Siasa za Humphrey Polepole zaiponza TRC. Safari za treni Dar - Kilimanjaro zaanza kupuuzwa, Wizara ya Uchukuzi yalaumiwa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,580
217,962
Kitendo cha Polepole kutumia mali ya umma ili kutafuta umaarufu kwa chama chake kilichochoka cha CCM kimewatafakarisha baadhi ya wadau wa usafiri, ambao wameweka msimamo wa kutokutumia usafiri huo abadani.

Polepole si kiongozi wa serikali wala si Ofisa wa Shirika la reli ama wizara husika, haifahamiki alikopata kiherehere cha kuingilia mipango isiyomhusu na kujichomeka kwenye kinachoitwa uzinduzi wa safari za treni Kilimanjaro - Dar, Watanzania si wajinga kiasi hicho.

Wizara ya Uchukuzi na Shirika la Reli msitumike kishamba namna hii, sasa kwa taarifa yenu wadau hawatatumia huo usafiri wenu wa kisiasa. Wameapa kuendelea kutumia Ngorika, Dar Express, Kidia one, Kilimanjaro na Sai Baba.

Sasa siku mkianza kutukanwa hadharani kwa kuchelewesha gawio msimlilie mtu, mfuateni Polepole awasaidie.
 
Wacheni uzushi, inaonekana wengi bado hamjamuelewa Magufuli, treni sasa hadi Moshi, wakazi wa Kilimanjaro kunufaika pakubwa, hayo mengine hakuna mwenye haja nayo. Magufuli anafanya mambo ambayo yataandika historia ya Afrika upya.

..nani anayekwenda huko ana muda wa kupoteza kupanda treni?

..badala ya kukarabati hiyo reli, bora fedha zingeelekezwa kujenga barabara za vijijini.

..serikali imejifanyia tu huu mradi bila kushirikisha wadau na wananchi.
 
Wacheni uzushi, inaonekana wengi bado hamjamuelewa Magufuli, treni sasa hadi Moshi, wakazi wa Kilimanjaro kunufaika pakubwa, hayo mengine hakuna mwenye haja nayo. Magufuli anafanya mambo ambayo yataandika historia ya Afrika upya.
Labda kama umezaliwa jana
 
Chaguo la kupanda train au kuacha hilo litabaki la abiria kutokana na sababu zao za kiuchumi, access ya usafiri mwingine au sababu zingine zozote zenye manufaa (inaweza kuwa ata mizigo anayobeba).

Kwa ivyo hiyo train angejenga mtu yeyote au kunadiwa na mtu yoyote kutokana na uwezo wa mfuko wa mtanzania wa kawaida na bei ya nauli itapata tu abiria wa kutosha kwenye vituo vyote itakayosimama.

Hila CCM propaganda imewashinda wao siku hizi hata maiti za watu maarufu wanakimbilia jeneza tells you kwamba ubunifu Lumumba kwa sasa hakuna tena.
 
..nani anayekwenda huko ana muda wa kupoteza kupanda treni?

..badala ya kukarabati hiyo reli, bora fedha zingeelekezwa kujenga barabara za vijijini.

..serikali imejifanyia tu huu mradi bila kushirikisha wadau na wananchi.
Wewe unaangalia upande wa abiria tu..., ambao reli haina uzito sana nao.

Reli hiyo ni mhimu sana kusafirishia mizigo, kama saruji toka Tanga na Dar es Salaam badala ya kutegemea toka Kenya kwa bei nafuu.

Mimi naunga mkono sana kukarabatiwa kwa reli zetu zote zifanye kazi vizuri.

Hii haina maana barabara zitaacha kuboreshwa.
 
..nani anayekwenda huko ana muda wa kupoteza kupanda treni?

..badala ya kukarabati hiyo reli, bora fedha zingeelekezwa kujenga barabara za vijijini.

..serikali imejifanyia tu huu mradi bila kushirikisha wadau na wananchi.
Mkuu;
Wewe unaishi kwenye viunga vya nchi za nje mpaka unaelekea kuzeekea huko bila kurudi Tanzania utajua hali ya maisha ya wananchi hasa wa kipato cha chini nchini!

Halafu tatizo lako unaangalia upande wa abiria pekee badala ya kuangalia usafirishaji wa mizigo ambao ndio muhimu zaidi.

Nina uhakika treni hii itapata abiria wengi na mizigo mingi sana!

Wasiwasi wangu ni kwa baadhi ya wafanyakazi wa sekta ya usafiri wa mabasi kukosa kazi baada ya wateja wao kuhamia kwenye usafiri wa treni.
 
Erythro, haya mawazo mepesi mepesi hivi mtayaacha lini?

Yaani watu wakapande au wasipande gari la moshi kwa sababu ya mtu kama Polepole? Hebu wewe lifikirie hili tena.
Polepole anaongeza thamani gani kwenye chama chake anapojihusisha na mradi huo? Hivi mtu mwenye akili timamu ataanza kusifia CCM kwa vile Polepole kajitokeza na kupiga kelele kwenye usafiri huo?

Erythro, kuna mambo ya mhimu zaidi yanayostahili kushikiwa bendera kuliko hili uliloleta hapa.

Mimi nakuuliza. Hivi uchaguzi mkuu mwakani mtashiriki mkiwa na uhakika wa kuambulia hata viti vitano tu kwa hali ilivyo sasa?
Kuna kichwa rafiki yangu, kuhusu jambo zito kama hili.
 
Mkuu Erythrocyte, kwanza hii hoja sii kweli, ni uzushi tuu, na ikitokea root hiyo kukosa abiria, sababu itakuwa ni time taken na sio sababu ya Polepole. Tena kwa Christmastime hata wakipeleka treni 3 per day, zote zitajaa, ila after holiday season ndio I can't tell.

Sio wengi wanafahamu kuwa jambo lolote la kimaendeleo linalofanywa na awamu hii, ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM, Ilani ndio mkataba kati ya chama na wananchi kilipokifanya kishindi na kuaminiwa kuunda serikali, hivyo utekelezaji ilani ndio msahafu wa serikali na sera zote za nchi zinatokana na ilani hiyo.

Humphrey Polepole sio tuu ndiye Katibu Mwenezi responsible kutangaza msendeleo ya utekelezaji ilani, pia ni mjumbe wa CC ya NEC ya CCM, responsible for sera, hivyo anapaswa awepo katika kila tukio la kimaendeleo la kitaifa ili ashuhudie utekelezaji wa ilani, na sio yeye tuu, wenyeviti, makatibu na waenezi wa CCM nchi nzima wanapaswa wawepo kwenye kila shughuli ya maendeleo ya mkoa, wilaya, kata, vijijini, mitaa, vitongoji, mashina, matawi, hadi kwenye nyumba kumi kumi kwa mjumbe wa nyumba 10, na hii ndio sababu pekee inaiwezesha CCM kutawala milele Tanzania, kwasababu CCM ndicho chama pekee kilichotapakaa nchi nzima, na kuwafikia wananchi wote.

Na kiukweli CCM kinakubalika sana, uthibitisho ni huu ushindi wa kishindo cha asilimia 99.9% wa serikali za mitaa, kama utangulizi tuu, kazi hii nzuri ya CCM itakamilishwa mwakani kwenye uchaguzi Mkuu wa 2020, ambayo CCM itazoa ushindi wa kisulisuli wa asilimia 99.99%, na kuirudisha rasmi Tanzania kuwa nchi ya chama kimoja cha siasa, baada ya 2020, kazi itakuwa ni moja tuu, kuwaletea maendeleo Watanzania, tutapaa kimaendeleo, tutakuwa kama China, kimaendeleo.


P
 
Hivi mnawajua wachaga au mnawasikia?

Nani alisema moshi tunashida ya kupanda hayo matolori?

Hiyo reli ilikufa kwakua haikuwa na tija, na hata sasa haina tija.

Hakuna mchaga utakayemsafirisha kwenda moshi kwa saa 18 kisa tofauti ya Tsh 4000 kwenye basi.

Itakufa tena na tena.
 
wakupinga.com
..nani anayekwenda huko ana muda wa kupoteza kupanda treni?

..badala ya kukarabati hiyo reli, bora fedha zingeelekezwa kujenga barabara za vijijini.

..serikali imejifanyia tu huu mradi bila kushirikisha wadau na wananchi.
 
Back
Top Bottom