Siasa za kuuana: Wahanga wanaweza kuwa wenye kuhusika na wasiohusika

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
7,338
2,000
Kwa kila mtu mwenye akili, siasa za mauaji ni siasa mbaya za hatari na hazifai kabisa, yatupasa kuziogopa kuzidi UKIMWI.

Siasa za kuuana huchagizwa pale wanaofanya hivyo vitendo wanapokuwa wamejiaminisha kwamba wao wanaweza kutekeleza azma zao bila consequences zozote kwa upande wao na pia hudhani kwamba kwa kutekeleza mauaji hayo basi ni jambo zuri kwa kuwa yule watakayekuwa wamemuua atakuwa hayupo tena kusumbuasumbua!.

Ubaya wa siasa za mauaji ukiachilia mbali hali ya kuchafua nchi au jamii husika, Inaweza kusababisha UNINTENDED CONSEQUENCES kama Vile KISASI ( REVENGE).

Ikishafikia hatua hii ni mbaya, kwa sababu siyo kila nafsi duniani imeumbwa Kutulia, kujikunyata, kunyenyekea ikionewa!. Kuna Nafsi Ukizipiga Ngumi ya Sikio na yenyewe inakulia Timing inakupiga ya Jicho, Ukiiuliza Unaonaje na yenyewe inakujibu unajisikiaje?

Kibaya cha Siasa za mauaji ni kwamba wanaweza kuingizwa katika mapambano watu wasiohusika kabisa na gemu hii ovu. Unaweza Kuonea mtu, na yeye au watu wake wakataka kulipa visasi!. Hili jambo ni la kuogofya sana kwa sababu madhara yake ni makubwa na lisipothibitiwa ipasavyo ikageuka kuwa mwendelezo wa visasi na kisha asitokee mtu wa kukema

Wahanga wengine wanaweza kuwa ni wanafamilia. Ukidhuru mtu, watu wake wanaweza kwenda mbali hadi kuingiza wanafamilia katika mchezo wa visasi. Sasa hiyo ni hatari sana.

Sisi kama Taifa yatupaswa kutokubali kuingia katika mtego wa "kumalizana", maana ikishafikia hatua hiyo busara hukaa pembeni na mashetani wanywa damu hufanya kazi ya kuchochea huku, kisha wakachochea kule ili yaendelee kunywa damu za watu wasio na hatia.

Kuna watu dunia hii wanasubira kweli, unaweza kumdili leo, yeye akakuchorea raketi miaka 10 ijayo kulipiza kisasi!

Tit for Tat ni mbaya, Tusikubali sisi kama Taifa Kutumbukia katika Mtego wa Kudhuriana na pia kulipizana visasi!

"PETRO HEBU RUDISHA PANGA LAKO ALANI MAANA AISHIYE KWA UPANGA ATAKUFA KWA UPANGA"- Yesu Wa Nazareth

AMANI KWA WOTE!
 
mkafrend

JF-Expert Member
May 12, 2014
3,053
2,000
Sisi kama Taifa yatupaswa kutokubali kuingia katika mtego wa "kumalizana" said:
Hii nimeipenda - jamani tuendelee kushikamana kutetea amani ya taifa letu - mtu akijaribu kutuweka nje ya mstari wa amani tumshanage kwa maneno na vitendo
 
RockCarnegie

JF-Expert Member
Jan 17, 2019
894
1,000
Kwa kila mtu mwenye akili, siasa za mauaji ni siasa mbaya za hatari na hazifai kabisa, yatupasa kuziogopa kuzidi UKIMWI.

Siasa za kuuana huchagizwa pale wanaofanya hivyo vitendo wanapokuwa wamejiaminisha kwamba wao wanaweza kutekeleza azma zao bila consequences zozote kwa upande wao na pia hudhani kwamba kwa kutekeleza mauaji hayo basi ni jambo zuri kwa kuwa yule watakayekuwa wamemuua atakuwa hayupo tena kusumbuasumbua!.

Ubaya wa siasa za mauaji ukiachilia mbali hali ya kuchafua nchi au jamii husika, Inaweza kusababisha UNINTENDED CONSEQUENCES kama Vile KISASI ( REVENGE).

Ikishafikia hatua hii ni mbaya, kwa sababu siyo kila nafsi duniani imeumbwa Kutulia, kujikunyata, kunyenyekea ikionewa!. Kuna Nafsi Ukizipiga Ngumi ya Sikio na yenyewe inakulia Timing inakupiga ya Jicho, Ukiiuliza Unaonaje na yenyewe inakujibu unajisikiaje?

Kibaya cha Siasa za mauaji ni kwamba wanaweza kuingizwa katika mapambano watu wasiohusika kabisa na gemu hii ovu. Unaweza Kuonea mtu, na yeye au watu wake wakataka kulipa visasi!. Hili jambo ni la kuogofya sana kwa sababu madhara yake ni makubwa na lisipothibitiwa ipasavyo ikageuka kuwa mwendelezo wa visasi na kisha asitokee mtu wa kukema

Wahanga wengine wanaweza kuwa ni wanafamilia. Ukidhuru mtu, watu wake wanaweza kwenda mbali hadi kuingiza wanafamilia katika mchezo wa visasi. Sasa hiyo ni hatari sana.

Sisi kama Taifa yatupaswa kutokubali kuingia katika mtego wa "kumalizana", maana ikishafikia hatua hiyo busara hukaa pembeni na mashetani wanywa damu hufanya kazi ya kuchochea huku, kisha wakachochea kule ili yaendelee kunywa damu za watu wasio na hatia.

Kuna watu dunia hii wanasubira kweli, unaweza kumdili leo, yeye akakuchorea raketi miaka 10 ijayo kulipiza kisasi!

Tit for Tat ni mbaya, Tusikubali sisi kama Taifa Kutumbukia katika Mtego wa Kudhuriana na pia kulipizana visasi!

"PETRO HEBU RUDISHA PANGA LAKO ALANI MAANA AISHIYE KWA UPANGA ATAKUFA KWA UPANGA"- Yesu Wa Nazareth

AMANI KWA WOTE!
Amina
 
Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,197
2,000
Tumekuwa wapole mno ,mwisho wana tumalizia Ndugu zetu kwa Sababu za kipuuuz kabisa.
 
introvert

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
1,324
2,000
Tumeshavuka mstari na ni ngumu kurudi nyuma.

Wanaofanya haya kila siku wanaishi kwa hofu kuzidi jana. Tusitegemee waondoke madarakani maana leo wana maadui wengi ndani na nje ya chama kuliko jana. Kesho wana maswali mengi kujibu kuliko leo.

Ni ajabu watu wapo tayari kufungia macho maovu kulinda nafasi zao na matumbo yao kisa tu sasa wao wapo mezani na ni zamu yao kula kwa kisingizio cha uzalendo.

Mfano hawa wanaofungwa huku ushahidi haujakamilika, kesho wakipata madaraka watasamehe hawa waliowatesa? Au wanaotekwa na kupotea, hata kama Serikali haihusiki, unafikiri kesho ndugu, jamaa na marafiki zao wakishika madaraka watasamehe?
 
Emisesayo

Senior Member
Feb 16, 2019
129
250
imeandikwa jino kwa jino jicho kwa jicho bila shaka mwandishi wa kitabu alikusudia kujenga ukakamavu wa kiakili sio uonewe unakalia kusema MUNGU yupo!
 
moudgulf

JF-Expert Member
Jan 23, 2017
87,681
2,000
Nakubalina wewe
Kwa kila mtu mwenye akili, siasa za mauaji ni siasa mbaya za hatari na hazifai kabisa, yatupasa kuziogopa kuzidi UKIMWI.

Siasa za kuuana huchagizwa pale wanaofanya hivyo vitendo wanapokuwa wamejiaminisha kwamba wao wanaweza kutekeleza azma zao bila consequences zozote kwa upande wao na pia hudhani kwamba kwa kutekeleza mauaji hayo basi ni jambo zuri kwa kuwa yule watakayekuwa wamemuua atakuwa hayupo tena kusumbuasumbua!.

Ubaya wa siasa za mauaji ukiachilia mbali hali ya kuchafua nchi au jamii husika, Inaweza kusababisha UNINTENDED CONSEQUENCES kama Vile KISASI ( REVENGE).

Ikishafikia hatua hii ni mbaya, kwa sababu siyo kila nafsi duniani imeumbwa Kutulia, kujikunyata, kunyenyekea ikionewa!. Kuna Nafsi Ukizipiga Ngumi ya Sikio na yenyewe inakulia Timing inakupiga ya Jicho, Ukiiuliza Unaonaje na yenyewe inakujibu unajisikiaje?

Kibaya cha Siasa za mauaji ni kwamba wanaweza kuingizwa katika mapambano watu wasiohusika kabisa na gemu hii ovu. Unaweza Kuonea mtu, na yeye au watu wake wakataka kulipa visasi!. Hili jambo ni la kuogofya sana kwa sababu madhara yake ni makubwa na lisipothibitiwa ipasavyo ikageuka kuwa mwendelezo wa visasi na kisha asitokee mtu wa kukema

Wahanga wengine wanaweza kuwa ni wanafamilia. Ukidhuru mtu, watu wake wanaweza kwenda mbali hadi kuingiza wanafamilia katika mchezo wa visasi. Sasa hiyo ni hatari sana.

Sisi kama Taifa yatupaswa kutokubali kuingia katika mtego wa "kumalizana", maana ikishafikia hatua hiyo busara hukaa pembeni na mashetani wanywa damu hufanya kazi ya kuchochea huku, kisha wakachochea kule ili yaendelee kunywa damu za watu wasio na hatia.

Kuna watu dunia hii wanasubira kweli, unaweza kumdili leo, yeye akakuchorea raketi miaka 10 ijayo kulipiza kisasi!

Tit for Tat ni mbaya, Tusikubali sisi kama Taifa Kutumbukia katika Mtego wa Kudhuriana na pia kulipizana visasi!

"PETRO HEBU RUDISHA PANGA LAKO ALANI MAANA AISHIYE KWA UPANGA ATAKUFA KWA UPANGA"- Yesu Wa Nazareth

AMANI KWA WOTE!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
ROMUARD KYARUZI

JF-Expert Member
Sep 18, 2018
684
500
Ebu jamani dini zinazohibuka kila leo za manabii,zinawaweka watu hofu kuwa watakufa wakihama dini zao,eti kuna Freemason wanaonyonya damu za watu hili wapate utajili,Wengine wanawaaminisha kupata utajiri wa hajabu bila jasho,kwa kupitia miujiza ebu chunguza kuna siri gani ya miujiza.Mbona munachunguza waganga wa kienyeji hawa wajaja wa miujiza wana tofauti gani na waganga wa kienyeji
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
7,338
2,000
Tumekuwa wapole mno ,mwisho wana tumalizia Ndugu zetu kwa Sababu za kipuuuz kabisa.
Tuwe makini sana tusikaribishe utaratibu wa Tit for tat!

Kama mtu una akili za kudhuru watu wengine, basi na watu wengine nao wakiamua kuzitumia akili zao kukudhuru wanaweza pia!

Tutunze amani!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom