Siasa za Nje, Balozi zetu na Safari ya Simba Zimbabwe kwa mafukara wa Lengthen.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa za Nje, Balozi zetu na Safari ya Simba Zimbabwe kwa mafukara wa Lengthen....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Iga, Mar 17, 2010.

 1. I

  Iga Senior Member

  #1
  Mar 17, 2010
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  IMEWAHI kuzungumzwa katika makala za Jumapili za Insha za kaka Makilla-ambaye incidentally namheshimu kama kisima cha fikra angavu, mpya na zenye kumjali Mtanzania wa kawaida kwamba ni vizuri balozi zetu huko nje zingelifikiria kuwa na HOSTELI INAYOPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA.
  Hosteli hiyo pamoja na kwamba itakuwa inaendeshwa kibiashara lakini itakuwa ni nafuu mno kwa Mtanzania yeyote anayetembelea nchi husika.

  Humo katika hosteli kutakuwa na vyumba safi vya kulala; maduka, sehemu za kufanyia kazi za kiofisi na kumbi ndogo za mikutano ya kitaaluma na kibiashara.

  Kungelikuwa na hoteli, baa na vile vile vyumba au suite ambayo mtu anaweza akajipikia mwenyewe.

  Aidha kila chumba kitakuwa na kompyuta iliyounganishwa na intaneti, redio na televisheni kwa matumizi binafsi ya mgeni.

  Hii ina maana, kwa mfano, Simba walivyofika Harare wasingesumbuka hata kidogo maana wangelikuwa wameshafanya booking zao Ubalozini na wanasubiriwa kupata huduma sawa na nyumbani.

  Hosteli hizo hazitakuwa kwa ajili ya wanamichezo tu bali hosteli hizo tarajiwa- zitawafaa pia wanafunzi wa muda mfupi wanaofika huko nje; wagonjwa wa muda mfupi; wafanyabiashara; walimu na wahadhiri wa vyuo vikuu wanaofika pia kwa muda mfupi; na bila kusahau watumishi, maofisa serikali na viongozi wetu ambao hawatakuwa na mashauzi na watakubali kuishi katika hosteli yetu wenyewe huko nchi za nje.

  Harare na Lengthen ni changamoto mpya kwa Bw. Membe kulifanyia mchakato jambo hili haraka iwezekanavyo. Hili ndio jibu moja kwa utandawazi, je, tunasubiri nini?
   
 2. R

  RAY DONOVAN Senior Member

  #2
  Aug 22, 2016
  Joined: Jul 2, 2015
  Messages: 144
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 60
  duh

  kazi kweli kweli
   
Loading...