani yangu kinasema zitiini mamlaka zilizowekwa lakini hazikusema wenye mamlaka ni wadogo zake Mungu ama ni wawakilishi wa Mungu bali wanayafanya yale yampendezayo Mungu kwa kuwa ama wameteuliwa au wamechaguliwa na watu naye akishasema sauti ya watu ni sauti ya Mungu. Hivyo basi tunapaswa kumweshimu kiongozi wetu na kumuunga mkono lakini hatupaswi kumfananisha na Mungu kwani Mungu alikuwako, yupo na atakuwako dahari na dahari wewe na miaka yako kadhaa ulimwengu huu ni kiasi gani cha nafasi unaichukua katika umri wa mwenyezi Mungu mpaka ufananishwe naye?......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom