Siasa za kitoto na kishamba zitatuletea maendeleo bandia

haha

JF-Expert Member
Apr 21, 2013
1,400
1,628
Kiukweli Tanzania bila kukaa na kutafakari kwa kina tutsjikuta tunapiga mark time miaka nenda rudi na kujidifu kwa maendeleo bandia.

Najaribu kutazaa yanayojitokeza baada ya kuondoka kwa Aliyekuws rais wa awamu ya Tano.

Kiukweli Mh alijenga nidhamu ya uoga!!! Walinyima watu kufikiri na kutoa maamuzi ya mstakabali wao!!! Aliamua nani awe mbunge na nani asiwe mbunge.

Kiukweli kama taifa tulikuwa tunapotea pakubwa.

Sasa yanayojiri ni wazi alijenge taifa lililojaa viongozi waona na wanafiki tuu
Sasa wabunge ndio wanadhihirisha hili.

Mfano wabunge wa kagera kukataa mkoa wa kagera usimegwe ili kuanzisha mkoa wa Chato

Alipokua hai hili hawakudhubutu kulizungumza hata kama walikuwa na hoja za msingi kwani wangeshughulikiwa sawasawa!! Sasa chato ingekuwa ni maendeleo lakini bandia

Mfano mwingine ni hili LA deni LA taifa!!nimeshangaa sana kusikia wabunge wakikalama kutaka deni lifanyiwe "auditing" kwan ni kubwa mno!! Wakati ule wabunge wa ccm walimsifu kwa kujenga nchi kwa pesa za ndani!!!MH akawa anatamba nchi yetu ni Tajiri

Sasa wanatwambia ndani ya miaka mitano tuu kakopa Mara tatu ya watangulizi wake waliotawala miaka kumi!?? Mbaya zaidi wabunge hawa leo wanaolaumu walitaka kumuongezea Muda ili aendelee !?? Sasa walikuea hawajui kama nchi INA kopa!

Je wabunge hawahusishwi!??kufanya maamuzi!?je maamuzi yalikuwa ya MTU mmoja!! Je so siasa za kitoto za maendeleo bandia!?

Juzi ,PAC kamati ya bunge ilikagua hesabu za ATC !! Ikasema shirika linajiendesha kwa hasara kubwa mno!!zaid ya billion 500!!! Sasa nani alinunua ndege bila kuwa na mipango!??sio siasa za kitoto hizi!? Je hayo sio maendeleo bandia!?

ndege nyingi tulizonunua kwann zitupe hasara kiasi hiki!? Haya maendeleo sio ya bandia!?
Mh!! Hakutaka MTU kumkosoa kabisa!!

Ni siasa za ajabu kabisa mwisho wa siku wananchi wanabeba gharama na umasikini unatamalaki!

Waliokuwa wanamsifia sasa wanageuka!??

Siasa za kitoto mwisho wake ni maendeleo bandio
 
Katiba inapaswa iongezewe nguvu na makali, ili asitokee mtu akajifanyia atakacho na wengine wakaufyata kisa huyo mtu ni rais. Rais kama raia yeyote anatakiwa kuwa chini ya sheria za nchi.
 
Hii Nchi ina makima wengi sana,Ujinga Umetamalaki katika Nchi yetu.uwezo wa mwananchi mmoja kutafakari mambo kuchuja na kupata jawabu sahihi kuhusu mambo muhimu ya kitaifa na uraia kwa ujumla ni Mdogo mnooo..

Katika mazingira kama hayo ni ngumu sana Wananchi kuwawajibisha viongozi wao katika mambo yanayowahusu wao..
 
Hii Nchi ina makima wengi sana,Ujinga Umetamalaki katika Nchi yetu.uwezo wa mwananchi mmoja kutafakari mambo kuchuja na kupata jawabu sahihi kuhusu mambo muhimu ya kitaifa na uraia kwa ujumla ni Mdogo mnooo..

Katika mazingira kama hayo ni ngumu sana Wananchi kuwawajibisha viongozi wao katika mambo yanayowahusu wao..
Hao viongozi wenye kwenye vyama vyao hawa wajibiki kutoka na makosa yao unategemea wawajibike kwenye ngazi ya taifa.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom