Siasa za Kamanda Muroto na Kifo cha Sheikh Rashid Bura

chaliko

Senior Member
Apr 1, 2019
180
802
Amani iwe ndugu zangu wa Jamii Forum.

Nimeisikiliza kwa Makini taarifa ya RPC wa Dodoma Ndugu Muroto juu ya Kifo cha Ndugu yetu Mpendwa Marehemu Sheikh Rashid Bura ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa The Dalai Islamic Centre.

Awali ya yote napenda Jamii ifahamu kuwa;

a/ Sheikh Rashid Bura alikuwa ni Rafiki yake na Kamanda Muroto.

b/ Sheikh Rashid Bura alikuwa ni Mmiliki wa ZAMZAM PRE & PRIMARY SCHOOL.

c/ Sheikh Rashid Bura alikuwa akijishughulisha na shughuli nyingine pia (Naiweka kapuni kwa Sasa) licha ya kuwa ni Mmiliki wa Shule.

Kamanda Muroto ameficha mengi juu ya Kifo cha Sheikh Rashid Bura. Hapa naomba nielezee utata uliopo juu ya Kifo chake.

UTATA.

1. SAFARI,
a/ Marehemu Sheikh Rashid Bura alisafiri kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam siku ya Ijumaa Tarehe 20/12/2019 na siyo Tarehe 21/12/2019 kama alivyosema Kamanda Muroto. Tarehe 21/12/2019 ilikuwa ndiyo siku ya Kongamano / Mkutano huo wa Kidini. Katika Safari hiyo waliondoka watu wawili katika chombo kimoja cha usafiri.

b/ Tarehe 22 Marehemu alirudi Dodoma lakini akiwa amemuacha aliyeenda naye Safari huko Dar es salaam. Alipofika Dodoma alienda Kuswali katika MSIKITI wa NUNGE na baadae kuelekea Ofisini kwake.

NB: KWENYE TAREHE YA SAFARI KUNA JAMBO HALIPO SAWA.

2. MAWASILIANO,
Marehemu Sheikh Bura, aliwasiliana na Ndugu zake kwa njia ya Maongezi kwa mara ya Mwisho Jumamosi Usiku akiwa Dar es salaam. Baada ya hapo Simu za Ndugu zake hazikupokelewa tena na Meseji hazikujibiwa pia. Siku ya Jumapili Mawasiliano yaliyopatikana Pekee ni UJUMBE wa WHATSAPP ambao uliwapa taarifa Ndugu kuwa Amewasili Dodoma. Baada ya hapo hakukuwa na Mawasiliano tena.

NB: SHEIKH BURA HAKUWAHI KUTOPOKEA SIMU AU KUKOSEKANA HEWANI SIKU ZOTE AMBAZO AMEKUWA AKISAFIRI. KUTOPOKEA SIMU NA KUKOSEKANA KWAKE HEWANI KUMELETA MKANGANYIKO MKUBWA.

3. MAZINGIRA YA KUPATIKANA KWAKE,
Mazingira ya kupatikana kwa Sheikh Bura yana utata mwingi Sana,

a/ Sheikh Bura alipatikana Ofisini kwake siku ya tatu baada ya Mauti yake tena Mwili ukiwa umeanza kuharibika. Maswali ya kujiuliza,

i/ Je Ofisi yake haina Msaidizi wa Kazi ambaye angeweza kugundua kifo chake?

ii/ Je Ofisi za Jirani hawakuweza kusikia hata harufu ya kitu kinachotoa harufu kutoka Ofisini kwake?

b/ Polisi na Ndugu walipofika Ofisini kwake walikuta Mlango umefungwa na walipo uvunja na kuingia ndani walikuta mwili wa Marehemu LAKINI UFUNGUO HAUKUWEPO MLANGONI NA HATA NDANI PIA. Swali la kujiuliza, NI NANI ALIMFUNGIA SHEIKH BURA KWA NJE?

(Kumbuka kabla ya Mlango kuvunjwa uliagizwa UFUNGUO WA AKIBA kutoka Nyumbani na ulipoletwa uliingia hadi ndani lakini haukuweza kufungua Mlango. Je KITASA kilibadilishwa na ni nani alibadilisha KITASA?)

c/ Mwili wa Marehemu Sheikh Bura ulikutwa na Vazi lake la Kanzu lakini likiwa na Damu. Swali la kujiuliza, JE DAMU HII KWENYE KANZU YA MAREHEMU ILITOKA WAPI?

4. SIKU YA MAZISHI,
Siku ya Mazishi 26/12/2019 Mwili wa Marehemu Sheikh Bura ulitolewa Mochwari na kupelekwa Nyumbani kwake na Gari la Polisi na hata kutoka Nyumbani kwenda eneo la Mazishi (MAKABURI YA CHAMWINO / CHINANGALI) Mwili wake ulipelekwa na Gari la Polisi. Polisi pia walitoa basi lao kwa ajili ya kubeba wafiwa. Basi hili lilikwama Kwenye eneo karibu kabisa Ofisi ya Serikali ya Mtaa. Maswali ya Kujiuliza,

i/ Je ni utaratibu wa kawaida kwa Magari ya Jeshi la Polisi kubeba Mwili wa Marehemu mpaka Nyumbani na Eneo la Maziko?

ii/ Je ni utaratibu wa kawaida kwa Basi la Jeshi la Polisi kubeba wafiwa?

iii/ Uwepo wa Jeshi la Polisi kwenye eneo la tukio kulimaanisha nini?

(Kumbuka pia pale MOCHWARI MWILI ULITOLEWA NJE NA PUNDE KIDOGO KURUDISHWA NDANI, hii ilisababishwa na Mmoja wa Ndugu wa Marehemu KUKATAA KUSAINI REPORT YA MAREHEMU KULINGANA NA TAARIFA YA POLISI NA DAKTARI PIA. Je nini kilimfanya KIJANA akubali ku-saini REPORT YA DAKTARI?)

Nawasilisha.

Zaidi, soma;

Unahoji!?,unatuhumu!?, Au hoja yako Nini na Zaid swali kwako wewe ndie ulie funga mlango!? Umejuaje Kama mlango ulifungwa kwa nje!?

Maswali Zaid kwako.unawezaje kujua kuwa she narehemu huwa anapokea simu akiwa dar!?

Je ulimpigia na hakupokea simu!? VIP mlipanga Safari moja na narehemu!?

Naona hili suala unalijua vizur ni Rai yangu jitokeze usaidie polisi.

Huenda kupitia wewe Kama ni mroto au muuaji yeyote atakamatwa.unaijua hii ishu vizur Kama unazo data wapo wengi wa kuwapa jitokeze uwe shujaa kwa hili tutakuwa nyuma yako
 
Amani iwe ndugu zangu wa Jamii Forum.

Nimeisikiliza kwa Makini taarifa ya RPC wa Dodoma Ndugu Muroto juu ya Kifo cha Ndugu yetu Mpendwa Marehemu Sheikh Rashid Bura ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa The Dalai Islamic Centre.

Awali ya yote napenda Jamii ifahamu kuwa;

a/ Sheikh Rashid Bura alikuwa ni Rafiki yake na Kamanda Muroto.

b/ Sheikh Rashid Bura alikuwa ni Mmiliki wa ZAMZAM PRE & PRIMARY SCHOOL.

c/ Sheikh Rashid Bura alikuwa akijishughulisha na shughuli nyingine pia (Naiweka kapuni kwa Sasa) licha ya kuwa ni Mmiliki wa Shule.

Kamanda Muroto ameficha mengi juu ya Kifo cha Sheikh Rashid Bura. Hapa naomba nielezee utata uliopo juu ya Kifo chake.

UTATA.

1. SAFARI,
a/ Marehemu Sheikh Rashid Bura alisafiri kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam siku ya Ijumaa Tarehe 20/12/2019 na siyo Tarehe 21/12/2019 kama alivyosema Kamanda Muroto. Tarehe 21/12/2019 ilikuwa ndiyo siku ya Kongamano / Mkutano huo wa Kidini. Katika Safari hiyo waliondoka watu wawili katika chombo kimoja cha usafiri.

b/ Tarehe 22 Marehemu alirudi Dodoma lakini akiwa amemuacha aliyeenda naye Safari huko Dar es salaam. Alipofika Dodoma alienda Kuswali katika MSIKITI wa NUNGE na baadae kuelekea Ofisini kwake.

NB: KWENYE TAREHE YA SAFARI KUNA JAMBO HALIPO SAWA.

2. MAWASILIANO,
Marehemu Sheikh Bura, aliwasiliana na Ndugu zake kwa njia ya Maongezi kwa mara ya Mwisho Jumamosi Usiku akiwa Dar es salaam. Baada ya hapo Simu za Ndugu zake hazikupokelewa tena na Meseji hazikujibiwa pia. Siku ya Jumapili Mawasiliano yaliyopatikana Pekee ni UJUMBE wa WHATSAPP ambao uliwapa taarifa Ndugu kuwa Amewasili Dodoma. Baada ya hapo hakukuwa na Mawasiliano tena.

NB: SHEIKH BURA HAKUWAHI KUTOPOKEA SIMU AU KUKOSEKANA HEWANI SIKU ZOTE AMBAZO AMEKUWA AKISAFIRI. KUTOPOKEA SIMU NA KUKOSEKANA KWAKE HEWANI KUMELETA MKANGANYIKO MKUBWA.

3. MAZINGIRA YA KUPATIKANA KWAKE,
Mazingira ya kupatikana kwa Sheikh Bura yana utata mwingi Sana,

a/ Sheikh Bura alipatikana Ofisini kwake siku ya tatu baada ya Mauti yake tena Mwili ukiwa umeanza kuharibika. Maswali ya kujiuliza,

i/ Je Ofisi yake haina Msaidizi wa Kazi ambaye angeweza kugundua kifo chake?

ii/ Je Ofisi za Jirani hawakuweza kusikia hata harufu ya kitu kinachotoa harufu kutoka Ofisini kwake?

b/ Polisi na Ndugu walipofika Ofisini kwake walikuta Mlango umefungwa na walipo uvunja na kuingia ndani walikuta mwili wa Marehemu LAKINI UFUNGUO HAUKUWEPO MLANGONI NA HATA NDANI PIA. Swali la kujiuliza, NI NANI ALIMFUNGIA SHEIKH BURA KWA NJE?

c/ Mwili wa Marehemu Sheikh Bura ulikutwa na Vazi lake la Kanzu lakini likiwa na Damu. Swali la kujiuliza, JE DAMU HII KWENYE KANZU YA MAREHEMU ILITOKA WAPI?

4. SIKU YA MAZISHI,
Siku ya Mazishi 26/12/2019 Mwili wa Marehemu Sheikh Bura ulitolewa Mochwari na kupelekwa Nyumbani kwake na Gari la Polisi na hata kutoka Nyumbani kwenda eneo la Mazishi (MAKABURI YA CHAMWINO / CHINANGALI) Mwili wake ulipelekwa na Gari la Polisi. Polisi pia walitoa basi lao kwa ajili ya kubeba wafiwa. Basi hili lilikwama Kwenye eneo karibu kabisa Ofisi ya Serikali ya Mtaa. Maswali ya Kujiuliza,

i/ Je ni utaratibu wa kawaida kwa Magari ya Jeshi la Polisi kubeba Mwili wa Marehemu mpaka Nyumbani na Eneo la Maziko?

ii/ Je ni utaratibu wa kawaida kwa Basi la Jeshi la Polisi kubeba wafiwa?

iii/ Uwepo wa Jeshi la Polisi kwenye eneo la tukio kulimaanisha nini?

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
1.Umeshasema Kamanda alikuwa rafiki wa marehemu, kama kuna huo urafiki basi rafiki anaweza kuelekeza matumizi ya gari la ofisi kwaajili ya msiba wa rafiki
2. Marehemu wamfahamu vyema, kwanini usimuulize mhudumu wa ofisi au huyo MTU mwingine aliyesafiri naye akueleze chanzo?
3. Hiyo kazi ya marehemu usiyotaka kuitaja, je huoni umeficha taarifa muhimu kwa jamii inayofuatilia hilo tukio?
Polisi wanajitahidi sana kiutendaji, kuwaelekezea lawama kwa kila tukio tunawaonea.
NB: Wewe kama unafahamu chanzo cha msiba, ieleze JF badala ya kutuhumu idara za serikali
 
b/ Sheikh Rashid Bura alikuwa ni Mmiliki wa ZAMZAM PRE & PRIMARY SCHOOL.

c/ Sheikh Rashid Bura alikuwa akijishughulisha na shughuli nyingine pia (Naiweka kapuni kwa Sasa) licha ya kuwa ni Mmiliki wa Shule

Sent using Jamii Forums mobile app

Alikuwa TISS?
Je inawezekana ni clearance of evidence?
Ipi?
Ni tukio gani lilitokea katika himaya yake /Eneo lake? Ambalo ni tishio kwa usalama wa viongozi/watawala?

Mahusiano binafsi je?
 
naandika tena hz ni juhudi za kuua sekta binafsi tena matajiri wazawa!!Mengi alishaandika!matajiri wazawa hawapendwi!!!Bora uwe na asili YA ASIA!!!RUGE,MUFRUKI,SAMI,MENGI NA WENGINE WANAFUATA!!!MBONA BAKHRESA,MO,MANJI HAWAUAWI????
Siku yako ikifika utakufa tu. Ulitaka afe Bakharesa baada ya Mengi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Polisi kuhusika moja kwa moja kwenye mazishi sijashangaa sana. Maana marehemu alikuwa afisa upelelezi wa polisi kwa muda mrefu tu na huko ndiko alikofahamiana na RPC Muroto na ameshawahi kuwa afisa ulinzi ikulu kipindi cha Mwl nyerere.
Pia yanayosemwa mtaani alikuwa anatumikia TISS mpaka umauti unamfika.

Kuhusu mengine uliyoyaandika kama ni kweli na mimi pia umenifanya nijiulize maswali mengi bila majibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NAVYOFAHAMU TISS OFFICERS HUWA HAWASTAAFU...

Back
Top Bottom