Siasa za Humphrey Polepole zaiponza TRC. Safari za treni Dar - Kilimanjaro zaanza kupuuzwa, Wizara ya Uchukuzi yalaumiwa

Hahahaha, binafsi napenda treni kwa ajiri ya kula bata tu , huwa nikifika Zambia napanda treni ya Tazara ,
Safari na bata mwanzo mwisho
Ili upate tiketi wamesema uende na barua ya Mwenyekiti wa mtaa, au Passport au kitambulisho cha Taifa.... Kama una ugomvi na mwenyekiti wa mtaa ndo umekula kwako mazima...
 
Sasa baada ya December na Wachaga kurudi kwenye shughuli zao na treni utasimama siyo??
Wachagga kazi ipo . huwa ikifika december usafiri wa mabasi ubongo huwa ni washida sana hasa karibu na krismass bei za mabasi yanapanda hata hivyo watu wanakosa usafiri mpaka daladala kubwa huruhusiwa kubeba abiria kuwapeleka moshi. Pia haitoshi watu hukaa stendi ya ubongo na kukosa usafiri na kila mwaka wanalalamika usafiri shida.

Leo Mh. Rais kaazisha usafiri wa treni kwenda moshi ambayo itapunguza matatizo ya abiria na mizigo. Lakini wachagga bado wanalalamika wanasema hawapandi hiyo ni siasa kaleta makufuli. Makonda aliwasema ni kweli kabisa.

Mimi nawafananisha wachagga na enzi za nabii mussa alipokwenda kuwaokoa kutoka kwa farao kwa ajili ya mateso walipokuwa njiani wanaondoka wakamwa mbia nabii mussa tuna njaa tutapata wapi chakula nabii mussa akamuomba mungu chakula kikawa kinakuja kutoka mbinguni kila siku wanakula chakula fresh.

Mwisho wa siku wakambwambia nabii mussa tumechoka na chakula chako
 
Jana nilikuwa club moja maarufu ya pombe hapa kimara baruti, baada yakusomwa taarifa hyo na tv pendwa ya wachaga kuhusu treni kuzinduliwa kwenda moshi, wachaga wote walikipuka kwa shangwe na vigeregere kwa furaha kuu. Lakini nilibifunza yafuatayo. 1. Kumbe wachaga wengi ndo wanywaji wapombe kuliko kabila zingine. 2. Ma bar_med wengi niwachaga, na 3 kumbe wameteseka mda mrefu sana. Maana magufuri babalao ndo ilitawala baa nzima
Kwanza kwenda Moshi December is not mandatory lakini Wachaga wamekuwa wanaenda kila end of the year kwa sababu kwenda na kurudi mtu anashindwaje kutenga laki mbili au tatu kwa mwaka mzima?
 
Unatesekaje jombaa?? Huwezi pata laki moja ya nauli ya Bus kwa mwaka mzima?? Unashindwa kufanya bookings Kilimanjaro bus kwenda Moshi na kurudi na kulipia in advance?? Mnakwama wapi? Kama huna gari huna hata jamaa yako mwenye gari mnachanga mafuta mnaenda wote na kurudi??
Mimi nadhani tujikite kwenye msingi wa kwamba kuna unafuu wa usafiri utapatikana.Tunatesekaga jamani.Ni kitu kizuri sana.Haya mambo ya kuangalia watu badala ya mafanikio hayanisaidia sana ninapokuwa na mke na watoto wangu Ubungo kondakta ananitajia elfu arobaini kwa kichwa,tena kwa dharau.Natoa pongezi zangu kwa hatua hii, 'irrespective' ya hali watakayoanza nayo.
 
Mi naona tatizo liko na shirika la reli lenyewe, hivi wamepata majibu ya kwanini njia hiyo ilitelekezwa awali na sasa kuna uhitaji wa huduma hiyo umejitokeza. Kuna wanaosema reli itasaidia kusafirisha mizigo lakini tafiti zinaonesha kuwa reli zetu zina garama kubwa kuzidi hata magari ya mizigo. Hicho ndo kiini cha tatizo. Sioni kwa njia chakavu kama hiyo inayohitaji matengenezo kila siku itakuwa na faida kwa TRC. Kama yangekuwa mawazo yangu wangeboresha huduma ya reli Kigoma na Mpanda badala ya kuhangaika na hiyo njia. Kwa utaalam wangu mdogo reli ina faida inaposafirisha mzigo kuanzia km 600 na kuendelea chini ya huo umbali huo usafirishaji kwa njia ya barabara unakuwa na gharama ndogo zaidi.
Umeongea vizuri na kitaaluma... Mfano nimefuatilia huo ukarabati walioufanya kwenye hii reli coz inapita jirani kabisa na home huko kijijini. Yaani ni ukarabati very lightly, hasa kwenye lile tuta la reli ambalo for 25 years lilitelekezwa mawe yote hakuna, maji yakawa yanapita juu yake etc. Sikuona tuta likiimarishwa kwa kujengwa imara na kusindiliwa, sasa nina wasiwasi sana hasa treni za mizigo zenye mabehewa mpaka 20 yaliyojaa mizigo.
 
Kitendo cha Polepole kutumia mali ya umma ili kutafuta umaarufu kwa chama chake kilichochoka cha CCM kimewatafakarisha baadhi ya wadau wa usafiri, ambao wameweka msimamo wa kutokutumia usafiri huo abadani.

Polepole si kiongozi wa serikali wala si Ofisa wa Shirika la reli ama wizara husika, haifahamiki alikopata kiherehere cha kuingilia mipango isiyomhusu na kujichomeka kwenye kinachoitwa uzinduzi wa safari za treni Kilimanjaro - Dar, Watanzania si wajinga kiasi hicho.

Wizara ya Uchukuzi na Shirika la Reli msitumike kishamba namna hii, sasa kwa taarifa yenu wadau hawatatumia huo usafiri wenu wa kisiasa. Wameapa kuendelea kutumia Ngorika, Dar Express, Kidia one, Kilimanjaro na Sai Baba.

Sasa siku mkianza kutukanwa hadharani kwa kuchelewesha gawio msimlilie mtu, mfuateni Polepole awasaidie.

Sidhani kama litapata abiria, ninavyoona mimi, abiria wengi wanapenda kusafiri asubuhi. Na wengi safari za kulala njiani hawapendi.

Ukitaka kujua angalia mabasi kama Kilimanjaro au Dar Ex kila siku yainajaa abiria wakati bei zao ni tofauti na mabasi yanayopakia abiria stendi.

Lakini abiria hawapandi mabasi ya bei nafuu wanaangalia yanayofika muda muafaka.

Na kiherehere cha Polepole asipoangalia vizuri ndiyo watu watalisusa kabisa.
 
Back
Top Bottom