Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,498
- 51,092
Kwa kila mtu mwenye akili, siasa za mauaji ni siasa mbaya za hatari na hazifai kabisa, yatupasa kuziogopa kuzidi UKIMWI.
Siasa za kuuana huchagizwa pale wanaofanya hivyo vitendo wanapokuwa wamejiaminisha kwamba wao wanaweza kutekeleza azma zao bila consequences zozote kwa upande wao na pia hudhani kwamba kwa kutekeleza mauaji hayo basi ni jambo zuri kwa kuwa yule watakayekuwa wamemuua atakuwa hayupo tena kusumbuasumbua!.
Ubaya wa siasa za mauaji ukiachilia mbali hali ya kuchafua nchi au jamii husika, Inaweza kusababisha UNINTENDED CONSEQUENCES kama Vile KISASI ( REVENGE).
Ikishafikia hatua hii ni mbaya, kwa sababu siyo kila nafsi duniani imeumbwa Kutulia, kujikunyata, kunyenyekea ikionewa!. Kuna Nafsi Ukizipiga Ngumi ya Sikio na yenyewe inakulia Timing inakupiga ya Jicho, Ukiiuliza Unaonaje na yenyewe inakujibu unajisikiaje?
Kibaya cha Siasa za mauaji ni kwamba wanaweza kuingizwa katika mapambano watu wasiohusika kabisa na gemu hii ovu. Unaweza Kuonea mtu, na yeye au watu wake wakataka kulipa visasi!. Hili jambo ni la kuogofya sana kwa sababu madhara yake ni makubwa na lisipothibitiwa ipasavyo ikageuka kuwa mwendelezo wa visasi na kisha asitokee mtu wa kukema
Wahanga wengine wanaweza kuwa ni wanafamilia. Ukidhuru mtu, watu wake wanaweza kwenda mbali hadi kuingiza wanafamilia katika mchezo wa visasi. Sasa hiyo ni hatari sana.
Sisi kama Taifa yatupaswa kutokubali kuingia katika mtego wa "kumalizana", maana ikishafikia hatua hiyo busara hukaa pembeni na mashetani wanywa damu hufanya kazi ya kuchochea huku, kisha wakachochea kule ili yaendelee kunywa damu za watu wasio na hatia.
Kuna watu dunia hii wanasubira kweli, unaweza kumdili leo, yeye akakuchorea raketi miaka 10 ijayo kulipiza kisasi!
Tit for Tat ni mbaya, Tusikubali sisi kama Taifa Kutumbukia katika Mtego wa Kudhuriana na pia kulipizana visasi!
"PETRO HEBU RUDISHA PANGA LAKO ALANI MAANA AISHIYE KWA UPANGA ATAKUFA KWA UPANGA"- Yesu Wa Nazareth
AMANI KWA WOTE!