Siasa za kiimla zimetuletea mkwamo wa kiuchumi. Tunavukaje kibiashara?

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,240
9,527
Habari zenu wanajamii?

Ilitegemewa leo nisimame hapa kuendelea kuilaumu na kuilaani serikali kwa mkwamo wa maisha mtaani ambayo kimsingi inapaswa kulaumiwa na kulaaniwa, ila biashara zinakufa na hili si jambo jema.

Nadhani tunaofanya biashara tupeane mbinu za kuvuka katika kipindi hiki na lawama na laana tuzipunguze kidogo kwaajili ya 2020.
Ukisimamisha biashara ukapoteza mtaji na kupotea sokoni huwa ni vigumu sana kurudi hata katika hali uliyokuwa nayo awali!
Brand yako ikishapotea ni kazi sana kuirudisha kwenye akili za wateje.

Hapa natoa mbinu chache na wengine watajazia ili kumsaidia mfanyabiashara kusurvive kipindi hiki!

1.Wasiliana mapema na taasisi za fedha unazofanya kazi nazo- wanaokukopesha.
Waeleze ugumu unaopitia na mbinu ulizopanga kukabiliana nao.
Waeleze mahitaji yako ya kifedha na hakikisha kusuasua kwako hakutakuwa kwa kushtukiza kwao.

2.Andaa budget na cash flow zitakazoendana na uhalisia wa hali ya biashara. Tegemea wakati mbaya zaidi kibiashara na ujiandae kukabiliana nao.

3.Hakikisha unapata taarifa za mtiririko wa fedha katika biashara yako kwa usahihi na kwa wakati. Lengo ni kujua kila shilingi katika biashara yako inakwenda wapi.
Hakikisha unapata hesabu za mauzo zilizo sahihi na kama unazalisha bidhaa hakikisha unapata hesabu sahihi ya bidhaa unazozalisha.
Pambanua taarifa utakazohitaji na hakikisha unazipata kwa wakati ili uweze kufanya maamuzi sahihi!.

4. Punguza gharama zisizo za lazima wakati huu kwa kutumia busara! Hakikisha huduma kwa wateja haziathiriwi na punguzo hili la gharama.
Angalia sehemu tano ambazo unatumia gharama kubwa zaidi kisha uzipunguze kwa busara. Kisha angalia tano zinazofuata na ufanye vivyo hivyo.
Endelea mpaka ujiridhishe gharama zimepungua.

Nisiwachoshe kwa leo mimi tu peke yangu.
Nikiona thread hii ina tija nitaendelea wakati mwingine.
Karibuni kwa michango ya mbinu zaidi.
 
Back
Top Bottom