Kenya 2022 Siasa za Kenya: Rais Uhuru Kenyatta atangaza rasmi kumuunga mkono Raila Odinga uchaguzi mkuu, August - 2022

Kenya 2022 General Election
..Kenyatta ni bangi kwelikweli.

..Ni ajabu kwa Raisi anayetoka madarakani kutokumuunga mkono makamu wake ambaye anayejaribu kuwa Raisi.
Ni ajabu kwa katiba yetu ! Huko duniani kwenye katiba za maslahi ya wanachi sio ajabu.
Uhuru ana practice the best of their constitution, ! Freedom, ! Huku kwetu move kama hiyo haiwezekani

Caged birds , think that flying is an illness!
 
Ruto alikurupuka sana kumletea Kenyatta ujuaji, akaacha kufanya majukumu yake ya makamu wa Rais akaanza kampeni, hiki ndicho kilichomkera Kenyata hadi ameamua kumwaga mboga na ugali, namuona Odinga njia nyeupe kuwa Rais wa Kenya jana alifunika sana Mombasa.

Kama sio Ruto uhuru asingekuwa rais.
 
Hapo kwenye suala la ukabila hoja yako haina mashiko. Katiba ya Kenya ya sasa haijatatua tatizo la ukabila. Ndio maana wakapendekeza mpango wa BBI (kama unajua ni nini). Hata ukifuatilia kampeni za uchaguzi mkuu zinazoendelea sasa, utagundua kwamba ukabila ndio unaendesha siasa za Kenya kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande mwingine, katiba ya sasa ya Tanzania ina misingi imara sana ya umoja wa kitaifa. Ni kweli ina mapungufu mengi na inahitaji mabadiliko makubwa, lakini ndiyo inayotufanya tusiwe na mawazo ya kikabila kwa kiwango kikubwa.
Ukabila unakumbatuwa siku zote na udikteta kama haujui Hilo. Kwenye Demokrasia ukabila unatoweka wenyewe.
Na Demokrasia ni zao la katiba Bora.

Hivi unajua Kenya ilikotoka chini ya Katiba ya Chama kushika hatamu na kila mtu kufuata Nyayo chini ya KANU?

Kwa Sasa wapo mbali sana. Uhuru Mkikuyu asingeweza kueleweka Kwa wakikuyu Kwa kumsapoti Raila Mjaluo.
Kuundwa Kwa BBI ni matokeo ya Katiba Bora ambayo Kwa kiwango kikubwa ilikubaliwa na waKenya wengi.

Tukubali Kwa Ile Kenya ya zamani Kwa Sasa imebadilika sana. Ukabila ulikua ni mbaya mana uliingia mpaka kwenye vyombo vya Dola.
Wakati wenzetu wamejitahidi kuhama Huko kwetu tunaelekea Huko na tunakwenda Kwa kusuasua Lakini ni wazi tunaelekea kwenye ukabila. Katiba inayompa Rais mamlaka makuba ni lazima iendane na ama Ukabila au Udini au Ukanda mana nguvu ya kuteua na kutengua ni lazima iendane na upande wa kutegemea Vinginevyo unaweza ukahujumiwa.

Lakini katiba iliyompunguzia mamlaka Rais inaipa mihimili mingine nguvu ya kuhimili misukiosuka ya kisheria na kisiasa.

Hivi katiba ya kifalme inampa inaendesha nchi ama kikanda au kidini au kikabila full stop. Kagame watoto wake anawapa position za juu kwenye vyombo vya Dola hakuna wa kuhoji, Museveni n.k. Lakini Katiba ya Kenya Rais hawezi kuendelea wakikuyu nakuwaacha makabila mengine, ataulizwa na hata kushtakiwa.


Hali hiyo inampa nafasi ya kusimamia haki bila kutegemea kabila Moja .

Ili utawale bila kukosolewa ni lazima uwe na nguvu ndani ya Dola yenye watu wa upande wako zaidi. Ili wengine waogope kwenda kinyume na wewe. Unaweza ukaengemea kwenye Udini ,ukabila au Ukanda.
Kuna awamu ilishambuliwa sana Kwa ukabila lakini ilifanya vile ili iwanyooshe watu. Unajipanga mpaka chini. Kila idara ili wasaliti waonekane mapema.Yote ni nguvu ya Katiba inayotoa mwanya wa kuteua kila mtu kwenye nafasi ya juu.

Ukabila unatakiwa udhibitiwe na sio eti sisi watanzania hatuna. Ukabila Kwa wananchi huku chini haupo lakini watawala wanautumia sana ili wajihakikishie kuwa wanapata kura.
Bahati mbaya wanaofanya hayo katiba inawalinda.

Angalia ishu ya Wamasai kule Ngorongoro. Woga ni ukabila unaotumika badala ya hoja. Watu wanatumia ukabila kisiasa badala ya hoja za kitaalam na za kimaendeleo.

Kenya tunajua ilipotoka na ilipo.
Watu maarufu wa makabila mengine walikua wanauawa sana ili TU Wakikuyu wasipate wapinzani ndani ya Dola. Moi aliwekwa kimkakati TU lakini Dola yote ilikua ni ya Wakikuyu. Ajira ndani ya vyombo vya Dola kipao mbele ilikua ni wakikuyu. Sasa Kenya imebadilika sana ni lazima tuwasifu. Watanzania tulikuwa pazuri lakini tunapuuza Misingi ya kuimarisha umoja ambayo ni katiba inayotambua ushindani wa haki kisiasa.

Umoja wetu ulikua wakati wa Chama kimoja na katiba yake.
Sasa Kuna vyama vingi na lengo ni kuingia madarakani unategemea Nini Kwa Watawala kama sio kutumia katiba inayowapa nguvu kuendelea kutawala na kudhibiti wapinzani wao.Hapo lazima waangalie mbinu za kudhibiti Dola. Mbinu Moja wapo ni ukabila ,Udini na Ukanda, mpaka umri Sasa ni kigezo Cha kuvuta chawa wadumu.
 
Ni ajabu na kweli...

Na kwa wafuatiliaji wa siasa zà Kenya, hivi Kenyatta na Odinga wanatokea chama kimoja cha siasa au ni wanachama wa vyama tofauti...?

Anyway, vyovyote iwavyo. Ila iko hivi;

Kwamba, kwa mujibu wa taarifa ya habari ya leo saa 2 usiku huu ya ITV - Tanzania, Uhuru Kenyatta ametangaza rasmi kumuunga mkono hasimu wake mkubwa wa kisiasa mzee Rails Odinga katika uchaguzi mkuu nchini humo utakaofanyika mwezi August, 2022.

Kwani hapa TZ hili haliwezekani? Nani atashangaa iwapo mwaka 2025 Rais Samia Suluhu Hassan [CCM] akawashangazà wana CCM kwa kumuunga mkono Freeman Mbowe au Tundu Lissu [CHADEMA]?
Mimi navyoona Uhuru na Ruto wametengeneza mgogoro fake Udinga atakuja kushituka Ruto yuko Ikulu siasa ni sayansi ya kucheza na akili za watu
 
Basi hapo ndio unajiona umeandika kizungu kabisa, duh.
Kwa katiba iliyopo ni ngumu sana kukwapua kura za Raila labda kura zisitoshe.

Jamii mara nyingi haipendi uhuni wa kisiasa. Wanaonufaika na uhuni wa kisiasa ni kakundi ka watu wasiozidi 2000. Hao wanaleta propaganda za kihuni Kwa maslahi yao.
 
Abduli Nondo acha ujuaji wewe
emoji16.png
emoji16.png
emoji16.png
Kwa nini hukulamba sukari?
 
Raila na Jomo (The Fathers walitokea mbali) hizi familia zina historia ni basi tu hapa katikati kupishana..., kwahio sio Ajabu...
 
Ruto alikurupuka sana kumletea Kenyatta ujuaji, akaacha kufanya majukumu yake ya makamu wa Rais akaanza kampeni, hiki ndicho kilichomkera Kenyata hadi ameamua kumwaga mboga na ugali, namuona Odinga njia nyeupe kuwa Rais wa Kenya jana alifunika sana Mombasa.
Ruto alitaka kumuua kenyatta, ndege sliyotaka kupanda uhuru ilikua iangukesasa Raila ndo akamvuta pembeni uhuru na kumtonya asipande ile ndege toka hapo nasikia ndo ikawa bifu la ukweli,
Kama lowasa alipoona JK atagombea awamu ya pili wakati makubaliano ilikua waachiane(sidhani kama kweli),na lowasa akaanzisha harakati za kutaka awe mwenyekitiwa ccm, zikazimwa.
Ruto nae alikuwa na agreement na uhuru uli waachiane term, na uhuru akavunja makubaliano
 
Kenya waketuacha Mbali sana sana Karne nzima kisiasa.
Wakati Kenya imeepukana na ukabila na Udini na Ukanda ambao uliwasumbua Kwa muda mrefu chini ya Katiba ya kijinga inayolea utawala wa kidikteta na uchama Dola KANU, sisi chini ya CCM ndio asubuhi kabisa watu wanaendekeza UCCM,uchadema ,uACT, ujamaa feki ,ubepari uchwara, ukabila Ukanda,Udini,ujinsia,ujana ,uprofesa ,uDr ,darasa la Saba,udigree na ujinga mwingi unaotugawa wakati Mwalimu alijitahidi kiasi Fulani kutuambia kuwa tuungane na kuwa kitu kimoja.

Kenya Chini ya Katiba Mpya ukabila unafutika Kwa Kasi ya ajabu . Anachaguliwa mtu sio Kabila au dini yake .

Tanzania Chini ya Katiba ya maslahi tuliyonayo tunalea janga baya sana linalozidi kutugawa japo wachache wanafurahia mana kwao umoja wa watanzania sio shida alimradi wapate madaraka. Rais akiwa na madaraka makubwa sana anaweza akajenga hata mfumo wa familia yake kufanya anachotaka bila kuulizwa na yeyote. Bunge limewekwa mfukoni, Mahakama pia na vyombo vya Dola. Kila taasisi ipo chini ya mtu mmoja anayeteua nafasi zote zenye maslahi makubwa.Nani asiyetaka kuwa Jaji Akatajirika haraka haraka na mbaya zaidi wanateuliwa Vijana ambao wanamatamanio Mengi hivyo wanapenda sifa na kuwa na Mali na anasa za kila aina. Nani asiyetaka vyeo vikubwa kwenye vyombo vya Dola. Nani asiyetaka Ubunge wa kupewa Kwa nguvu ya Dola. Nani anayetaka biashara zake zifilisiwe?
Akitokea Rais mwenye hulka ya Ukanda ule wa akina Museveni na Kagame akajichomeka hapa Tanzania Chini ya Katiba hii tuliyonayo tutalia na kusaga meno. Ni rahisi sana kutumia katiba hii na kuipeleka nchi unakotaka. Ukitaka kuleta Udini ni rahisi sana. Ukitaka ukabila ni rahisi sana hasa Kwa makabila makubwa kama Wamasai,wasukuma,wachaga,wanyakyusa,Wangoni, Wagogo ,Wairaki na jamii yao n.k. Ni rahisi sana. Unaweka chawa wengi halafu unateua marafiki, unateua wa mrengo unaoutaka kuanzia kwenye Dola mpaka bungeni. Anayeleta chokochoko anapewa kesi ya Ugaidi na kufilisiwa. Akienda mahakamani anakutana na Jaji aliyepewa offer ya ujaji ili ale maisha. Ukienda Polisi unakutana na wanaoahidiwa uIGP wa Mchongo .
Ukienda bungeni unakutana na wabunge wa kupewa sio kuchaguliwa. Unaamua TU uitawale nchi kibabe, kidini ,kikabila ,kikanda, kirafiki,kifisadi ,Kijamaa,kibepari n.k. utakavyoona inafaa.

Katiba Mpya ni muhimu sana. Mtu mwenye sifa Bora atapata uongozi TU kupitia Chama chochote. Huu ujinga wa katiba chakavu wa kupata viongozi wabovu Kwa kubebwa na Dola na vyama chini ya chaguzi zilizojaa rushwa inabidi tuachane nao.

Tupate Katiba mpya ili tushindanishe hoja,uwezo na maono ya mtu sio ujinga ule wa kampeni kupambwa na nyimbo za wasanii na vijembe badala ya sere ,midahalo n k.
Nonsense
 
Back
Top Bottom