siasa za mkuchika,olimpiki na bakuli la emilian partrick.

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,414
8,369
...waziri wa michezo na utamaduni ni john mkuchika ..huyu ni kati ya wale marafiki wa kikwete alioingia nao jeshini akiwamo..marehemu capt.ukiwaona ramadhani mwinshehe ditopile mzuzuri,luteni makamba,luteni lowassa ets...

katika utendaji wa wizara hii naona ni sifuri tangu enzi za khatib...ni kama kijiwe...imekuwa wizara ya kungojea kutoa pongezi bila kujua zimekujaje..haina sera wala mwelekeo wa kisera kuinua michezo...

kwa wizara hii michezo maana yake ni mpira wa miguu tu...haiongelei riadha,masumbwi,kuogelea..ets ni aibu tupu.pale nchi ya milioni 40 inaposhindwa mfano..kupeleka wanariadha kwenye mashindano ya dunia london..KWA KUKOSA NAULI TU!!!...hadi ikabidi katibu mkuu suleiman nyambui akatembeze bakuli la nauli..akakutana na wasanii ambao walimwambia kama anataka kulipiwa nauli aweke watoto wa hao wafadhali kwenye list ya wanamichezo ili wapewe visa za uk....aibu..uk wakashtuka wakawanyima visa wakimbiaji wetu wote!

hawa ndio mawaziri wetu..ameshindwa hata kumleta kocha wa ngumi ..kama tulipoikuwa na gharisa CARICASESA yule mcuba ambaye enzi zake kila olimpiki tulikuwa na uhakika wa medali za ngumi!

kali ya yote na aibu ya yote na uchungu ...nimeshuhudia ITV wakitangaza bakuli mfano wa lile la MEWATA ..kwenye luninga omba omba ya kusaidia bondia wetu EMILIAN PARTRICK akae kambini na kumszaidia aende CHINA olimpiki...YAANI serikali haina pesa ya kumuweka bondia mmoja kambini...wala haina uwezo wa kumlipia nauli..sasa tujiulize wizara hii huomba kila chama cha michezo kipeleke ratiba na budget ...ili watenge pesa za mwaka mzima,tujiulize na aibu hii pesa hizi wizara inafanyia nini hadi tunakuwa ombaomba..

wakati haya yakiendelea jirani zetu kenya kila michezo hupeleka ndege nzima ya watu 200 kwenye michezo iwe ya afrika au dunia...sisi hata mmoja anatushinda!!

sasa huyu capt mkuchika ...naibu katibu mkuu wa chama cha mapinduzi ...anafanya nini hapo?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom