Siasa za Igunga na vituko vya Tendwa!

Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,423
2,045
Hapa kuna utata kama sheria zimekiukwa alafu kampeini zinaendelea wapi tunaelekea jama sheria,kanuni na maadili ya uchaguzi.Tendwa na NEC wameshindwa kusimamia sheria then nini umuhimu wa sheria hizi?
 
TBC1 wamerusha mahojiano na Mh Tendwa na pia mkutano wa Tume ya Uchaguzi na waandishi wa habari. Ingawa habari zenyewe zimekuwa fupi fupi tu, nimemshangaa Tendwa kwa kulalamikia kuwa sarakasi za kampeni na kuishia hapa kana kwamba hana lolote analoweza kufanya. Ameishia kusema kuwa angetamani uchaguzi huo ufutwe.

Tume nayo imeishia kulaani fujo zinazoendelea bila kueleza hatua watakazochukua!!
 
Nao wanaishia kulalamika tuuu? kama JK na Pinda wanavolalamika hata ktk mambo ambayo ungetegemea watoe directives? basi mbombo ngafu!
 
Nao wanaishia kulalamika tuuu? kama JK na Pinda wanavolalamika hata ktk mambo ambayo ungetegemea watoe directives? basi mbombo ngafu!


Unajua sababu yake? Ni kwa sababu wavunjaji wakubwa wa sheria na kanuni na chama cha magamba. Ingekuwa ni CDm hatua kali zingechukuliwa dhidi yao.

kama vile akina Kasulumbai na wenzake kushitakiwa na polisi kwa kumvua hijab Dc, wakati wafuasi wa CCM wanawapiga hati mahututi wafuasi wa upinzani lakini hata hawakamatwi.
 
timu ya refa inafanya vurugu, unategemea refa atapiga filimbi??

hili liserikali rojorojo halina maana.
 
Wote ni magamba tu hakuna wa kumtegemea. Tume imejaa magamba hawawezi wajibika kwa mwajiri wao si atawatimua na kuwaweka vibaraka wengine, ndo maana wanaufyata km mbwa koko anayekula vinyesi vya walevi! Ndo maana tunataka Katiba mpya itakayotutoa kwenye huu upuuzi wa magamba
 
Kuna kila dalili za uchaguzi mdogo katika jimbo la igunga kufutwa, Katika taarifa ya habari ya TBCI Msajili wa Vyama Mr.Tendwa ameonesha pendekezo la kufutwa kwa uchaguzi huo kwa kigezo kwamba watu wengi watakufa siku ya uchaguzi hivyo kufuta uchaguzi huo kutaokoa maafa. Jambo hili lina ukweli kiasi gani, mnaofuatilia uchaguzi huo kwa karibu naomba mtujuze kulikoni, nini kinaendelea huko na kama kweli hoja ya Tendwa ya kufuta uchaguzi ina msingi wowote.
 
Jamani jamani huyu tendwa hamjui kuwa ni msanii tuu ni mchumia tumbo asiejua anachokifanya.
 
hv kwanini mtu anapewa madaraka juu ya kitengo fulani kama hawezi kutoa uamzi ajiudhuru maake majukumu yamemshinda,yaani ninamachungu na viongozi wasio timiza wajibu.
 
sijui tu huyo bwana ikulu itakua inamemwambia sisiem ikishindwa tu na kazi hana ndo mana anatamani uchaguzi ufutwe
 
Upendeleo wa kisiasa na ukandamizaji wa kidikteta vikikomaa huzaa kama yale yanayoendelea Syria. Viongozi na watanzania wapenda amani haya mambo ni ya kuyapiga vita. Ccm wasidhani wanaweza kucheza rafu tu na amani ikaendelea kuwepo milele.
Unajua sababu yake? Ni kwa sababu wavunjaji wakubwa wa sheria na kanuni na chama cha magamba. Ingekuwa ni CDm hatua kali zingechukuliwa dhidi yao.

kama vile akina Kasulumbai na wenzake kushitakiwa na polisi kwa kumvua hijab Dc, wakati wafuasi wa CCM wanawapiga hati mahututi wafuasi wa upinzani lakini hata hawakamatwi.
 
Kama viongozi wenye mamlaka nao wanalalamika nani sasa afanye maamuzi...
Sio CCM jamani.............hi hawa!!
katuni-majira-8-2-113.jpg
 
kama wakiufuta basi siyo kwa sababu ya vurugu bali ni kwa ajili ya kuona kuwa CCM haiwezi kushinda na hivyo watafanya hivyo kuiokoa CCM.
 
Source TBC-1 taarifa ya habari saa 2.00kamili usiku 26-09-2011,Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa alisema hivi,"Kama ningekuwa na mamlaka kwa yanayotokea Igunga ningefuta uchaguzi ule hata sasa ninavyozungumza",akaendelea,"yanayotokea pale ni kama Polisi hakuna,Serikali haipo,kila kitu hovyo kabisa".Sasa sijui kama amejianzia au ndio wakuu wamemtupa,maana maumivu ya kichwa hawa Magamba huanza polepole!
 
Ukiona hivyo ujue huo ni uthibitisho wa kwamba CCM maji ya shingo!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom