Siasa za Tanzania bwana! Zitto Kabwe anapambana kuudhoofisha upinzani! so Amazing!

H.T.P

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,163
2,000
Ujue mi kuna wakati napata mashaka sana na Zito kabwe, hivi ni kiumbe wa aina gani? yaani yeye wenzake wakihangaika kuutafuta ukombozi wa taifa lao yeye yuko busy kuwarudisha nyuma! hii nayo inanipa mashaka kama kweli huyu ni mtanzania.

Ni ajabu sana Dr Slaa alipokua CHADEMA zito alikua hampendi akisema anatumia vibaya madaraka, leo akisikia kuna mtu anamkosoa Dr zito tena anamshambulia huyo mtu, kwasababu tu Dr kanunuliwa CCM basi kawa rafiki wa zito! sasa zito umesimama wapi? ujue unapoteza credibility yako...Wewe hufai hata kuwa Msimamizi wa mradi wa kuku kama ndo ulivyo ndumi la kuwili
 

mzalendoact

Member
Jun 22, 2015
87
0
Wewe ndo hufai. Tuamini lipi Dr. Slaa kanunuliwa au mbowe kauza chama. Kabla ya kumsema mwenzio anapoteza credibility jiulize wewe ulishawahi kuwa na chembe ya hiyo credibility? Tunamuunga mkono slaa kwa maana ya misingi. Ukombozi unaoletwa kwa gharama ya kuacha misingi ni sawa na ule wa makaburu wa Afrika kusini 1910 na Zimbabwe 1963. Wewe kama unaona huo ndio Ukombozi achana na ambao tunaona hilo ni changa la macho. Otherwise think of making yourself credible before your talk about others loosing credibility.
 

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
23,567
2,000
Kwani ni uongo kusema Chadema ni ccm b.?

Hivi mnafikiri nchi nzima tunaweza kununuliwa na Lowassa?

Mbona Lowassa kahamia Chadema Lakini hatusikii ccm wakimwita msaliti zaidi ya kupambana naye majukwaani.

Sasa nyie yeyote anapingana na nyie anaitwa msaliti.

Siku mkija kuacha kutumia akili za mbowe ndio mtamwelewa Zitto.
 

Kitoabu

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
5,964
2,000
Ujue mi kuna wakati napata mashaka sana na zito kabwe, hivi ni kiumbe wa aina gani? yaani yeye wenzake wakihangaika kuutafuta ukombozi wa taifa lao yeye yuko busy kuwarudisha nyuma! hii nayo inanipa mashaka kama kweli huyu ni mtanzania.

Ni ajabu sana Dr Slaa alipokua Chadema zito alikua hampendi akisema anatumia vibaya madaraka, leo akisikia kuna mtu anamkosoa Dr zito tena anamshambulia huyo mtu, kwasababu tu Dr kanunuliwa CCM basi kawa rafiki wa zito! sasa zito umesimama wapi? ujue unapoteza credibility yako...Wewe hufai hata kuwa Msimamizi wa mradi wa kuku kama ndo ulivyo ndumi la kuwili[MENTION][/MENTION]
Kwanini usianze kupatwa na shaka na mwenyekiti wako? Ambae alitembea nchi nzima akituaminisha wa TZ kua Lowasa ni fisadi papa nchi hii, naleo anarudi tena kwa wananchi na kuwaambia kua Lowasa ndio mabadiliko?!

Haumpendi Zitto kwa majungu yako tu

Nakumkubali mtu au kutokumkubali ni uamuzi wa mtu, hivyo sina budi kuheshimu hisia zako.KITO
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom