Imekuwa ni kawaida sasa kila migogoro ya kisiasa inapozuka kule Zanzibar akili zetu huaminishwa jambo moja tu. Kwamba matatizo ya kisiasa ya Zanzibar ni ya kihistoria basi na kwa hivyo ni kana kwamba hakuna dawa.
Wasomi wetu huishia hapo na kubaki kimya kuhalalisha mabavu na uonevu dhidi ya wanyonge kwa kuweka vazi la historia.
Kwamba huko nyuma kulitokea uovu wa watawala wa kisultani na wazungu dhidi ya waafrika mpaka yalipofanyika mapinduzi na tunaaminishwa msemo ule wa kutesa kwa zamu na kwamba sasa iachwe historia ya kulipiza visasi kwa vizazi vya Wazanzibari ilimradi tu watawala wanalinda mapinduzi.
Kuna masuali mengi ya kujiuliza kuhusu huu unafiki wa watawala na kibwagizo hiki cha historia.
Kwa mfano
Kuna umuhimu gani wa kukubali kusaini itifaki ya haki za binadamu na utawala bora ilihali unajuwa masharti yatakubana pale unapotekeleza dhana ya kulinda mapinduzi ? viongozi wanafanya unafiki kujifanya wameridhia demokrasia ya vyama vingi huku wakitumia mabavu kuzuiya haki na masharti ya vyama vingi.
Bahati mbaya mazingira ya Zanzibar yanaathiriwa na siasa za muungano na ubaya unakuja pale upande wa pili wa muungano(Tanganyika) inapounga mkono Historia na kuendeleza mpasuko huo.
Kwa hili Tanganyika na watawala (CCM) hawajawahi kuwa katikati(middle man) kuhakikisha wazanzibari wanaungana kwa dhati bali ni hao Tanganyika hutumika kama mkakati wa KUDHOOFISHA UMOJA WA WAZANZIBARI WAKIDHANI KUFANYA HIVYO NDIVYO WANALINDA MAPINDUZI NA MUUNGANO
Haya yanayoendelea sasa yalitokea 1995, 2000, 2005 na 2010. sio mageni.
Kwamba wazanzibari wamekuwa watumwa wa historia na ngoma hii inapigwa na wasomi wetu, wana dini na wanasheria uchwara. Wazanzibari wanyonge wamekosa mtetezi.
Kwa nini miaka zaidi ya 50 ya Mapinduzi hakukuwa na FOCUS ya kuondowa mtafaruku wa visasi badala yake mpasuko unaendelezwa na huhitimishwa kwa siasa za historia?
Mitaala ya kielimu, uchumi na maingiliano hazikutumika kama fursa za kuondowa siasa mbaya badala yake chuki, ubaguzi na uhasama umeendelezwa kwa makusudi ili wazanzibari wasiwe wamoja na hatimae wagawanyike ili wengine wafikie malengo ya kisiasa.
Dunia nayo iko wapi? kule Zanzibar kuna kitisho gani kwa dunia kiasi kwamba haki za wazanzibari hazina nafasi kama zilivyo za binadamu wengine? ama ndio siasa za historia hazipaswi kuingiliwa hata kama zinakiuka misingi ya utawala bora?
Kiburi cha watawala wa Tanzania,ulafi, na ubinafsi kwa upande wa Zanzibar hufichwa kwenye kigaga cha neno historia na hapo utaambiwa tunalinda mapinduzi na muungano.
Siasa za historia Hazina mwisho na watu hawaoni umuhimu wa kufika tamati kuna nini Zanzibar?
Tunasubiri nini tena ikiwa hata Maridhiano yaliingizwa kwenye katiba ya marekebisho ya 2010 kwa nguvu kubwa lakini kwa nini hayastawi yanavunjwa na kunajisiwa yakisimamiwa bila kificho na wahafidhina ambao wanalindwa na serikali zote mbili kwa nini?
Jibu ni moja tu, ili wajanja waendelee kula, kuishi na kufikia malengo lazima wazanzibari wateseke kwa siasa za Historia.
Msikate tamaa wazanzibari iko siku itafika na haiko mbali.
Mungu ibariki Tanzania
Mungu wabariki wazanzibari wote wanyonge.