Siasa za Maji taka zishindwe - DR. Slaa upo juu babaa - Umewakamata! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa za Maji taka zishindwe - DR. Slaa upo juu babaa - Umewakamata!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by ELNIN0, Sep 9, 2010.

 1. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Wakuu si ushabiki ila nasema ki ukweli kabisa for the first time katika uchaguzi huu tunaona CCM - Ikiweweseka, juzi na jana nilikuwa Arusha nimezunguka sana mjini, talk of the town ilikuwa CCM wapuuzi kumpandikizia kesi DR Slaa eti tumshushie imani yetu kwake hatudanganyiki na kibaya zaidi hii issue imechukuliwa 100% na wananchi wa arusha kuwa ni njama za CCM kutaka kumchafua - vijiwe vya taxi, bodaboda, bajaji, daladala na hata kwa kina mama lishe mazungumzo yalikuwa hayo tu.

  Utamaduni wa mwafrika huwa hautilii sana maanani masuala haya na ndiyo maana wengi wao walisikika wakisema " Huyo mwanaume ni mwanaume kweli yaaani hadi unanyang'anywa mke unakuwa wapi ?, sasa eti anataka hela za mezani alipwe na mwanaume mwenzake aisee fanya kazi wewe acha kuomba pesa ya mezani babanguu ni ujinga huo" haya yalikika kwa baadhi ya maoni wananchi hapo Arusha.

  Baada ya kushindwa hoja ya U - Padri na udini sasa hii hoja nayo imegonga mwamba, pamoja na magazeti hasa ya Rai, Mtanzania achilia mbali haya ya udaku kuandika jambo hili kiushabiki lakini wananchi bado wana imani kubwa sana na mgombea wa CHADEMA mheshimiwa DR. Slaa.

  Kuhusu magazeti yaliyokuwa yanagawiwa bure Wananchi wamesema hawadanganyiki na pesa za CCM kujaribu kumharibia DR. Slaa na wakaenda mbali zaidi na kusema kwamba hawatamchagua mgombea wa CCM arusha mjini sababu ameolewa zanzibar - aende akaishi ya mumewe aiache Arusha yetu.

  Mgombea huyo wa Ubunge Arusha Mjini kwa tiketi ya CCM ambaye pia ni waziri ktka serikali ya sasa alikwepa mdahalo uliondaliwa na NEC bila kutoa sababu za msingi.

  Wakuu nilitaka niwahabarishe hayo yaliyojiri hapo arusha mjini katika pitapita zangu za juzi na jana kabla ya kurudi DAR.
   
 2. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Wenye habari zingine, maeneo mengine kama kanda ya ziwa, kati, kuzini na maeneo ya tanga watupe habari kamili kuhusu wananchi wanayapokeaje haya mambo ya kuchafuana. Ahsante Elnino.
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Tatizo CCM imejaa watu wa taarabu. Wantumia muda na pesa kueneza 'mipasho' kwa hamnazo. Lakini wamebugi. Bora hayo magazeti wangeyapeleka Pwani, Morogoro na Tanga wangeeleweka. Siyo Arusha.
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nakubaliana kabisa na hili "siasa za maji taka zishindwe, tena na zilegee!!!!!!
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  CCM imexpire,its time for other parties.
  CCM ilikuwa enzi za Mwalimu
   
 6. Gobret

  Gobret JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2010
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Akhsante Mkuu. Ukweli utasimama siku zote. Laiti CCM wangalijua jinsi walivyojichakachua WENYEWE ktk hili na kuwa wananchi si WAJINGA ki-hivyo. Watu wanazidi kupoteza imani kwa CCM. HUU NDIO MWISHO WA CCM. CHADEMA JANA NA LEO, NYAKATI NA ENZI PIA. DK SLAA CAN NEVER BE STOPPED BY STINKING/ HALUCINATING BUCCAL CAVITIES OF CCM. GO DR SLAA. GOD BLESS YOUR EFFORTS.
   
 7. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Arusha hali sii shwari kwa huyo Mama Batilda. Kwanza hakusoma alama za nyakati , pili aliye nyuma yake anafahamika..Ni EL . Kwamba ni Mzanzibar,na kwamba alikuwa Waziri wa Mzingira kwa miaka mitano akashindwa kuisadia Arusha hadi ikabaki chafu kuliko miji yote huku kaskazini ndio nyimbo za Waarusha.
   
 8. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu tafadhali, tutake radhi!! sisi HATUDNGANYIKI, wamemfukuza meneja wakiwanda cha mtibwa wakifikiri kwa hilo watatudanganya, hiyo janja ya nyani kwishastukiwa. Tuanajua mwenye kiwanda anayenyonya jasho la watu maskini ni Fisadi Mkapa, ambaye huyu prezidaa alisema tumwache apumzike yani ukiwa mwizi na mhujumu uchumi badala ya kwenda keko, unaacha upumzike.
   
 9. W

  WildCard JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Tunajichafua wenyewe kama akina Wayne Rooney, Tiger Woods, John Terry, Bill Clinton,...., halafu tukionyeshwa uchafu huo tunang'aka, tunarusha lawama kungine! Sikumtarajia shujaa wangu Dr Slaa anase kwa akina mama kwa kiwango hiki.
   
 10. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Mtu kwenye akili timamu lazima atan'gamua na kujua huu ulikuwa upuuzi tosha kuharibu reputation ya DR. Slaa, na uzuri watanzania wameshaamua so we kaa kimya.
  Kizuri zaidi CHADEMA wameachia public kuamua suala hili na wananchi wameshaliona ni craps za CCM - kataa au ukubali na hili litawatafuna zaidi.

  I mean nani asiyejua UCHAFU wa wagombea wa CCM, je kama CHADEMA wangeamua kuania ufisadi wa kimapenzi na ufusuka kuanzia kwenye chaguzi za CCM je tungefika wapi?
   
 11. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  EL NINO umesema kweli.

  Hakika Chama Cha Majambazi(CCM) uchaguzi wa mwaka huu cha moto wanakiona.
  Wamejaribu mbinu zote za kumchafua Dk.Slaa lakini zimegonga mwamba. Wameishiwa kabisa na sera wamebakia kurushia watu maji taka wakidhani kuwa sera za maji taka zitawasaidia. Nawaambia is too late for them to catch CHADEMA's flying chopper. Wao warieee tu!!!!

  Inasikitisha kuona Katibu wao Msambaa au tumwite Mshamba wa Bumbuli akihaha kwenye magazeti uchwara na udaku kuwanunua waandishi uchwara eti waandike juu ya Dk. Slaa kuchukua mke wa mtu. Ni uzezeta na upumbavu ambao watu wenye akili timamu hawawezi kudanganyika.
  This guy called Mahimbo where was he for the past 3 years when his x-wife vacated his home???????????????Babu Makamba hizo ni mbinu za kizamani sana zilishapitwa na wakti.

  Nataka Mahimbo atuambia miaka 3 alikuwa wapiaTunamshangaa kukurupuka siku ile Josephine alipotambulishwa Jangwani kuwa ni fiance wa Dokta Slaa. Nataka atoke huko alipo atuambia ni kitu kimetokea baada ya siku ile pale Jangwani. Bado anatakiwa authibitishie umma wa Watanzania kuwa hajanunuliwa na Makamba ili kujaribu kumchafua Dk. Slaa.

  Mimi nawapa CCM na MAHIMBO ushauri wa bure:
  Kwa MAHIMBO namwabia yafuatayo: MAHIMBO AENDE HARAKA SANA AKAFUTE HIYO KESI MAHAKAMANI MAANA AKIENDELEA KUKOMAA NAYO KWA KULAGHAIWA KUWA KIBARAKA WA CCM BASI AJUE KUWA ANAWATUKANA WATANZANIA NA ITAKUJA KUMGHARIMU MAISHA YAKE.

  Watanzania tu wastaaarabu sana lakini kama mtu akianza kuleta kuingilia maswala binafsi ambayo hayana tija wala faida kwa Watanzania tunamwona kuwa ameishiwa na amefilisika kisiasa. Hapa ndipo walipofikia CCM.

  Wakumbuke kwamba hata kama kweli Josephine ni mke wa huyo Mahimbo ambaye bila shaka ana matatizo ya aidha kisaikolojia,kiuchumi au pengine lililo kubwa zaidi ni MAMBO HAYAWEZI KITANDANI basi amwachie Dk Slaa achukue mchuma. Maana inaonesha Dk. Slaa ni lijali na Dume la mbegu ndiyo maana Mahimbo kaachwa solemba kwa vile MAMBO HAYAWEZI!!!!!!!!!!!!!!!!

  KWA CCM NA MAKAMBA WAO nasema hivi:

  Pale Bndeni kwa mzee anayeheshimika sana Mzee Madiba kuna kamchezo ka aina hii kalifanywa kwa huyu Mzee wa Kizulu anayetamba kwa jina la JACOB ZUMA. Wapinzani wake ndani ya ANC walianza siasa za maji taka kumchafua kwa kuingilia mambo yake ya binafsi. Kila kitu kiliwekwa hadharani. Mzee mzima akasimamishwa mbale ya Pilato akapigwa maswali kuhusu alivyofanya ngono na mwanamke asiye mkewe pasipo hata kutumia kondomu!!!!!!!. Mzee Zuma akasema mbele ya Plato kuwa yeye alikuwa akimaliza shughuli anaosha mashina yake kwa maji. Kumbuka hapa Zuma alikuwa bado hajawa Rais wa Afrika Kusini. CCM Mpo?????!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Lakini uchaguzi ulipokuja Zuma akapeta na kuwa Rais wa Afrika Kusini mpaka leo hii. Kwa hiyo CCM nataka mjifunze kutoka kwa Jacob Zuma. Na laiti kama mngelisoma alama za nyakati huu ujinga mnaotuonyesha WATANZANIA MSINGEUFANYA.

  Makamba watu wana kustahi tu lakini watakapoamua kumwaga mambo yako ya kibinafsi pamoja na huyo Mwenyekiti wako Tanzania patakuwa hapatoshi.Kwanza nasikia hiyo nundu uliyonayo kwenye paji la uso ulipigwa rungu wakti ukinyemela mke wa mtu! Kama ni uongo jitokeze ukanushe. Pambaf!

  Wasalaaamu.
   
 12. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante Baba...Vipi kuhusu mgombea Ubunge wao Aliyekimbia Mdahalo juzi...!?
   
 13. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,899
  Likes Received: 12,031
  Trophy Points: 280
  Duh!
   
 14. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,899
  Likes Received: 12,031
  Trophy Points: 280
  ELNINO

  Ume hit penyewe habisa haya ndiyo maneno yanayosemwa na akina mama mitaani kuwa hadi mwanamke anakimbia jua huyo jamaa si ridhiki. Harafu Makamba amebugi step kupeleka hayo magazeti ya umbea Arusha na Moshi huko siko, nawajua kinamama wa huko walivyo wachakalikaji asubuhi utamwona kabeba mikungu ya ndizi anakwenda sokoni kufanya biashara kama si Tengeru sehemu nyingine, huyo hana muda wa kufanya umbea. Kuna mtoa hoja hapo juu kasema angepeleka mikoa mingine siitaji ingawa najua hata huko HAWADANGANYIKI.
   
 15. comp

  comp Member

  #15
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi Makamba ana elimu gan jamani? Yan strategies zake ni kichekesho kweli. Mi naona kama anamwongezea umaarufu Dr Slaa. Kwa vile sasa hivi magazeti yao yote habari kubwa ni `Dr Slaa na Josephine`. Hata wanavijiji sasa wanamjua Dr Slaa na wana shauku ya kutaka kujua anasema nini.
   
 16. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #16
  Sep 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  May be ni kwa sababu wakati wa "foolish age" alikuwa seminarini, na sasa ndio analipizia hayo mambo uzeeni.

  Sikutarajia mtu kama Dr. Slaa akitupe kigezo cha uadilifu kirahisi namna hiyo.
   
 17. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #17
  Sep 10, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Duh! Wameiba password yako nini mkuu?
   
 18. jimwax

  jimwax Member

  #18
  Sep 10, 2010
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii kesi ya kuiba mke, kibongo bongo haimati wala nini, ccm wasituletee mambo ya tiger woods hapa, tunachotaka kusikia ni kwamba dr slaa anaingia ikulu november.
   
 19. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #19
  Sep 10, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Sijui unasema nini? Kwamba Arusha wanampenda Dr. Slaa? Lakini Arusha ni nyumbani kwake.kama wanampenda siyo hoja. Huyu mtu kama anashtakiwa kwamba amemuiba mke wa mtu,hawezi kushinda Uchaguzi,hapaswi kushinda Uchaguzi,kwa sababu that is immoral. This is a confused person,ambaye anafikiria kwamba reputation yake inakuwa enhanced akituhumiwa kuiba mke wa mtu.
  Swali langu ni kwmba yule jamaa aliyeibiwa mke alibembelezwa asiende mahakamani? Kwa sababu Bwana Yesu alisema ukibishana na adui yako,try to settle it out of Court. Usikubali mambo kama haya yaende Mahakamani.
  CHADEMA mimi nataka kuwapa friendly advice,nguvu zao zielekezwe katika wabunge,na siyo huyu mgombea Urais.
  Urais sasa kushindana na Kikwete ni kazi ya Lipumba. Lipumba napaswa kuingia katika hii nafasi iliyoachwa wazi na kuvurunda kwa Dr. Slaa ambaye sasa ana slur kubwa katika utendaji kazi wake.
  Na swali kwa Kikwete,kwa nini anataka kuikoa Handeni isichukuliwe na Bahari? Hii inahitaji ufafanuzi. Kwa nini watu wa Handeni wasiambiwe kwenda kujenga mahali pengine? Kwa nini tushindane na Bahari?
   
 20. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #20
  Sep 10, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ganesh,
  You want to talk about morality? Is Kikwete moral? Mengine tunanyamaza tu ameshakuwa rais wetu lakini hakuna mtu mchafu katika mambo
  ya morality kama Kikwete. Tumechoka kushauriwa tuelekeze nguvu zetu kwenye ubunge wakati nchi inaendelea kuoza chini ya uongozi wa Kikwete na Makamba. Ukitaka kumwuua nyoka unampiga kichwani na this time tunaipiga CCM kichwani. Then utaona itakavyosambaratika.
  Keep morals out of this.
   
Loading...