Siasa za" Mohamed Said" ni za kusimuliwa na upotoshaji

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Wanabodi, Kuna msemo unasema" knowing your risk exposure is better than living with good expectation "

Hii kauli hutafsiriwa sio rasimi kama ni bora ukafahamu Madhara unayoweza yapata kuliko ukapuuza na kuamua kuishi kwa matumaini au kutegemea mambo mazuri

Mohamed Said amekuwa akiishi hii kauli humu jamii forum lakini akiitekeleza kinyume chake kwenye maandishi yake

Habari zake zote ni hearsay au habari za kusikia na kusimuliwa, Hivi kila mtu akiamua kusimulia habari za Babu yake jinsi alivyoshiriki vita ya kwanza ya dunia nadhani vitabu havitatosha, Miaka ya 1990 na mwanzoni ya miaka ya 2000 kila Mzee alisimulia alishiriki vita ya kwanza ya dunia, Mzee yupi mkweli?

Habari zake zote ni brainwashed au habari za mtu aliyejazwa fikra mfu, Fikra ambayo hawezi kutoka nje ya uelewa binafsi, Yale aliyeyojazwa kuwa waislam wanaonewa yeye ndie ameyabeba bila kuchuja kuonyesha waislam wanaonewa bali walifanya kazi kubwa ya uhuru, Hivi kama uislamu ulihubiri ukombozi kuna watu makatili dunia hii kama waarabu, Leo hii uarabuni Saudi, Omani ni maeneo ya manyanyaso na mateso kwa watu weusi

Habari zake nyingi ni outdated au zilizopita na wakati na kukosa ushawishi kwa kundi la vijana, Amejitahidi kubadilisha Mada ya Professor kabudi kumshauri Makonda atafute na kupambanua maeneo ambayo wapigania uhuru waliishia au pata mafunzo hapa nchini, Yeye amekuja na story za Abdul sykes alizosimuliwa

Ushauri:
Hakuna utafiti unaofanywa kwa hearsay au kusimuliwa kama wa Mohamed Said, Utafiti ni hatua, Sio kila simulizi ya kwenye vituo vya kahawa au msikitini lazima ulazimishe watu kuviamini, Jiulize kwanini watu wanaweza kutetea habari za Mkwawa wa wahehe lakini sio story zako za kwenye vitabu vya Abdul Sykes

Kuendekeza udini karne hii ya ishirini na moja umekwisha chelewa sana, Hii kazi ilikupasa kuifanya wakati nchi ikiitwa Tanganyika, Unaowahubiria humu wengi wamezaliwa ndani ya uhuru tukiitwa Tanzania, Mohamed Said bado anaishi karne ya ishirini, Amegeuka mmisionari akitengeneza Propaganda za miaka ile Wamisionari wanagawa nguo huku wakibeba madini na dhahabu
 
Mkuu acha kuchafua watu na wewe lete historia y'all nchi kwa kadri unavyoifahamu tuipime Kama ya mzee moh'd said n ya kupotosha

Hoja hujibiwa kwa hoja unabaki kumsema mzee wa watu wakat wewe huweki historia unayoifahamu
Historia ya kusimuliwa, Unajua pale Peramiho Mission Abate wa kwanza ni Litimbandyosi Mwakifuna, na alikuwa Babu yangu akitokea Nanjilinji,

Khaa kweli hii dunia hizi shule za kata ni shida sana, Huyo hana anachojua zaidi ya kusimuliwa mara na mtoto wa Abdul sykes, mara mkewe, Kuna mtu atasimulia ujinga wa mzazi wake?

Binadamu kazi yetu ni kusifia familia zetu
 
Hata abasia ya peramiho ina historia yake na wazee ndio huwa wanatusimulia ukweli

Hebu muheshimu huyo mzee bana Binafs sioni tatzo lake sababu sijaona mtu mwingne aliyeleta historia ya taifa hili zaidiii naona tu mnapinga hoja Zach mzee bila kuleta zenu Binafs n mkatoloki tena nimezaliwa eneo ambalo ukatoliki imeanzia kwa mkoa wa ruvuma peramiho lakn nashangaa mnapoingiza Udini kwenye nyuzi za huyu mzee
Historia ya kusimuliwa, Unajua pale Peramiho Mission Abate wa kwanza ni Litimbandyosi Mwakifuna, na alikuwa Babu yangu akitokea Nanjilinji,

Khaa kweli hii dunia hizi shule za kata ni shida sana, Huyo hana anachojua zaidi ya kusimuliwa mara na mtoto wa Abdul sykes, mara mkewe, Kuna mtu atasimulia ujinga wa mzazi wake?

Binadamu kazi yetu ni kusifia familia zetu
 
  1. Habari zake zote ni hearsay au habari za kusikia na kusimuliwa,
  2. Habari zake zote ni brainwashed au habari za mtu aliyejazwa
  3. Habari zake nyingi ni outdated au zilizopita na wakati na kukosa ushawishi kwa kundi la vijana,
Mkuu Gussie,
japo hata mimi huwa napingana na Mkuu Maalim
Mohammed Said katika maeneo makuu mawili, urongo na udini wenye some ill motives behind, lakini mnyonge mnyongeni,haki yake mpeni!, Tanzania tangu tupate uhuru, na vyuo vikuu vyetu vyote, tuna maprofesa wa historia wenye ma Ph.D kibao, lakini hakuna hata mmoja ameandika chochote cha maana katika historia ya taifa letu, hivyo Mohammed Said, anapoandika historia ya babu zake ni haki yake. Nawewe andika historia ya babu zako.

Naomba kumtetea Maalim Mohammed Said katika maeneo matatu haya

  • Habari zake zote ni hearsay au habari za kusikia na kusimuliwa-Sii kweli, kuna aina tatu tuu za kupata habari, 1. Kushuhudia, hii inaitwa 1st hand information, 1st hand news, witnessing, kuona ni kuamini. 2. Kuhadithiwa au kusimuliwa na mashuhuda waliishuhudia,hii inaitwa 2nd hand information or 2nd hand news. 3. Kufanya reseach, utafiti kwa kusoma kilichotokea na kuandukwa na waliotangulia. Neno Hearsay ni habari za kusikia tuu ambazo hazijafanyiwa utafiti. Mohammed Said anakusanya info kutoka hivyo vyanzo vitatu, hivyo its not true kusema habari zake zote ni hearsay, japo kwenye fasihi simulizi, hearsay huwa haikosekani, na ndipo hapo maurongo huwa yanaibukia kwa yeye kudanganywa na wasimulizi wake na kuingia mazima.
  • Habari zake zote ni brainwashed-sii kweli, sio kila kitu cha Mohammed Said ni brainwash, zipo simulizi zake nyingi za visa vya kweli vilivyotokea kwa lengo la uhifadhi wa historia ya kweli ya babu zake na wale wazee wa Gerezani.
  • Habari zake nyingi ni outdated au zilizopita na wakati na kukosa ushawishi kwa kundi la vijana-pia hii si kweli. Historia zote duniani ni mambo ya kale, lakini sio kila jambo la kale ni outdated, history is the study of past events in relations to the present, and to determine the future. Kati ya wana jf wenye ushawishi mkubwa humu jf, ni Maalim Mohammed Said, kuna issue fulani kuhusu Zanzibar, tulibishana humu, ghafla iligeuka shubiri, maana sikujua kama ana wafuasi wengi kivike, waliibuka watu humu sio tuu kunisonga na kunizonga kama mainzi wanavyozonga utumbo wa jana, bali ilifikia stage ya mimi kutishiwa maisha nisikanyage Zanzibar, nitakutana na cha mtema kuni. Ilimbidi Maalim awapooze vijana wake, na kuepusha shari zaidi, mode waliufunga uzi ule, hivyo kwenye hoja za ushawishi na ufuasi, mfano Maalim Mohamned Said akihamasisha wafuasi wake wakutane msikiti fulani siku ya Ijumaa, na baada ya swala, watakwenda kwa amani kulikomboa eneo fulani la babu zao, liliporwa enzi za wakoloni.
  • Watajitokeza watu kila kona, patakuwa hapatoshi.
  • Wakoloni Wajerumani na Waingereza, pamoja na udhalimu wao wote, waliheshimu makaburi, hivyo katika maeneo yote serikali ya mkoloni iliyatwaa, hata kama kulikuwa na msikiti, msikiti ulivunjwa, ila yale makaburi ya msikiti, waliyaheshimu, hata wakijenga, hapo kwenye makaburi walipaacha na makaburi hayo yapo mpaka leo, japo hutujui ni ya kina nani, ila waliyahifadhi.
  • Sasa katika Swala hiyo, Maalim Mohamned Said akatoa historia ya eneo fulani pale Feri lilikuwa eneo la msikiti, wakoloni Wajerumani wakalitwaa na kuuvunja msikiti ule, na kujenga jengo fulani jeupe, ushahidi ni makaburi ya Waislamu yaliyohifadhiwa humo, hivyo ikapigwa takbir twende tukalikomboe eneo letu.
  • Waislamu wa Ilala na Buguruni na Temeke, wao wakusanyikiea lile jengo pale Taraza next to Dar Group ili kutangazia umma, kuwa Waiskamu wa Dar es Salaam wamekomboa eneo lao. Waislamu wa Kinondoni wao wakusanyikie lile jengo pale oppsite Bamaga, kutangazia habari njema hiyo.
  • Amimi usiamini, kuna mtu kwenye jengo hilo atafurushwa!, polisi wote wa Kamanda Sirro can't stop them, labda wawatumie vijana wa Mabeyo, and there will be a blood bath!.
  • Hivyo Maalim Mohammed Said, japo very humble, mswahalina na down to earth, sii mtu wa mchezo mchezo, kuna mbegu fulani huwa anaipanda, siku mvua zikinyesha, hicho anachokipanda kikachipua, kikakota, kikakomaa na kuzaa matunda...kuna mahali hapatakalika!.
P.
 
Sina maneno ya kuwapa iliwahi kutolewa hoja ya MTU mwenye nia dhabiti na wa kuweza kuandika historia ya kweli ya Tanganyika hata mwalimu aliwahi ambiwa ajibu mbona ilikua ngumu leteni unayopinga historia aloandika ndio tutajua
Mkuu Gussie,
japo hata mimi huwa napingana na Mkuu Maalim
Mohammed Said katika maeneo makuu mawili, urongo na udini wenye some ill motives behind, lakini mnyonge mnyongeni,haki yake mpeni!, Tanzania tangu tupate uhuru, na vyuo vikuu vyetu vyote, tuna maprofesa wa historia wenye ma Ph.D kibao, lakini hakuna hata mmoja ameandika chochote cha maana katika historia ya taifa letu, hivyo Mohammed Said, anapoandika historia ya babu zake ni haki yake. Nawewe andika historia ya babu zako.
 
Andika yako.. usisahau kunitagi

Maisha ya enzi za zamani walijuaje yaliyopita?.. unafikiri kulikua na haya mfano ya mitandao n.k.

Jionee aibu.. tutaendelea kumsoma kama kawaida.
 
Kuna msemo kwamba "mshindi ndiye ana haki ya kuandika historia"

Baada ya vita ya kwanza ya dunia,mshindi ndiye ali-influence historia iandikweje kwa upande wake na upande wa adui yake. Pia kwa vita ya pili ya dunia,mshindi ndiye aliyepika historia na kuilisha dunia.

Hii iko maeneo yote,hata Kagame anasema katika mauaji ya kimbari waliokufa ni Watusi tu,wahutu hawakufa,yeye Kagame ni mshindi na anaandika historia anavyotaka bila kujali kwamba hao watu walikuwa wanauwana.

Hata vita vya kagera,tunapata upande mmoja wa stories

Ndani ya vyama vya siasa,,iwe TANU,CCM,TLP,CHADEMA, mshindi ndiye huandika historia, ukishindwa mpambano wa kisiasa aliyekushinda ataandaa wataalam wa historia watakaosimulia yake hasa anayoyataka,na kuyasema mabaya tu ya mpinzani yake, au kumfuta kabisa

Nani anamsoma Bibi Titi? Oscar Kambona, Kassanga Tumbo? Hanga? Babu? James Mapalala? Ally Mukhsin,Fundikira, na listi ni ndefu,
Hawa walishindwa vita kisiasa,waliowashinda ndio waliandika historia ya Tanzania,hawakuwaongelea ipasavyo au hawakutajwa kabisa,au waliwataja kwa kupotosha.
Baadhi zilitungwa nyimbo kuwaimba mashuleni kwamba ni maharamia wabaya kwa kuunga mkono ubepari,shule zinamilikiwa na mshindi,pia mitaala ya elimu!

Hata katika mapinduzi ya kijeshi,mshindi ndiye anaandika historia!
 
Mkuu Gussie,
japo hata mimi huwa napingana na Mkuu Maalim
Mohammed Said katika maeneo makuu mawili, urongo na udini wenye some ill motives behind, lakini mnyonge mnyongeni,haki yake mpeni!, Tanzania tangu tupate uhuru, na vyuo vikuu vyetu vyote, tuna maprofesa wa historia wenye ma Ph.D kibao, lakini hakuna hata mmoja ameandika chochote cha maana katika historia ya taifa letu, hivyo Mohammed Said, anapoandika historia ya babu zake ni haki yake. Nawewe andika historia ya babu zako.

Naomba kumtetea Maalim Mohammed Said katika maeneo matatu haya

  • Habari zake zote ni hearsay au habari za kusikia na kusimuliwa-Sii kweli, kuna aina tatu tuu za kupata habari, 1. Kushuhudia, hii inaitwa 1st hand information, 1st hand news, witnessing, kuona ni kuamini. 2. Kuhadithiwa au kusimuliwa na mashuhuda waliishuhudia,hii inaitwa 2nd hand information or 2nd hand news. 3. Kufanya reseach, utafiti kwa kusoma kilichotokea na kuandukwa na waliotangulia. Neno Hearsay ni habari za kusikia tuu ambazo hazijafanyiwa utafiti. Mohammed Said anakusanya info kutoka hivyo vyanzo vitatu, hivyo its not true kusema habari zake zote ni hearsay, japo kwenye fasihi simulizi, hearsay huwa haikosekani, na ndipo hapo maurongo huwa yanaibukia kwa yeye kudanganywa na wasimulizi wake na kuingia mazima.
  • Habari zake zote ni brainwashed-sii kweli, sio kila kitu cha Mohammed Said ni brainwash, zipo simulizi zake nyingi za visa vya kweli vilivyotokea kwa lengo la uhifadhi wa historia ya kweli ya babu zake na wale wazee wa Gerezani.
  • Habari zake nyingi ni outdated au zilizopita na wakati na kukosa ushawishi kwa kundi la vijana-pia hii si kweli. Historia zote duniani ni mambo ya kale, lakini sio kila jambo la kale ni outdated, history is the study of past events in relations to the present, and to determine the future. Kati ya wana jf wenye ushawishi mkubwa humu jf, ni Maalim Mohammed Said, kuna issue fulani kuhusu Zanzibar, tulibishana humu, ghafla iligeuka shubiri, maana sikujua kama ana wafuasi wengi kivike, waliibuka watu humu sio tuu kunisonga na kunizonga kama mainzi wanavyozonga utumbo wa jana, bali ilifikia stage ya mimi kutishiwa maisha nisikanyage Zanzibar, nitakutana na cha mtema kuni. Ilimbidi Maalim awapooze vijana wake, na kuepusha shari zaidi, mode waliufunga uzi ule, hivyo kwenye hoja za ushawishi na ufuasi, mfano Maalim Mohamned Said akihamasisha wafuasi wake wakutane msikiti fulani siku ya Ijumaa, na baada ya swala, watakwenda kwa amani kulikomboa eneo fulani la babu zao, liliporwa enzi za wakoloni.
  • Watajitokeza watu kila kona, patakuwa hapatoshi.
  • Wakoloni Wajerumani na Waingereza, pamoja na udhalimu wao wote, waliheshimu makaburi, hivyo katika maeneo yote serikali ya mkoloni iliyatwaa, hata kama kulikuwa na msikiti, msikiti ulivunjwa, ila yale makaburi ya msikiti, waliyaheshimu, hata wakijenga, hapo kwenye makaburi walipaacha na makaburi hayo yapo mpaka leo, japo hutujui ni ya kina nani, ila waliyahifadhi.
  • Sasa katika Swala hiyo, Maalim Mohamned Said akatoa historia ya eneo fulani pale Feri lilikuwa eneo la msikiti, wakoloni Wajerumani wakalitwaa na kuuvunja msikiti ule, na kujenga jengo fulani jeupe, ushahidi ni makaburi ya Waislamu yaliyohifadhiwa humo, hivyo ikapigwa takbir twende tukalikomboe eneo letu.
  • Waislamu wa Ilala na Buguruni na Temeke, wao wakusanyikiea lile jengo pale Taraza next to Dar Group ili kutangazia umma, kuwa Waiskamu wa Dar es Salaam wamekomboa eneo lao. Waislamu wa Kinondoni wao wakusanyikie lile jengo pale oppsite Bamaga, kutangazia habari njema hiyo.
  • Amimi usiamini, kuna mtu kwenye jengo hilo atafurushwa!, polisi wote wa Kamanda Sirro can't stop them, labda wawatumie vijana wa Mabeyo, and there will be a blood bath!.
  • Hivyo Maalim Mohammed Said, japo very humble, mswahalina na down to earth, sii mtu wa mchezo mchezo, kuna mbegu fulani huwa anaipanda, siku mvua zikinyesha, hicho anachokipanda kikachipua, kikakota, kikakomaa na kuzaa matunda...kuna mahali hapatakalika!.
P.

Paskal na Mzee mwanakijiji huwa nawaelewa sana. Ila huyu mzee Mohamed Said sijui huwa anawaza nn? Udini umemtafuna hadi uwezo wake wakufikiri umekuwa chini sana.

Kila siku yeye ni waislamu wanaonewa, waislam wanaonewa. Vp kuhusu wapagani na imani zingine? Au anazani wanaostahili haki katika nchi hii ni waislam na wapinzani wake wakristo pekee? Hakika umesema vyema mbegu anayoipanda ajiandae ghala yakuhifadhia mavuno.

Nawashangaa sana hawa watu wa imani. Wanapokuwa ktk ibada zao wanahubiri kuwa baada ya kifo kuna pepo (mbinguni) kwa wenye haki kwa maana hiyo nilizani wangeachana na madai ya haki duniani wapambane waitafute haki yakuwapeleka peponi kinyume na hapo wanatuchanganya.
 
Habari zake zote ni hearsay au habari za kusikia na kusimuliwa, Hivi kila mtu akiamua kusimulia habari za Babu yake jinsi alivyoshiriki vita ya kwanza ya dunia nadhani vitabu havitatosha, Miaka ya 1990 na mwanzoni ya miaka ya 2000 kila Mzee alisimulia alishiriki vita ya kwanza ya dunia, Mzee yupi mkweli?

Kaka inaonekana hujaisoma elimu ya kuhakiki habari,unafikiri kila mtu anaweza kusimulia habari za babu yake alishiriki vipi vita vya kagera ? Hili jambo haliwezekani sababu watu hawana habari za watu wao,kama unaona kusimulia ni jambo rahisi,embu tutajie mababu zako sita katika uzao wako.

Hizi takwimu za kusema "kila mzee alisimulia" umezipata na tutaziamini vipi ? Je wewe ulisikia au ulisoma vitabuni haya unayoyasema ?

Je kwako wewe kila habari ya kusimuliwa ni ya uongo au ? Na ili habari ya kusimuliwa ikubaliwe na iwe kweli inatakiwa kukidhi vigezo gani ?
 
Mkuu acha kuchafua watu na wewe lete historia y'all nchi kwa kadri unavyoifahamu tuipime Kama ya mzee moh'd said n ya kupotosha

Hoja hujibiwa kwa hoja unabaki kumsema mzee wa watu wakat wewe huweki historia unayoifahamu
Tatizo kubwa kwetu mkuu ni uvivu... uvivu wa kusoma... uvivu wa kufikiri.... uvivu wa kutafiti... uvivu wa kujitambua... uvivu wa kubaini... uvivu... uvivu. .. uvivu...
Ndio maana "NDIYOOOO..... NA KUGONGA MEZA VIMESHAMIRI!!!"
Tunaaminishwa na tunatakiwa kuamini UHURU WA TANGANYIKA ULILETWA NA MTU MMOJA!!! HAPO NDIPO MOHAMMED SAID ANAPOITWA MUONGO!!!
 
Nani alisema uhuru uliletwa na mtu mmoja?
 
UMESHAWAHI SOMA HISTORIA ?

SHULE YA MSINGI AU PIA KIDATO CHA KWANZA? SOURCES OF HISTORY?

KUNA oral traditions masimulizi kwa njia ya mdomo !

hivyo basi MOHAMED SAID kama kasimuliwa haina shida labda kama UNA WIVU AMBAO

Ashakum si matusi na NYIE WANAWAKE MNAO SANA
Kwa hiyo Yeye alisimuliwa majina ya kiislam tu, Wale wenye majina ya kitamaduni kama Andendekisye huko Mbeya hawakushiriki au?
 
Back
Top Bottom