Siasa za kiafrika zina tija?


Kasimba G

Kasimba G

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2011
Messages
2,660
Likes
664
Points
280
Kasimba G

Kasimba G

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2011
2,660 664 280
Kati ya vitu ambavyo nikitafakali nabaki na huzuni, ni jinsi siasa za kiafrika zinavyoendeshwa, wanasiasa wengi wa kiafrika hawajui lengo la siasa na zaidi saana hawajui jinsi ya kuucheza mchezo wa siasa kwa manufaa mapana ya jamii.

Mifano hai ni kwa wale wanokumbuka jinsi papa Mobutu alivyokuwa akicheza mchezo wake wa siasa kwa manufaa yake na kusahau manufaa mapana zaidi ya siasa katika jamii iliyokuwa inamzunguka, inasemekana Mobutu aliruhusu mfumo wa vyama vingi, lakini akaunda zaidi ya robo tatu vyama vyake! Huu ndio udhaifu wa sisi waafrika, kila wakati hujifikilia zaidi manufaa yetu binafsi!

Lengo la elimu ni kuisaidia jamii husika, mfano Medical Drs Huwa wanatibu wanadamu wenye matatizo ya afya ili wawe vizuri kwa ujenzi wa jamii husika, Engineers, hutengeneza means za kurahisisha maisha kwa mwanadamu, mfano Gari, ndege, Machineries za aina mbali mbali, Ujenzi wa nyumba, barabara, Madaraja ili mradi jamii husika inanufaika, Sociologist huangalia matatizo ya kijamii na kuyatatua, n.k. Lengo la elimu na siasa mala nyingi halina tofauti, ukimkuta mtu mwenye elimu ambaye badala ya kuisaidia jamii yeye anaizulumu jamii, kiufupi ni kuwa anakuwa hajaelimika!

Hivyohivyo ukimkuta mwanasiasa ambaye badara ya kufikilia maslahi mapana ya jamii yeye anajiendekeza na umimi wake anakuwa amepungukiwa akili, lakini bahati mbaya wasomi wengi wa kiafrika na wanasiasa wetu, huwa hawazingatii lengo haswa la wao kuwepo, badala yake hujiangalia wenyewe tuu! Huwa wanakuwa wamekosa sifa ya kuwa wanasiasa au wana taaluma!

Ukiangalia kwa makini utangundua kitamaduni, karibu nchi nyingi za kiafrika zina namna moja ya upunguani huu, selfishness at its maximum, sasa huku kwetu siasa za namna hiyo zimeekuwepo na watu badala ya kuwahuzunikia mapunguani wa jinsi hiyo, hutokea mala nyingi tunawasimia na umafia wao, hivyo mwisho wa siku jamii nzima inakuwa na mapunnguani, kwakuwa tunakuwa tunajua madhala ya siasa za namna hiyo lakini kwa kuwa labda kwa namna moja au nyingine zinakuwa na manufaa kwetu, huwa tunajifanya mapuunguani na kuzishabikia!

Hapa nina maana kuwa we need a fair ground kwa kufanyia siasa zetu, hebu jamii zetu zibadirike na tuzingatie haki zaidi badala ya ubinafsi. Wanasiasa vijana lazima mjifunze kutunza utu wenu msiwe rahisi kununuliwa, utanunuluwa ndio lakini kumbuka hautadumu kitambo, utakuwa umekwisha kisiasa na jamii haitakuja kukuamini hata siku moja, zaidi ya hayo, hebu basi tufungue macho na tujue maslahi mapana ya jamii zinazotuzunguka, tuwe kwa ajiri ya jamii tusiwe kwa ajira ya Ubinafsi!

Wanasiasa vijana mjifunze kutoka kwa mifano iliyo hai, Huwa nasoma vitabu vingi tuu, lakini huwa nasoma pia biblia, Wasaliti katika jamii huwa wapo, chukulia mfano wa Petro na Yuda katika biblia, wote walikuwa wasaliti, lakini Petro alitubu na tunaona jinsi alivyokuwa nguzo ya ukristo baadaye, lakini Yuda hakutubu akajinyonga, Huu sio mfano wa kidini tuu, ni mfano wa kijamii, Wanazuoni wanasema Petro alisaliti lakini hakuwa amepewa kitu ndio maana ikawa kwake rahisi kutubu, lakini Yuda alipeewa hela ndio maana ikawa ngumu kwake kutubu zaidi ya kuona suruhisho rahisi kwake zaidi ni kujinyonga! Vijana tusipende kupewa hela ili tufanye usaliti, tutajinyonga mwisho wa siku.

Wanasiasa tujichunge na roho za usaliti zitatumaliza!

Nawasilisha.
 

Forum statistics

Threads 1,237,886
Members 475,775
Posts 29,304,753