Siasa za Mzumbe hazijengi! Mzumbe kuna Tatizo: Elimu inashuka, Ufisadi unatamalaki

bhikola

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,130
1,660
Heshima mbele wana JF

Kuna WIZI na UFISADI mkubwa umetokea katika pesa zetu tunazochanga kama ada ya association, Siwezi pita vumbi wakati lami ipo.... Rais ambaye anatakiwa kuondoka madarakani anafahamika kama MOSES MOMBA (DISSERTATION) amekwapua fedha taslimu 32,000,000 (wanafunzi 1,600 ada 20,000) katika akaunti na ushahidi ukiwepo maana tulimuandikia barua wabunge tukiomba hesabu za mwaka hakujibu kabisa. Rais huyu anafanya mambo mengi ambayo inasemekana anasapotiwa na menejiment.

Hakuna chuo kina matatizo Dar kama Mzumbe, hakuna chuo wanafunzi wa masterz wanateseka kama mzumbe, hakuna library ya kutosha,hakuna bookshop, hakuna sehemu za kusomea, hakuna stationary za kutosha,hakuna AC za kueleweka, msimbazi center ndio kero wanafunzi wamekuwa kama watumwa wa ada (mamilioni) wanayolipa.....tulitegemea pesa yetu ya MUSO iweze kutufuta machozi ila mtu mmoja (MOMBA) akishirikiana na mmoja kati ya lecturers wa menejiment wametafuna pesa zetu...


Demokrasia inabakwa waziwazi: kwa mfano FRED NGAJIRO...huyu ndie mwanafunzi aliyeshinda urais ili ampokee momba kijiti ila mpaka leo hajaapishwa!!!!!!!!!!!!!! Je unajua sababu,,,,,,,, Ngajiro ni mwanaharakati mzuri sana na mpenda amani aliahidi kuweka kila kitu sawa ila inasemekana haelewani na MOMBA na ndio sababu hataki kumuapisha kisa mtu aliyemuweka yeye anaitwa JOHN D. NGOWI ambaye alishindwa*Si unajua gari linalovutwa haliwezi kuovertake.... NGOWI alikuwa mshindi wa tatu ila aliappeal matokeo kwa kushinikizwa na MOMBA kuwa atapewa URAIS kwa sharti la kutochunguza shillingi 32,000,000 ...Hivi sasa Ngajiro anaishi kwa vitisho vikubwa na manyanyaso mengi maana hili linasemekana kwa habari zisizo rasmi linasapotiwa na PROF MBWAMBO...sasa hatujui kama mkuu nae ni mshiriki katika huu mchezo...Ila tumeanza kupoteza imani nae kama habari zake za kwenye jamii forum.

KWANINI RAIS TULIYEMCHAGUA HAAPISHWI MPAKA SASA,SIKILIZA, tunaamin Menejiment ina buy time ili tumalize mitihani wamuapishe JOHN NGOWI kwa ushawishi wa Momba...wanataka kuweka Rais wao sasa kwanini walitupotezea
muda wa kupiga kura...NDUGU zangu sisi ni wasomi tukikubaliana na hili tutakuwa hatujitendei haki, Classreps tunawatesa ilibid wapewe hata allowance ya vocha tu ambayo ni ndogo sana........ Momba aliilipa electro cometteeya watu watatu sh 30,000 kila mtu na alitoa hela kwenye walet, je pesa ya umoja ndio inatolewa bila kusainiwa? NDUGU unaijua hiyo bajeti aliyosema ilitumika!!!!!!! AIBU AIBU AIBU TUPUUUUUU!!!!! Mimi ni mmoja kati ya classreps ndio maana najua uchungu wa ile pesa yetu....MOMBA amekula pesa ya intake yao 2010 amekula yetu ya 2011 na kuna uwezekano anataka kula na ya 2012....je huu woga ni halali yetu watu wa level ya masters!!! katiba inasema rais anaongoza kwa mwaka mmoja tu...

WAKATI ANAJUA HATA PA KUSOMEA CHUO HAKUNA nini maana ya kutuwakilisha kisa sisi sio classmates wake,alikubali sera ya kulipa vitabu kisa yeye hakuchajiwa maana alikuwa dissertation,alikubali wenzake wakapangiwa dissertation supervisors wa morogoro na mpaka leo wanalia maana wanaishi Dar, tunadai hela za vitabu 250,000 huwa hana hata time....MTU HUYU HANA TOFAUTI NA UKIMWI maana ANAUA BILA AIBU Mmzumbe ya Dar inadharaauliwa na kuitwa VODA FASTA YA PROF MBWAMBO, maana uongozi wake umekosa busara walimu wanafundisha kiswahili, mwalimu mmoja anasimamia dissertation watu 80 jaman tunashindwa kuiga mazuri kutoka kwa wenzetu...Tunaanza kujilaumu kusoma mzumbe tena ya Dar ya Prof. Mbwambo.

Jamani kwa sasa tutegemee kupangiwa supervisors wa morogoro na kutorudishiwa 250,000 za vitabu,,,Ngajiro alishinda kura madarasa yote ya msimbazi yaliyopiga kura Je aliwapa Rushwa?nhakuna mtu hata mmoja ambaye alifika nusu yake katika urais sasa appeal zinatoka wapi... HAPA TUNAHITAJI BUSARA YA VC KABISA MAANA PROF MBWAMBO ANATUFUNDISHA TUWE MABALOZI WABAYA WA MZUMBE....

Wenzetu wa procurement saa10 hawakupiga kura kwa sababu kubwa MOMBA aliwadharau siku ya uchaguzi pia aliwaambia HATA WASIPOPIGA KURA WATATAWALIWA TU ila yeye amelipotosha hili, poleni sana ndugu... MOMBA aliwahi kusema WANAWAKE WA MZUMBE NIWACHAFU SANA (wengine wakiwa ni mama zake kabisa) mbele ya darasa la MPA ya asubuhi na wote ni mashahidi na ndio sababu wanamchukia...

Hiyo ndiyo hali halisi ya Mzumbe University Dar cumpus, wanajamvi ushauri please, tunafanyaje ili kupata kwanza haki yetu, na pili elimu iliyo bora kama tulivyotarajia!

Pia natoa rai kwa watu wa PCCB, vyombo vya habari, na wapinga ufisadi wafike chuoni hapo wapate cha kuiambia jamii ili ielewe kinachoendelea, pia hatua stahili zichukuliwe. Kamati za bunge kama ile ya zito ya mashirika ya umma huwa inafika vyuoni kweli?? maana hiki ni chuo cha umma, nafikiri kuna haja ya kuvitazama kwa upya. Jamani hela zetu zinaliwaaaaaaaaaaaaaaaaa

Nawasilisha
 
Umeelezea vizuri na kwa uzalendo matatizo yanayowakabili.
Matatizo ya aina hii yapo vyuo vingi vya elimu ya juu, they usually take an advantage that wanafunzi ni watu wa kupita kwa hiyo hakuna atakayefuatilia michango na mapato ya taasisi.
Lakini kila taasisi ina taratibu zake.
Nashauri utaratibu uzingatiwe ili kupata ukweli na kuchukua hatua ikiwamo kuibua mambo haya katika vikao vyenu.
 
kazi mnayo tatizo your too soft to act..ishue kama hii ingetokea pale MLIMANI mgesikia moto wake ila mzumbe mnapenda kusifiwa sana kama chuo cha amani hakina fujo matokeo yake wanawatia vidole machoni sasa komaeni maybe one day utoto wa mama utawatoka mtaanza kuchukua action
 
Kama hali halisi ni hii kama ilivyoelezwa hapo juu bila shaka mamlaka ya vyuo vikuu pamoja na shirikisho umoja wanavyuo nchini (TAHILISO) inapaswa kuingilia ilikuchunguza hali halisi na hatua madhubuti inapaswa kuchukuliwa dhidi ya vitendo viovu kwa wote wanaohusika na ikiwezekana kutazama upya mwenendo na utendaji wa menegimenti ili kukinusuru chuo hichi ambacho kimejibebea heshima ndani na nje ya nchi kwa miaka mingi sasa.
 
.....siamini kama wanazuoni wanaweza endeshwa kwa jinsi ulivyoeleza, na kama ni kweli, basi ninyi ni mazoba na mnachokutana nacho toka kwa momba ni astahili yenu...mwanazuoni hujikomboa mwenyewe...wa nje humuunga mkono kwa kumuhamasisha...vita dhidi ya ufisadi wa momba ni yenu wana mzumbe, hapa ilitakiwa mtupe taarifa ya namna harakati zinavyoendelea...ww na sijui mngesimama wapi wakati wa ukoloni!!!!
 
same to UDSM DARUSO IMEOZA na vijana wa ccm wametumwa wanaanza ufsadi wakiwa wachanga kwe sias
 
Wanafunzi wa mzumbe masters yenu ipo chini sana kila mtu hata vilaza wengi waliotoka CBE na TIA wanaikamata bila ya matatizo
 
tatizo pale mzumbe dsm campus kuna program za masters tu(hakuna undergraduate) na most of the students wanatoka makazini na wako off-campus hivyo wana muda mdogo wa kujishugulisha na issue za students association ,wengi wanakimbizana na kufukuzia pesa mtaani na baadae shule hivyo ultimately solidarity hakuna.
 
Wahusika wataupata ujumbe mkuu maana naamini wengine wapo JF..Ila kamanda kwakua wewe ni CR mfunge paka kengele, naamini kuna watu walitoa pesa ya vitabu yote ya semista ya 1 na ya 2, wakapewa vitabu vya semista ya 1 tu.. wanasubiri 1 aanzishe ili nao wakurupue, wapo waliolipia vitabu semista ya 1 ila hawakuchukua maana vilikuja vimechelewa.. nao wanasubiri wa kulianzisha tu, wapo waliochoshwa na mwenendo mzima wa siasa za Mzumbe.. nao wanasubiri mtu aanzishe.. na wapo wenye kero zao na ma DR wanaojua kukomoa badala ya kufundisha eg. Dr Barongo.. nao pia wanatafuta mtu wa kulianzisha..CR unaweza anzisha kitu na watu tukafuata, hebu tujaribu kiongozi afu uone tunavowakimbiza, pata uthubutu wa kusimama mbele na kusema imetosha au tuma mail kwenye mail ya group ili mapambano yaanze!! VITA NI VITA, HATA YA MANENO NI VITA PIA..
 
wewe FRED NGAJIRO acha kunangania utu wa madaraka tena inaelekea wewe ni kibaraka wa CCM umebakiza week mbili tuu uondoke consecrate kwenye mitihani acha kungangania madaraka...Kwa jinsi nilivyosoma maelezo yako unamchamfua Momba na Prof Mbwambo kwa sababu ya kutaka kungangania madaraka...mimi ni mwanafunzi mwenzio hapa chuoni...uliingia kwenye kinyanganyiro cha madaraka bila kuangalia katiba inasema nini na mpaka sasa katiba imekufunga unaona uanze kuchafua watu...hii si mara ya kwanza Prof. Mbwambo kuchafuliwa bali kumbuka hata raisi wa nchi hii watu wanasema mengi lakini kuna mazuri anayoyafanya...pia kumbuka ukiona wanakusema sana ujue wamekukubali...Hongera Momba ndio unakuwa kisiasa ndio mambo ya siasa yalivyo...huwezi kukubalika kwa kila mtu...Bravo Rais wetu Momba kuongoza kwa miaka miwili imeonyesha ni jinsi gani ulivyo na upeo mkubwa wa madaraka...
 
MZUMBE DAR CAMPUS NI SIASA TU HAKUNA ELIMU PALE, Ukiwa na hela utafanyiwa Coursework zote na hata Thesis na maprofesa wa pale! Uongozi wa pale upo kipesa zaidi na sio kutoa elimu kwa jamii.
 
duh huyu jamaa hachokagi asee akiwa advance pale galanos tanga alichukua fomu za uraisi akapigwa chini kwasababu alionekana ni mtu aliye na msimamo wa tofauti sana kwanza jamaa hachekagi hovyo,namkubali sana alikuaga room mate wangu pale room namb 13 mkonge floor ya juu
 
oooops kumbe ni Mzumbe ya Dar! nilidhani ni hapa kwetu Changarawe, Mkongeni, Vikenge hadi Sangasanga! Poleni sana.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom