AUGUSTINO CHIWINGA
JF-Expert Member
- Apr 23, 2017
- 220
- 689
Hakuna ubishi kwamba Chadema imekamia kupata madaraka kwa gharama yoyote ile ikiwemo kuhalalisha ndoa za jinsia hapa Tanzania.
Tamaa na uchu huo wa madaraka walionao umewafanya wawe vituko na watu wasio na maana waliojipotezea heshima na kuaminika kwa Wananchi wa Tanzania.
Tabia yao ya kukosoa na kupinga nchi ya Tanzania kupata maendeleo inawachukiza Wananchi walio wengi haswa wakijiuliza ni nini haswa amacho Chadema wangefanya cha tofauti na kinachofanywa na Serikali iliyopo madarakani.
Siasa za kudandiadandia matukio ni mojawapo ya kitu kitakachowanyausha mwaka 2020.Ukiwa mdandiaji wa matukio unakua unakosa agenda zinazoeleweka matokeo yake tukio husikam likiisha na wewe unapotea.Lakini pia Chadema inawachanganya wanachama wake kwa kuwa hawaelewi Sera,Itikadi wala maelngo ya chama hicho.Hii inatoa inatoa mwanya wa kukimbiwa na wanachama na viongozi lakini pia wanakosa wanachama wapya.
Mbinu wanazotumia Chadema katika kuikabili CCM hazitaweza kufua dafu katika msingi mkubwa mmoja, CCM inafanya Siasa safi za maendeleo zinazoshughulika na changamoto za watu ilhali Chadema wamejiegemeza katika kufanya Siasa chafu, za matusi,kejeli, fujo, ulalamishi usio na sababu, uchochezi na uchonganishi wenye nia ya kutaka kuondoa amani utulivu uliotamalaki nchini.
Kifupi Chadema imekua chama cha ubabaishaji.Nilitegemea wangeitumia ngekewa ya kushinda majimbo mengi kama shamba darasa la kuonesha tofauti lakini, wabunge wake wamejigeuza kuwa wabunge wa kitaifa wakiyatelekeza majimbo yao na kuwaacha wapiga kura wao yatima. Si Wabunge si Madiwani wa Chadema wote wamekimbia majukumu na wajibu wao wamebakia na ulalamishi usio na faida.
Dhima ama shabaha ys chama chochote cha siasa ni kuwa na mtaji wa kutosha wa wanachama utakaokiwezesha kushika dola.Kwa maana wanachama ndio uhai wenyewe wa chama. Chadema ndani ya miaka hii mitatu imepukutisha wanachama wapenzi na mashabaiki wengi wasio na idadi kutokana na kuchanganyikiwa kisiasa baada ya kuona Ndg. John Pombe Joseph Magufuli akichapa kazi na kuleta maendeleo kwa kasi ya kipanga hivyo wamepoteza focus na wengine wamebakia kuzurura huko Ulaya wakiombaomba na kuitukana nchi yao.
Tungojee mnyausho wao mtakatifu mwaka 2020.
Augustino Chiwinga