Siasa yaleta kilio kwa wakulima wa miwa bonde la Kilombero

Sijaelewa! Wachome kwa makusudi ili wavune kwa dhalura, tatizo lipo toka miaka ya 1980, serikali ichukue hatua afu siasa iingie
Inaonekana tatizo la msingi sio wakulima bali
ni KUCHELEWA KUVUNWA MIWA KWA WAKATI
Inamaana wananchi wanachoma ili kushinikiza kiwanda kivune.
Kwa maana hiyo, uongozi wa Serikali ungetumia busara kushuhulikia tatizo la msingi na sio hilo la kukataza miwa isivunwe. Hao wananchi wamesha kosea ni kuwasaidia wakati tatizo la msingi likitafutiwa uvumbuzi...
 
Nchi imeshakuwa ya ovyo hii , mambo mengi yanaenda ovyo ovyo hakuna mipango , sijui ni wapi hawa viongozi wetu wanatupeleka .
Inafika mahari mtu unakaa unafikiriiiaaa mbaka machozi yanakulenga ukifikiria juu ya mambo yanayoendelea ndani ya hii nchi .
Eehh !! Mwenyenzi mungu muumba wa mbingu na na ardhi naomba wapiganie wananchi wamikumi wapiganie watanzania wapate kile wanachoitaji futa wotee wanaoyumbisha haki na amani ndani ya taifa hili amen.
Halafu sukari ikiadimika wanaanza kupiga porojo za ajabu. Juzi nilipita pale Tunduma sukari ya Zambia, well packed kilo moja sh 2000...
 
Mimi nashindwa kuelewa - Jee serikali au taasisi yake yoyote walichangia chochote kulima miwa hiyo?

Kama ndivyo - Wana haki ya kuwa na kauli kuhusu uvunaji.

Kama sivyo, kuna uonevu mbaya hapo utakaochangia watu kukata tamaa ya kulima zao hilo.
 
Poleni sana wanakilombero serikali yetu ni sikivu tunalifanyia kazi suala lenu hivi punde mtapata majibu
 
Back
Top Bottom