Tusemezane
New Member
- Jun 2, 2017
- 1
- 0
Nilikuwa nikishangaa na kujiuliza aina ya ushabiki wa soka hasa kwa timu zetu kubwa Yanga na Simba bila kupata majibu!
Nchi nyingi duniani zinazo timu ambazo ni wapinzania wa jadi, lakini upinzania huo hauifanyi timu moja kuifanyia hujuma timu pinzani pindi inapotetea taifa lake kwa kucheza na timu kutoka nje ya nchi husika. Kwetu hapa Tanzania imekuwa kinyume chake
Kwamba Yanga inapoiwakilisha Tanzania na kucheza na timu nyingine kutoka nje, basi wapenzi na mashabiki wa Simba wataishangilia timu ya kutoka nje bila kujali kuwa Yanga inaliwakilisha Taifa lao kwa faida yetu sote. Hali hii imekuwa hivyo vivyo kwa Wapenzi na mashabiki wa Yanga dhidi ya Simba
Upinzania wa timu hizi umechukua nafasi hadi timu yetu ya Taifa inapocheza. Utaona mashabiki wa Yanga wanawashangilia wachezaji wao na kuwazomea wachezaji wa Simba ndani ndani ya timu ya Taifa na mashabiki wa Simba kufanya vivyo hivyo. Kila shabiki wa Simba anamuombea mchezaji wa Yanga afanye vibaya katika mchezo husika, bila kujali kuwa kama mchezaji huyo ni kipa basi tutakuwa tumefungwa goli ambalo ni athari kwetu sote kama timu ya taifa.
Watu wengi tumekuwa tukilalamikia na kulaumu mwenendo huu kwamba haulinufaishi soka la nchi yetu, na hata timu kutoka nje ya nchi dhidi ya time zetu zimekuwa zikishangazwa na aina ya mashabiki wa Tanzania.
Sasa tunao upinzani wa kisiasa katika nchi yetu, ambapo tabia hii ya mashabiki wa soka kati ya Simba na Yanga imeonekana ni dhairi waTanzania tunayo hadi kwenye masuala muhimu ya nchi yetu. Kwamba mambo fulani kwa masilahi ya kitaifa yakifanywa na upande wa chama cha upinzani basi upande wa chama tawala watalibeza na kulipinga, na hali inakuwa vivyo hivyo jambo lenye tija likifanywa na upande wa chama tawala basi wapinzania watalibeza na kulipinga.
Kule bungeni hali hii inajidhihirisha wazi kabisa kwa pande zote hasa upande wa chama tawala kubeza michango yenye tija inayotolewa na wale wa upande wa upinzani. Na hii ndiyo ilipelekea upitishwaji wa mikataba ya kinyonyaji kwa wawekezaji dhidi ya taifa letu. Michango yote mizuri ya wapinzania kupinga unyonyanyi huu ilipingwa na wale wa chama tawala na mikataba hiyo ikapitishwa kwa wingi wa wabunge wa chama tawala.
Majuzi na sasa tunashuhudia Mh Rais akifanya usimamiaji wa mali za nchi hii katika sakata la michanga ya madini, jambo ambalo ni nadra kulisikia kutoka kwa viongozi wengi wa kiafrika. Lakini hali imekuwa vivyo hivyo, kwamba kwa vile limefanya na mtu kutoka chama tawala, basi wale wa kutoka upinzania wakalizomea na kulibeza.
Wengine wamefika mbali sana wakionyesha dalili zote za kuombea Rais ashindwe (tufungwe goli) katika sakata la michanga ya madini bila kujali kuwa jambo hili analifanya kwa masilahi ya taifa zima na kwamba kushindwa kwake tutakuwa tumeshindwa sote na itakuwa gharama na hasara kwa taifa zima.
Watanzania tutakuwa watu wa ajabu sana kufanya upinzani wa aina ya Simba na Yanga kwenye mambo muhimu ya taifa letu eti kisa ni pande tofauti za itikadi za kisisasa.
Lakini hatujachelewa, tunayo nafasi ya kurekebisha hali hii ambayo inaanza kuota mizizi, hasa kwa serikali kuwawezesha( Facilitation) wananchi wote kuiona Tanzania ni ya kwao na hivyo kuwa pamoja katika kuitetea nchi yetu bila kujali suala husika linasimamiwa au kuendeshwa na mtu kutoka upande fulani wa itikadi ya kisiasa.
Nawasilisha