Kenya 2022 Siasa za Kenya: Rais Uhuru Kenyatta atangaza rasmi kumuunga mkono Raila Odinga uchaguzi mkuu, August - 2022

Kenya 2022 General Election
Tanzania hatuwezi kuwa na vita ya ukabila kwa sababu tuna makabila mengi sana pengine kuliko nchi yoyote Africa .
Jaribu kufuatilia habari kijana.

Tanzania ina makabila yasiyozidi 130,. Congo DRC ina makabila 680. Mali ina makabila 720. Ivory Coast ina makabila 350. Kwahiyo usilishwe pumba na media za CCM kwamba Tanzania ina makabila mengi kuliko nchi zote barani Africa.
 
Ni ajabu na kweli...

Na kwa wafuatiliaji wa siasa zà Kenya, hivi Kenyatta na Odinga wanatokea chama kimoja cha siasa au ni wanachama wa vyama tofauti...?

Anyway, vyovyote iwavyo. Ila iko hivi;

Kwamba, kwa mujibu wa taarifa ya habari ya leo saa 2 usiku huu ya ITV - Tanzania, Uhuru Kenyatta ametangaza rasmi kumuunga mkono hasimu wake mkubwa wa kisiasa mzee Rails Odinga katika uchaguzi mkuu nchini humo utakaofanyika mwezi August, 2022.

Kwani hapa TZ hili haliwezekani? Nani atashangaa iwapo mwaka 2025 Rais Samia Suluhu Hassan [CCM] akawashangazà wana CCM kwa kumuunga mkono Freeman Mbowe au Tundu Lissu [CHADEMA]?

Nashangaa Sana mnaposema : Nairobi VS Dar es salaam

Hawa watu wanatushinda kila kitu
 
Jaribu kufuatilia habari kijana.

Tanzania ina makabila yasiyozidi 130,. Congo DRC ina makabila 680. Mali ina makabila 720. Ivory Coast ina makabila 350. Kwahiyo usilishwe pumba na media za CCM kwamba Tanzania ina makabila mengi kuliko nchi zote barani Africa.
Congo drc ina lugha na lahaja 700 plus , sio makabila !
Wachaga tu hapa wana lugha zaidi ya 10 na ni kabila moja
Wazaramo nao wana lahaja zao kadhaa na ni kabila moja

Sent from my RMX3085 using JamiiForums mobile app
 
Ni ajabu na kweli...

Na kwa wafuatiliaji wa siasa zà Kenya, hivi Kenyatta na Odinga wanatokea chama kimoja cha siasa au ni wanachama wa vyama tofauti...?

Anyway, vyovyote iwavyo. Ila iko hivi;

Kwamba, kwa mujibu wa taarifa ya habari ya leo saa 2 usiku huu ya ITV - Tanzania, Uhuru Kenyatta ametangaza rasmi kumuunga mkono hasimu wake mkubwa wa kisiasa mzee Rails Odinga katika uchaguzi mkuu nchini humo utakaofanyika mwezi August, 2022.

Kwani hapa TZ hili haliwezekani? Nani atashangaa iwapo mwaka 2025 Rais Samia Suluhu Hassan [CCM] akawashangazà wana CCM kwa kumuunga mkono Freeman Mbowe au Tundu Lissu [CHADEMA]?
Kwamba Samia aje kuunga mkono upinzani kwa siasa za Tanzania ? Kwa katiba hii hii yetu?
Covid 19 wansurvive bungeni kwa matamko tu , wanna know why?

Uhuru ni mkikuyu leo hii anamuunga mkono Jaluo, sio kwa kupenda , bali katiba yao kwa sasa imeondoa madaraka makubwa kwa Rais, hana la kufanya zuri zaidi ya kulinda maslahi mapana ya nchi yake .

Ukabila unaenda kupotea kenya ,

Sent from my RMX3085 using JamiiForums mobile app
 
Mwacheni odinga nae ashinde tu aiseh!! kipindi kile alishinda sema tu kenyatta alitumwa dola kubaki madarakani!!

O
Kwa Tanzania hopefully, itatokea pia....

Wako wawili ambao safari zao kisiasa zinafanana na Mzee Raila Odinga Odinga....

1. Urais Zanzibar alikuwepo gwiji la siasa za Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (bahati mbaya ni marehemu). Obviously, angekuwa hai bila shaka Mwinyi Jr, angemuunga mkono mwaka 2025 the same way Uhuru Kenyatta kafanya kwa Odinga...

2. Kwa u - Rais wa Tanganyika & JMT yupo Prof. Ibrahimu Lipumba mwenye rekodi ya kugombea mara nyingi bila mafanikio. Kilichoharibu integrity ya Prof Lipumba kama mwanasiasa nguli wa upinzani ni kuuza utu wake kwa shekeli kwa mawakala wa shetani - CCM

Kwa sasa tuna wanasiasa wawili ama watatu tu Tanzania walio upande wa tabaka la wananchi wa kawaida dhidi ya tabaka la watawala wanyonyaji na wakandamizaji chini ya CCM.....

Hawa ndiyo tunaoweza kuwatazama, kuwasikiliza na kuwaamini kwa lolote wasemalo na kuelekeza;

1. Tundu Antipas Mughway Lissu [CHADEMA]

2. Freeman Aikael Mbowe [CHADEMA]

3. Zitto Zubeir Ruyagwa Kabwe [ACT - Wazalendo] japo huyu kwa kiasi Fulani kwa mujibu wa jamii, integrity yake is little bit questionable & compromising....

However, to me, I still believe, Zitto Kabwe has a great chance to be Raila Odinga of Tanzania if only he stop thinking about himself - selfishness...!
 
Kenya waketuacha Mbali sana sana Karne nzima kisiasa.
Wakati Kenya imeepukana na ukabila na Udini na Ukanda ambao uliwasumbua Kwa muda mrefu chini ya Katiba ya kijinga inayolea utawala wa kidikteta na uchama Dola KANU, sisi chini ya CCM ndio asubuhi kabisa watu wanaendekeza UCCM,uchadema ,uACT, ujamaa feki ,ubepari uchwara, ukabila Ukanda,Udini,ujinsia,ujana ,uprofesa ,uDr ,darasa la Saba,udigree na ujinga mwingi unaotugawa wakati Mwalimu alijitahidi kiasi Fulani kutuambia kuwa tuungane na kuwa kitu kimoja.

Kenya Chini ya Katiba Mpya ukabila unafutika Kwa Kasi ya ajabu . Anachaguliwa mtu sio Kabila au dini yake .

Tanzania Chini ya Katiba ya maslahi tuliyonayo tunalea janga baya sana linalozidi kutugawa japo wachache wanafurahia mana kwao umoja wa watanzania sio shida alimradi wapate madaraka. Rais akiwa na madaraka makubwa sana anaweza akajenga hata mfumo wa familia yake kufanya anachotaka bila kuulizwa na yeyote. Bunge limewekwa mfukoni, Mahakama pia na vyombo vya Dola. Kila taasisi ipo chini ya mtu mmoja anayeteua nafasi zote zenye maslahi makubwa.Nani asiyetaka kuwa Jaji Akatajirika haraka haraka na mbaya zaidi wanateuliwa Vijana ambao wanamatamanio Mengi hivyo wanapenda sifa na kuwa na Mali na anasa za kila aina. Nani asiyetaka vyeo vikubwa kwenye vyombo vya Dola. Nani asiyetaka Ubunge wa kupewa Kwa nguvu ya Dola. Nani anayetaka biashara zake zifilisiwe?
Akitokea Rais mwenye hulka ya Ukanda ule wa akina Museveni na Kagame akajichomeka hapa Tanzania Chini ya Katiba hii tuliyonayo tutalia na kusaga meno. Ni rahisi sana kutumia katiba hii na kuipeleka nchi unakotaka. Ukitaka kuleta Udini ni rahisi sana. Ukitaka ukabila ni rahisi sana hasa Kwa makabila makubwa kama Wamasai,wasukuma,wachaga,wanyakyusa,Wangoni, Wagogo ,Wairaki na jamii yao n.k. Ni rahisi sana. Unaweka chawa wengi halafu unateua marafiki, unateua wa mrengo unaoutaka kuanzia kwenye Dola mpaka bungeni. Anayeleta chokochoko anapewa kesi ya Ugaidi na kufilisiwa. Akienda mahakamani anakutana na Jaji aliyepewa offer ya ujaji ili ale maisha. Ukienda Polisi unakutana na wanaoahidiwa uIGP wa Mchongo .
Ukienda bungeni unakutana na wabunge wa kupewa sio kuchaguliwa. Unaamua TU uitawale nchi kibabe, kidini ,kikabila ,kikanda, kirafiki,kifisadi ,Kijamaa,kibepari n.k. utakavyoona inafaa.

Katiba Mpya ni muhimu sana. Mtu mwenye sifa Bora atapata uongozi TU kupitia Chama chochote. Huu ujinga wa katiba chakavu wa kupata viongozi wabovu Kwa kubebwa na Dola na vyama chini ya chaguzi zilizojaa rushwa inabidi tuachane nao.

Tupate Katiba mpya ili tushindanishe hoja,uwezo na maono ya mtu sio ujinga ule wa kampeni kupambwa na nyimbo za wasanii na vijembe badala ya sere ,midahalo n k.
Comment bora ya mwaka
 
Back
Top Bottom