pakaywatek
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 4,641
- 6,267
Nimekua na wiki mbili sasa humu Kenya ninayoyashuhudia kwenye uteuzi wa wagombea ndani ya vyama ni hatari kwa uchaguzi ujao na huenda mwaka huu wakaingia kwenye machafuko tena kama hawatakua makini.
Nikianza na chama cha ODM, hiki chama nusura kiingie kwenye machafuko hususan maeneo ya magharibi mwa Kenya kutokana na kutuhumiana kuibiana kura, kuna mgombea moja aliongoza kwa % 80 zikiwa zimebaki Kata mbili tu kuitimisha ushindi wake, cha kushangaza hizo Kata mbili zililetwa kura za kukaribia na idadi ya nusu ya kura za wanachama ambazo awali zilisha hesabiwa na kukuta mgombea moja anaongoza kwa %80, na baada ya kujumuishwa huyu aliyekua na %20 akaongoza kwa %70 kilichofwata ni vurugu mpaka matokeo yakafutwa.
Na huo ni mfano wa maeneo mengi kukumbwa na vurugu na mpaka sasa haijulikani uteuzi utafanyika lini.
Jubilee; hawa baada ya kuona vurugu za ODM waliwacheka sana wakiongozwa na kinara wao Uhuru Kenyatta mpaka wakawakejeli kuwa ODM ndio chanzo cha vurugu nchini ndio maana uchaguzi wao umekumbwa na vurugu na hadi sasa wamevurugika hata hawajui ninani atapeperusha bendera kutoka kwenye muungano bandia kuwania urais.
Kilichotokea; Leo ndo ilikua siku ya uteuzi kwa chama cha jubilee kuteua wawaniaji wa viti mbalimbali kwenye uchaguzi ujao.
Jana huko nyeri eneo kati nchini wasimamizi wa uchaguzi ndani ya chama walifutwa wote na kuteua wapya kutokana na kuhisiwa kupokea rushwa toka kwa wawaniaji na kupelekea hadi Uhuru Kenyatta kutangaza kuwa hawatakubali kutokee vurugu na kusema huo ni mfano wa watakaojiusisha na maswala ya upendeleo, inasemekana tayari kuna sehemu nyingi kuna masanduku ya kura ambayo tayari yana kura kusubiri tu kutangazwa mshindi, na imepelekea leo jubilee kutangaza kusitisha uteuzi nchi nzima.
Inasemekana katika uteuzi wa jubilee kunauwezekano kukatokea vurugu kushinda hata ule wa ODM hasa maeneo ya kati na meru ambapo kuna mgawanyiko mkubwa wa jamii hizo ukizingatia kuwa kuna wanaojinasibu kuwa wako karibu na rais na ndiye amewatuma ingawa Jana rais Uhuru alikanusha kutuma watu wakagombee.
Siasa za Kenya mwaka huu ni tofauti kabisa, na huenda endapo muungano wa NASA ukimsimamisha Raila kwa Mara ya kwanza Uhuru anaweza kupata kura nyingi eneo la magharibi mwa Kenya hii ni kutokana na watu wengi kukasirishwa na uteuzi ambapo wengi wanaamini kuwa Raila ameingilia mchakato wa uteuzi wa wagombea, na hata juzi Uhuru alipokua kisumu mapokezi aliyopata hakuamini, ingawa katikati ya hutuba nyoka alitokea kwenye mkutano hadi kupelekea watu kutawanyika hovyo.
Hivyo pia kwa Raila anawezapata kura nyingi maeneo ya kati kutokana na siasa ambazo jubilee wataendesha, hivyo siasa za Kenya mwaka huu zitakua ni siasa za haina yake, na kama ikitokea vurugu hazitakua vurugu za ukabila tena bali za kiitikadi zaidi, na vurugu za kiitikadi ni mbaya kuliko hata vurugu za ukabila kwa sababu zenyewe ni mke kupigana na Mme,ndugu kwa ndugu nk.
Tuwaombee wakenya wafanye uchaguzi kwa amani.