Siasa za CCM na muungano wa Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa za CCM na muungano wa Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nanchi, Feb 2, 2012.

 1. nanchi

  nanchi Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 66
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Ndugu wanajamvi naomba kufahamu kutoka kwenu kuhusu muungano wa tanganyika na zanziba.1;nini sababu iliyopelekea kuwa na muungano.2;watanganyika na wazanzibar waliafiki?3;viongozi hawa walitumia njia gani kupata maoni ili kuidhinisha huo muungano?inanishangaza pale ninaposia suala la muungano kwenye katiba mpya halijadiliwi.
   
 2. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Msome Joseph Mihangwa kwenye magazeti ya Raia Mwema matoleo ya nyuma. Majibu ya maswali yako yote utayapata.
   
 3. m

  mtanganyikaa Member

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lengo la mwalimu lilikuwa kuiunganisha afrika iwe moja na akaanza na kuunga zanzibar baadaye kenya na uganda. kura ya maoni haikuitishwa. bahati mbaya kenya na uganda wakakataa. sasa sababu ya kuwa nchi mbili badala ya tatu au moja ni uwiano tofauti kati ya zanzibar na tanganyika
   
 4. k

  kicha JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 508
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 180
  Siamini mpaka leo unaulizia majibu ya maswali amabayo yako wazi miaka nenda miaka rudi
   
 5. nanchi

  nanchi Member

  #5
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 66
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Haukulazimishwa kuchangia mm nilitaka kujua na wenye busara wamefanya hivyo,usishobokee usicho kiweza.
   
 6. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Johmbaaa tulia hapa hapa, naingia Maktaba yangu naenda kukuchukulia nondo za kujibu maswali yako!
   
 7. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Hujaridi bado mpemba mbishi ..? Nasubiri nondo hizo yakhe ...
   
 8. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Katika
  kuuangalia muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwanza ni
  vyema zijulikane sababu hasa
  zailizopelekea Tanganyika na Zanzibar
  kufikia uamuzi wa kuungana. Kwa
  mujibu wa mafundisho ya mashuleni
  na vyuoni sababu kubwa za kuungana baina ya Tanganyika na
  Zanzibar ni hizi zifuatazo. Kwanza ni
  udugu wa damu na wenye mizizi
  mirefu uliyopo baina ya wanganyika
  na wazanzibari. Kwa kuirejea historia
  ya mafungamano baina visiwa vya Zanzibar na bara la Afrika itagundulika
  kwamba mafungamano hayo
  yameanzia kwa karne nyingi sana
  nyuma kiasi cha karne ya 15 au 16
  wakati muungano wa Tanganyika na
  Zanzibar uliibuka katikaki ya karne ya 20 ambapo asili za kibantu kwa
  wazanzibari tayari zimeshapotea kwa
  kiasi kikubwa kutokana na
  kuchanganya damu na watu wa asili
  za mbali mbali za kiasia ambao ndio
  wengi zaidi. Hata hivyo asili za wazanzibari ni vyanzo vingi vikiwemo
  Afrika, Pashia, India na Arabia.
  Ijapokuwa Afrika ni miongoni mwa
  vyanzo vya asili za wazanzibari lakini
  ifahamike kuwa ni kutokea sehemu
  mbali mbali za Afrika zikiwemo Tanganyika, Msumbiji, Malawi, Kenya,
  Uganda, Rwanda, Comoro nk. Sababu nyengine inayohusishwa na
  muungano wa Tanganyika na
  Zanzibar ni historia ya ushirikiano kati
  ya chama cha TANU na ASP, ambavyo
  vyote ni vyama vya kupigania
  ukombozi wa watu weusi kupitia harakati za kudai uhuru zilozozuka
  miaka ya 1950 na 60 katika bara la
  Afrika. Hapa ikumbukwe kuwa sio
  chama cha ASP peke yake
  kilichoshiriki mapambano ya
  kumng’oa mkoloni Zanzibar. Bila shaka kilichomvutia Nyerere na
  kuamua kukiunga mkono chama cha
  ASP peke yake na kufanya
  mashiriukiano nacho katika harakati
  za kudai uhuru wa Zanzibar ni ile ile
  itikadi ya mapambano dhidi ya watu wasio na ngozi nyeusi mambo
  ambayo yalikuwa yamepamba siasa
  za Karume. Vyama vyengine vya
  kizalendo vya wazanzibari havikuwa
  na mvuto wowote kwa Nyerere.
  Wakati chama cha TANU kinaongozwa na sera ya “uafrika” katika kupigania
  uhuru na hivyo kuwaunganisha
  watanganyika wote, ASP kwa upande
  wake iliifumania sera ya “ugozi
  mweusi” ikidhania kuwa ndio uafrika
  wenyewe na hivyo kuwatenga wazanzibari wengine. Vyama vya
  TANU na ASP vilisahau kwamba
  asilimia kubwa ya wazanzibari tofauti
  na watanganyika wakiwemo hao
  wenye ngozi nyeusi wana asili zao
  kutoka nje ya bara la Afrika. Muungano ni matokeo ya hofu mbili
  Hizi zilizotangulia kutajwa labda
  zinaweza kuwa sababu ndogo ndogo
  za muungano huu. Sababu muhimu
  hasa zilizopelekea muungano wa
  Tanganyika na Zanzibar ni hofu mbili zifuatazo. Hofu ya ya kwanza ilitokana
  na uwezo mdogo sana wa kijeshi na
  kiulinzi iliokuwanao serikali ya
  mwanzo ya mapinduzi. Nguvu za
  kijeshi na kiulinzi zikitegemea sana
  mizinga ya kichina na kisovieti ya kutungulia ndege pamoja na silaha
  ndogo ndogo (Armit 1986). Uwezo
  huo mdogo wa kujihami
  unawezakuwa ulijenga hofu kwa
  Karume na Nyerere juu ya uwezekano
  wa Sultani na Moh’d Shamte kujipanga na kurudi ili kufanya mapinduzi
  mapya (counter revolution) dhidi ya
  serikali ya Karume. Kutokana na hofu
  hiyo basi Nyrere alimshauri Karume
  kuziunganisha nchi zao ili kupata
  nguvu kubwa ya kiulinzi ya kuihami Zanzibar dhidi ya mapinduzi mapya. Hii
  inaweza kuwa ndio sababu kubwa ya
  Karume kushishitiza kwamba
  muungano huu utakuwa ni wa kipindi
  cha miaka kumi tu ambapo itabidi
  utathminiwe upya kama unahitajika au laa. Karume alifahamu wazi
  kwamba ndani ya kipindi hicho cha
  miaka kumi tayari serukali yake
  imeshajiimarisha vya kutosha kwa
  nguvu za kijeshi. Hofu ya pili ni ile iliyozifanya dola za
  magharibi kuiona serikali mpya ya
  mapinduzi ya Zanzibar kuwa
  ingeweza kuwa angamizo la ubepari
  katika ulimwengu na bara la Afrika.
  Ushiriki wa Babu na wakomyunisti katika mapinduzi ya 1964 iliiifanya
  serikali mpya ya mapinduzi kuwa ni
  tishio kwa Marekani na dola za
  magharibi. Hofu hii ya nchi za
  magharibi inathibitishwa na simu ya
  balozi wa marekani nchini Tanganyika wakati huo bwana William Leonhart
  alioituma kwa wizara ya mambo ya nje
  ya serikali ya marekani siku ya tarehe
  27 Aprili 1964 : “Sina wasiwasi kwamba
  watanganyika wanategemea kuwa
  wakomyunisti waliomo katika serikali
  ya Zanzibar watazimwa kwa
  kufunikwa na kutofungamana
  upande wowote kwa Tanganyika, lakini kutokana na kasi na nguvu za
  mwendo wa wakomyunisti
  wanaokwenda mbio nchini Zanzibar
  na sio kuitishia ka kuitumilia hali
  katika njia ambazo serikali ya
  Tanganyika haitoweza kuzifikiria. Ninaamin kwamba ni muhimu Nyerere
  apewe msaada wa kimya kimya wa
  kiasi kikubwa iwezekanavyo na nchi
  za magharibi tokea mwanzo” (Armit
  1986). Ingawa wengi wa makomred
  wakiongozwa na Babu waliukataa
  kwa nguvu zote muungano huo lakini
  Bwana Ali Sultan Bin Issa anasema
  katika kitabu cha Burgess cha The
  race, revolution and sruggle for human rights in Zanzibar: “Mimi binafsi sikuona tatizo kuukubali
  muungano. Japo kuwa lengo la
  Nyerere ilikuwa ni kuwameza
  wazanzibari, mimi niliona ni ukombozi
  na jukwaa kubwa zaidi la siasa zetu
  (za kikomyunisti). Pia ni fursa pekee ya kueneza ukomyunisti Tanzania
  bara” (Burgess 2009). Mkataba wa muungano
  Siku ya tarehe 22 Aprili 1964 Nyerere
  na Karume walitia sahihi mkataba wa
  muungano wa Tanganyika na
  Zanzibar. Kumbukumbu za kihistoria
  zinasonyesha kuwa Karume alidhani alitia sahihi mkataba wa kuzitambua
  nchi mbili huru zenye mamlaka kamili.
  Na hivi ndivyo ilivyokuwa katika
  mkataba huu wa mwanzo wa
  muungano. Yaani kwa mujibu wa
  mkataba huo mahusiano ya Tanganyika na Zanzibar kisiasa ni
  kama yalivyokuwa mahusiano baina
  ya Ireland ya Kaskazini na Uingereza.
  Mkataba huu wa mwanzo wa
  muungano uliiachia Zanzibar kiasi
  Fulani cha madaraka yake ya ndani kama vile polisi, mahakama, kilimo nk
  wakati madaraka muhimu kama vile
  mambo ya nje, ulinzi, biashara,
  shughuli za muungano, udhibiti wa
  fedha za kigeni na kuchagua maafisa
  (watendaji) wajuu kabisa wa Jamhuri ya muungano yalikuwa chini ya
  mamlaka yaserikali kuu ya
  muungano. Siku ya tarehe 25 Aprili
  1964 Bunge la Jamhuri ya Tanganyika
  ililiridhia sheria ya muungano kama
  ilivyoridhiwa na baraza la mapinduzi la serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
  Sheria ya muungano wa Tanganyika
  na Zanzibar ilielekeza mambo kumi na
  moja (11) yaliotokana moja kwa moja
  na “mkataba wa muungano”. Mkataba
  wa muungano uliutaka muungano huo hapo mwanzoni udumu kwa
  muda wa miaka kumi (10) tu, yaani
  kutoka 1964 hadi 1974. Hata hivyo
  mkataba hu wa asili ulio na saini za
  waasisi wawili wa muungano huo
  Karume na Nyerere haujulikani uliktokomea hadi leo hii. Muungano wa Tanganyika na
  Zanzibar ulifanywa kukidhi matakwa
  ya kisiasa ya watu wawili, Nyerere na
  Karume. Hakuna kura ya maoni wala
  mazingira yeyote ya kidemokrasia
  yalioandaliwa na kufanywa ili kuwasikiliza wananchi wa pande mbili
  za muungano kama wangependelea
  kuunganishwa kwa nchi zao au laa.
  Kifungu cha 6 (1) cha mkataba wa
  muungano kinasema kwamba “Rais
  wa kwanza wa Jamhuri ya muungano atakuwa Mwalimu Julius Kambarage
  Nyerere”. Kifungu cha 6 (2) kinasema
  “Makamo wa kwanza wa rais kwa
  mjibu wa mabadiliko yanayopatikana
  kwenye aya ya (c) kifungu kidogo (1)
  ya sehemu ya 5 atakuwa sheikh Abeid Karume”. Kuwepo kwa kifungu hichi
  cha 6 kwenye sheria ilioanzisha
  muungano (sheria namba 22, ya 1964
  kwa upande wa Tanganyika ni ishara
  ya wazi wazi kuwa muungano huu
  uliundwa kukidhi matashi ya watu wawili na sio dola mbili. Waasisi hawa
  wa muungano waligawana madaraka
  vile walivyoona wao wenyewe inafaa. Hapa ndipo safari ya Zanzibar
  kumezwa na Tanganyika ilipoanzia.
  Sheria ya muungano namba 22 ya
  1964 ilkuwa na dhamira nzuri pale
  jina la Jamhuri mpya ya muungano
  lilipoainishwa kuwa ni Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar. Kubadilishwa
  kwa jina hilo na kuitwa Jamhuri ya
  muungano wa Tanzania ni kiini macho
  muhimu katika hatua za awali za
  Nyerere za kuimeza Zanzibar. Hakuna
  mwanasiasa au mwanasheria anayeweza kuonyesha ni sheria ipi
  iliyoruhusu kutumika jina la Tanzania
  kwa Jamhuri ya muungano. Lengo
  hapa ilikuwa ni kulipoteza kabisa
  kabisa jina Tanganyika na ndio maana
  hata kulitaja baada ya muungano huo na hadi hivi sasa ni kero kubwa kwa
  viongozi wakuu wan chi wa upande
  wa Tanganyika. Mwanzoni kulitaja jina
  Tanganyika kulifananishwa na nia ya
  kutaka kuvunja muungano. Hadidu za
  makubaliano ya muungano zilibakisha baadhi ya mamlaka ya
  Zanzibar kwa raisi mtendaji wa
  Zanzibar ambaye alikuwa ni makamo
  raisi wa kwanza wa Jahmhuri ya
  muungano ili kulinda masilahi ya
  Zanzibar katika muungano. Hadidu hizo za muungano pia zilibakisha
  baadhi ya mamlaka ya Tanganyika
  kwa raisi mtendaji wa Tanganyika
  ambae alikuwa ni raisi wa kwanza wa
  Jamhuri ya muungano ili kulinda
  masilahi ya Tanganyika katika muungano. Hata hivyo Nyerere
  kimkakati na kwa makusudi aliamua
  kuitupilia mbali haki ya kuwa na raisi
  mtendaji wa Tanganyika ili yeye
  (Nyerere) abakie kuwa ndie mwenye
  nguvu zote na mamlaka ya juu kiutendaji kwa Tanganyika na
  Zanzibar. Hatua nyengine inaonesha
  mtego mkubwa ambao Karume
  alitegwa bila ya kuunasua ni vile
  kukubali kuendelea kutumika kwa
  muda katiba ya Tanganyika kama katiba ya Jamhuri ya muungano
  katika kipindi cha mpito hadi
  itakapotungwa katiba mpya ya
  Jamhuri ya muungano. Jambo hili
  lilimpa nafasi Nyerere kuendesha
  mambo ya muungano vile anavyoona yeye inafaa kama alivyokuwa
  akiiendesha serikali ya Tanganyika
  kwa kipindi cha miaka 13 kuanzia
  mwaka 1964 mpaka mwaka 1977
  ambapo katika ya Jamhuri ya
  muungano ilipatikana. Baada ya kuona mamlaka aliyonayo
  katika Jamhuri ya muungano
  hayamtoshi, Nyerere aliamua
  kuviunganyisha vyama vya TANU na
  ASP baada ya kifo cha Karume. Tarehe
  5 mwezi Februari 1977 wakati Zanzibar ikiwa ndani ya utawala wa
  Maalim Aboud Jumbe vyama vya TANU
  na ASP viliunganishwa na kufanya
  chama kipya chama cha mapinduzi
  (CCM) kilichohodhiwa kimamlaka na
  Nyerere. Huu ulikuwa ni mkakati wa kuusukuma mbele muungano na
  kuyatanua madaraka ya muungano
  huo ndani ya mikono ya Nyerere. CCM
  ilimfanya Nyerere kushika hatamu na
  kutoa maamuzi yasiopingika kama
  vile kulazimishwa kujiuzulu Maalim Aboud Jumbe. Halkadhalika kundi la
  wabunge 55 (G55) lilipozua suala la
  kuanzishwa kwa serikali ya
  Tanganyika mwaka 1992 lilikumbana
  na mkono mrefu wa madaraka ya
  Nyerere na kuzimwa mara moja. Ili kufanikisha malengo ya kuimaliza
  Zanzibar kwa kisingizio cha
  muungano ilimbidi Nyerere
  kuyashikiia madaraka ya Jamhuri ya
  muungano kwa muda wa miaka 20
  na uwenyekiti wa CCM kwa muda wa miaka 10. Hata hivyo baada ya kustaafu Nyerere
  bado aliionekana kuongoza nyuma ya
  pazia. Wengi hawakulitegemea jina la
  “chama cha mapinduzi” kuwa ndio
  jina la chama kipya baada ya
  kuunganishwa ASP na TANU mwaka 1977. Vyama vilivyoungana ni viwili
  kimoja ni TANU kilichoongoza uhuru
  wa Tanganyika na chengine ni ASP
  kilichoshiki mapinduzi ya Zanzibar.
  Hivyo basi wengi walitaraji jina la
  chama kipya litabeba dhima zote mbele yaani ile ya uhuru na ile ya
  kimapinduzi. Kinyume chake dhima ya
  kimapinduzi tu ndio iliyofanya jengo la
  chama kipya. Kwa wale wadau wa
  muungano kwa upande wa Zanzibar,
  wahafidhina wa kimapinduzi waliona kutumika jina “mapinduzi” kwenye
  chama hicho kipya ni fahari ya
  Zanzibar na hatua nyengine ya
  kuyalinda mapinduzi na serikali ya
  mapinduzi kwani kwao kudumu kwa
  mapinduzi ya 1964 ndio masilahi makuu yaliyokuwa yakiwatosha
  katika muungano. Watanzania
  wanaelekea nusu karne tokea
  kuasisiwa muungano wao huku nchi
  mbili zikiwa katika mitafaruku chungu
  mzima iliyozalikana na muungano huo uliokosa muundo wa usawa,
  mitafaruku ambayo hupewa jina la
  kupunguzwa makali yake kwa kuitwa
  “kero za muungano” Changamoto za Muungano
  Hapo awali suala la kuzungumzia
  kasoro za muungano liilichukuliwa na
  watawala kama uhaini. Aliyejaribu
  kufanya hivyo alinyamazishwa kimya
  au alikutana na mkono wa chuma wa serikali. Kufuatia ujio wa mfumo wa
  vyama vingi vya siasa Tanzania, fursa
  ya kuujadili mungano wa Tanzania
  ilipatikana. Hivi sasa mjadala kuhusu
  muungano wa Tanzania na kasoro
  zake sio kitu cha ajabu tena nchini Tanzania. Mambo ambayo mara nyingi
  huonekana kugonga vichwa vya
  mijadala ya muungano au maeneo
  yanayoonekana kuwa na kasoro ni
  haya yafuatayo.
  • Muundo wa muungano • Faida za muungano kwa pande zote
  mbii za muungano Changamoto kubwa ya muungano wa
  Tanganyika na Zanzibar ni muundo
  wa mungano huo. Muundo wa serikali
  mbili ulisimikwa na waasisi wawili wa
  muungano, Nyerere na Karume.
  Baadhi ya wanasiasa, wachambuzi na wananchi wanashauri mabadiliko
  kutoka serikali mbili kuelekea serikali
  moja ili kuifanya Tanzania kuwa nchi
  moja kamilifu, au kuelekea serikali
  tatu na kuifanya Tanzania kuwa
  shirikisho kamili. Utafiti uliofanyika katika mwaka wa 1994 na 2006
  unatoa tofauti ya maoni kati ya
  wananchi wa Tanzania bara, Unguja
  na Pemba kuhusiana na muundo wa
  muungano huo. Hii bila shaka ni
  ushawishi wa misimamo ya vyama vya siasa ambavyo wananchi hao
  wanaviunga mkono katika maeneo
  yao hayo pamoja na masilahi ya
  kisiasa ya sehemu hiyo ndani ya
  muungano. Takwimu zilizokusanywa
  na kamati ya Jaji Nyalali zinaonyesha kwamba muundo wa serikali mbili
  unaungwa mkono kwa kiwango cha
  juu Unguja (63.2%) na kiwango cha
  chini zaidi Pemba (34.6%). Muundo
  wa serikali moja unaonekana kuwa
  na wapenzi wengi Tanzania bara (27.5%) na wapenzi kidogo zaidi
  Pemba (4.1%). Kwa upande wa
  serikali tatu, muundo huu una
  ushabiki mkubwa katika kisiwa cha
  Pemba (32.4%) na ushabiki mdogo
  zaidi Unguja (9.4%). Wakati Zanzibar ilipounganishwa na
  Tanganyika, Karume na Nyerere
  walikuwa na maana tofauti kuhusu
  muungano huo. Wakati Nyerere
  alikuwa na maana ya Zanzibar
  kugeuka kipande kidogo cha ardhi ya Jamhuri mpya, Karume yeye
  hakuelewa hivyo bali alifahamu
  kwamba muungano ulikusudia kutoa
  uhusiano katika mambo Fulani,
  uhusiano ambao hautaleta hasara
  kwa pande zote mbili. Changamoto kubwa ya muungano wa Tanganyika
  na Zanzibar ni muundo wake. Wakati
  duniani kuna mifumo miwili mikuu ya
  muungano, mfumo wa serikali moja
  (unitary) na mfumo wa serikali za
  majimbo (federal), mfumo wa muungano wa Tanzania hauonekani
  kuwa na sifa yoyote kati ya mifumo
  hiyo miwili mikuu iliyopo duniani.
  Mfano wa unitary ni kama vile taifa la
  Marekani (United States of America)
  ambapo madola mengi yameungana na kuunda dola moja kubwa. Mfano
  wa federal ni kama vile taifa la
  Uengereza (United Kingdoms)
  ambapo madola mengi yameungana
  na kufanya dola moja ya Uengereza.
  Pamoja na kuwepo kwa dola moja kubwa ya Uengereza, nchi
  zilizoungana zimewachiwa mamlaka
  yake ya ndani. Nchi zote ndogo
  ndogo zina utiifu kwa serikali kuu ya
  Uengereza. Tanzania kwa upande
  wake ina mfumo wa kipekee katika muundo wa serikali mbili, serikali ya
  Jamhuri ya Muungano ambayo ni
  serikali iliyopotea ya Tanganyika ya
  awali ambayo imeongezewa mamlaka
  zaidi hadi visiwa vya Unguja na Pemba
  na serikali ya Zanzibar ambayo iko chini ya serikali ya Jamhuri ya
  Muungano. Hivyo basi matokeo ya
  muungano huo ni kuifanya serikali ya
  Tanganyika kutumia mamlaka zaidi
  nyuma ya pazia juu Zanzibar kwa jina
  la Jamhuri ya muungano. Kwa kuwa muundo huo uliotokana
  na mawazo na usomi wa Nyerere
  peke yake na hauko duniani kote
  ndio sababu umeshindwa kuzaa
  mfumo mzuri wa kiserikali na kutoa
  uhusiano wa kisiasa na kiutawala unaozikinaisha pande zote mbili
  zilizoungana. Muundo huo
  umesababisha kuzaliwa kwa ukaka
  baina ya pande mbili zilizoungana
  ambazo kabla ya kuungana zilikuwa
  na uhuru na mamlaka sawa sawa. Wako wasomi na wanasiasa
  wanaoutoa kasoro muundo huu wa
  serikali mbili na badala yake
  kupendekeza muundo wa serikali
  moja. Wengi wanaotoa mawazo haya
  ni wanasiasa na wasomi wa Tanzania bara. Ukweli ni kwamba muundo wa
  serikali moja ni kuzidisha matatizo ya
  muungano na kuuvuruga zaidi
  uhusiano mwema wa pande mbili
  uliopo. Mtu anaweza kujiuliza ni kwa
  nini iwe hivyo na ilhali itakapokuwepo serikali moja wazanzibari watakuwa
  na uwezo wa kuzifaidi na kuzitumia
  fursa na rasili mali zote za Tanzania
  bara kama vile wanyama pori, madini
  nk ijapokuwa fursa na rasilimali hizo
  zinakosekana kabisa Zanzibar. Halkadhalika pato la Tanzania bara
  sasa litaweza kutumika kwa ajili ya
  kuchangia maedeleo ya Zanzibar. Muundo wa serikali moja una athari
  nyingi kwa Zanzibar zikiwemo za
  kijamii na kiuchumi. Hapa
  zitazungumzwa chache muhimu.
  Athari ya kubwa zaidi ni kumalizika
  kwa heshima ya utamaduni wa Zanzibar inayoongozwa na misingi ya
  dini ya kiislamu. Utamaduni wa
  Zanzibar wa wazanzibari unatokana
  na dini ya kiislamu ambao una misingi
  ya heshima, upole, ukarimu, utulivu,
  kuaminiana na kushirikiana. Tabia za ulevi, kutovaa nguo za stara, kutokula
  hadharani mwezi mtukufiu wa
  Ramadhani, uhalifu, ujambazi nk ni
  mambo ambayo hayaonekani
  kupewa nafasi hata kidogo na misingi
  ya utamaduni wa wazanzibari. Mambo hayo ambayo ni ya kawaida sana
  huko Tanzania bara bila shaka
  yanategemewa kuwa ya kawaida na
  Zanzibar pale itakapokuwa sheria
  zinazotawala Tanzania bara ndizo
  zitakazotawala Zanzibar wakati huo Zanzibar itakapokuwa mkoa wa
  Tanzania. Athari nyengine ipo katika
  ardhi ya Zanzibar ambayo ni mali ya
  wazanzibari. Itakapokuwa Zanzibar ni
  mkoa mmoja wa Tanzania sheria ya
  ardhi nayo itakuwa ni moja kwa Tanzania yote. Kwa sasa sheria ya
  ardhi ya Zanzibar haimruhusu mtu
  yeyote ambaye si mzanzibari kumiliki
  ardhi Zanzibar. Sheria ya ardhi
  itakaporuhusu kila matanzania
  kumiliki ardhi Zanziba matokeo yake ni ardhi hiyo ambayo ni ndogo
  kuvamiwa na mamilioni ya watanzania
  bara na hivyo kupelekea wazanzibari
  kusambaratika kwa kukosa maeneo
  ya kuishi wao pamoja na kizazi chao
  cha baadae. Matatizo ya muungano uliopo wa
  Tanganyika na Zanziba ni mengi.
  Athari kubwa zaidi imepatikana
  upande wa mahusiano ya kiuchumi
  kati ya Tanganyika na Zanzibar. Hapa
  itazungumziwa kero moja ya kiuchumi ambayo itatosha kuitathmini athari
  mbaya ya kero nyingi nyengine kwa
  wazanzibari. Kero hii ni ile ya
  kuingizwa kwa suala la mafuta na gesi
  asilia katika orodha ya mambo ya
  muungano. Kwa kuwa mafuta na gesi asilia ni miongoni mwa rasilimali za
  machimbo ya chini ya ardhi ni jambo la
  kushangaza kuona machimbo
  mengine kama vile madini ya
  dhahabu, chuma, Uranium na
  Tanzanite hayakuingizwa katika kifungu hicho cha orodha ya mambo
  ya muungano. Hili liko wazi kabisa
  kwani mafuta na gesi asilia tafiti
  zinathibisha kuwa yako kwa wingi
  mno katika ardhi na bahari ya visiwa
  vya Unguja na Pemba wakati machimbo mengine yako Tanganyika
  pekee. Sababu ya kufanyika hivyo ni
  kuipa uwezo Tanganyika kufaidi utajri
  mkubwa utokanao na mafuta ambao
  ni muhimili muhimu sana wa kiuchumi
  ulimwenguni. Kampuni ya utafutaji wa mafuta ya
  Canada iliingia Zanzibar kwa lengo la
  kufanya utafiti juu ya upatikanaji wa
  mafuta na gesi asilia kwa leseni ya
  Tanzania Petroleum Development
  Coorporatin (TPDC) bila hata ya ridhaa na ushauri achilia mbali ruhusa ya
  Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar
  katika mwaka wa 1997. Kiini cha
  tatizo hili bila shaka ni vile kutolewa
  kibali na TPDC kwa ajili kufanyika
  utafiti katika maeneo ambayo kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar si eneo
  la muungano. Mkataba rasmi
  ukafungwa baina ya kampuni hiyo,
  serikali ya Jamhuri ya muungano wa
  Tanzania na TPDC kuanzisha shughuli
  za utafiti. TPDC ni chombo cha wizara ya nishati na madini ya Jamhuri ya
  muungano wa Tanzania, wizara
  ambayo hufanya shughuli zake zote
  kwa upande wa Tanganyika pekee. Wizara ya nishati na madini na TPDC
  ndio vyombo vitakavyohusika na
  ukusanyaji wa mapato ya leseni
  ambazo makampuni ya uchimbaji
  yatakuwa yakikata leseni hizo.
  Hlkadhalika vyombo hivyo ndio vitakavyohusika na ukusanyaji wa
  mapato ya uhuishaji wa leseni kila
  mwaka. Kwa utaratibu huo basi
  Zanzibar isengeambulia chochote.
  Hapa Dr Salmin akahoji itakuwaje
  chombo hicho bila shaka cha Tanzania bara kitakuwa na mamlaka ndani ya
  mipaka ya eneo la Zanzibar kwa
  kisingizio kwamba mafuta na gesi
  asilia ni suala la muungano. Serikali ya
  mapinduzi ya Zanzibar haikuweza
  kulistahmilia hata kidogo suala hilo na hivyo kuamua kutokuiruhusu
  kampuni hiyo kufanya shughuli zake.
  Hapo ndipo wazanzibari walipoanza
  kuwa kitu kimoja katika kudai suala la
  mafuta na gesi asilia liondoshwe
  katika orodha ya mambo ya muungano. Kamati ya waziri mkuu na
  waziri kiongozi ya kujadili kero za
  muungano iliyoanzishwa na Raisi
  Kikwete katika kikao chake cha
  mwanzo ilianza rasmi kulijadili suala
  hili. Kampuni kubwa za kibiashara
  ambazo zina makao yake upande wa
  Zanzibar zinanyimwa ruhusa ya
  kupanua biashara zao upande wa
  Tanzania bara. Kampuni hizo
  zinalazimishwa kuhamisha makazi yake kutokea Zanzibar na kuyapeleka
  Tanzania bara na kulipa kodi kwa
  serikali ya Jamhuri ya muungano
  ndipo masharti ya kufanya kazi zao
  Tanzania bara yatakapokamilika.
  Halkadhalika kutokana na vikwazo mbali mbali, mazingira ya kibiashara
  ya ndani ya Zanzibar hayawavutii
  wafanyabiashara wakubwa wa
  kizanzibari kuwekeza nchini mwao.
  Wote wameamua kuhamishia mitaji
  yao na kuiweka Dar es Salaam. Ofisi za taasisi za muungano ambazo zipo
  Zanzibar zinaonekana kujazwa na
  wafanyakazi kutokea Tanzania bara
  zaidi kuliko Zanzibar na hivyo kutoa
  sura kuwa taasisi hizo ni za
  Tanganyika. Zanzibar kama nchi pia hainufaiki inavyostahili misaada
  inayotolewa na marafaki zake.
  Misaada yote huingia katika mkono
  wa Tanganyika kwa kivuli cha
  Jamhuri ya Muungano huku Zanzibar
  ikiambulia patupu. Mustakbali wa Muungano
  Maoni ya wananchi yaliwahi
  kukusanywa kuhusu kuendelea au
  kuvunjika kwa muungano kupitia
  tume ya Jaji Nyalali. Kwa kuwa hakuna
  chama hata kimoja cha siasa kilicho na msimamo wa kutaka kukoma kwa
  muungano wa Tanganyika na
  Zanzibar basi inaweza kusemwa
  kwamba maoni hayo yaliyokusanywa
  ni ya wananchi wenyewe. Kiwango
  cha juu zaidi cha maoni yaliopendekeza kuvunjika kwa
  muungano kwa mujibu wa utafiti
  uiofanywa na kamati hiyo ya Jaji
  Nyalali mwaka wa 1994 ni kutoka
  Pemba (15.6%) na kiwngo cha chini
  kabisa ni kutoka Unguja (1.6%). Hii bila shaka ni kwa kuwa wapemba
  wanauthamini sana sana uzalendo
  wao na wanajivunia sana heshima na
  hadhi ya nchi yao. Ndio maana asilimia
  kubwa ya maoni kuhusu kuvunjika
  kwa muungano usio na usawa na wenye kupendelea upande mmoja wa
  muungano huo yakatokea Pemba.
  Hata hivyo takwimu hizi zinaweza
  kuwa tofauti na hali ya sasa baada ya
  miaka 15 ya kukuwa kwa siasa za
  vyama vingi hapa nchini jambo lililosababishwa na kulegezwa makali
  kwa baadhi ya kero za muungano. Ni ukweli usiopingika kwamba
  maendeleo ya Zanzibar yamefifia sana
  ndani ya muungano huo
  ukilinganisha na upande wa pili wa
  muungano na hakuna dalili zozote
  zinazoashiria faraja. Kinachoonekana ni kama kwamba viongozi
  wanawalazimisha wananchi
  kuukubali muungano wa nchi zao
  wakati wananch wenyewe hususan
  wazanzibari wanaonekana wazi
  kwamba hwaoni umuhimu mkubwa wa muungano huo. Bila shaka hata
  mke mkifunga ndoa, na hata kama
  mumejaaliwa kizazi katika ndoa hiyo,
  ikiwa hamukubaliani katika maisha ya
  ndoa kwea kutawaliwa na kero zisizo
  kwisha, basi wazee wenye hekima huwashaurini watoto wao waachane
  kwa salama kama vile walivyooana
  kwa salama hapo mwanzo. Katika
  mazingira hayo basi sio jambo la
  kushangaza kuwaona Wazanzibari
  wanauchukia Muungano, kwani wanaamini ndio kiini cha matatizo
  mengi ya kijamii, kiuchumi na kisiasa
  kwa Zanzibar
   
 9. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Shukran nimekuelewa ambaye hataelewa hii akapewe pilau ale ..

  Sent from my HTC Incredible S using Tapatalk
   
Loading...