Siasa yaleta kilio kwa wakulima wa miwa bonde la Kilombero

Tomahawk

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
218
250
Kwanza niseme wazi, mimi ni kijana na mmoja wa waathirika wa siasa kwenye uvunaji wa miwa msimu huu, bonde la mto kilombero.

Week moja imepita tangu ekari zaidi ya 2000 za wakulima wa nje wa miwa ziungue kwa dharula katika maeneo ya Matambiko, ilundo, msindazi na ruhembe na kusababisha hasara ya zaidi ya Tsh 3billions.

Kawaida miwa ikiungua kwa dharula kuna mkataba baina ya muwekezaji ambaye ni Illovo sugar group na wakulima wa nje, kuwa wakulima watavuna miwa yao ila watakatwa asilimia 5% ya pato lao na muwekezaji mara nyingi kutokana na kuwa na vifaa vya kisasa usaidia wakulima kuvuna miwa na miwa ufikishwa kiwandani na tatizo husika umalizwa ka aina iyo.

Cha ajabu? Miwa imeungua this time, anakuja mkuu wa wilaya anasema miwa isivunwe na atakayevuna na kujaribu kupeleka kiwandani akamatwe, anakuja tena mkuu wa mkoa anakazia umo umo kwa kauli ya mkuu wa wilaya.
Kumbuka: jimbo husika lenye uo mgogoro ni la mikumi ambalo mbunge wake ni Proffesor jay.

Watu tunahoji: iweje mkuu wa wilaya na mkoa (serikali) iingilie zoezi ili la uvunaji wakati wao hawausiki?

2) Iweje serikali ikatae kusaidia wananchi wake masikini kuvuna na kupeleka kiwandani ili hali muwekezaji yuko tayali kusaidia wakulima? ( mzungu yuko tayali kusaidia mtu mweusi, serikali, mtu mweusi anakataaa mtu mweusi mwenzake asisaidiwe????)

3) Serikali iko kwa manufaaa ya nani?

Hoja ya serikali: Ni kwamba wananchi wanajichomea makusudi, inawezekana mwananchi mmoja amechoma makusudi, sawa lakini mtoto wako mmoja akikojolea mboga nyumbani kwako, wewe baba utanyima chakula nyumba nzima?

Kwanini wakulima wanajichomea moto: wakulima wanajichomea moto kwakuwa kwenye vyama vya wakulima kuna rushwa mno ya kuchomewa ili uchomewe kwa wakati lazima utoe rushwa, sasa wengine masikini hawana rushwa kwa ghadhabu uchoma ili wavuniwe sasa madhara yake ekari nyingi zaidi ambazo hazikukusudiwa kuungua zinaunguwa. Na ili sio tatizo la leo ili tatizo la miwa kuungua limekuwepo since miaka ya 1980 na kiwanda kusaidiana na wakulima upambana kulitatua tatizo husika.

Rushwa: ni kweli kwenye vyama vya wakulima wa miwa wa nje kumekuwa na rushwa sana kikiongozwa na RCGA chini ya mwenyekiti wake Madenyeka. Iki chama kimekuwa kikilamikiwa mno na wakulima cha ajabu aya matatizo ya rushwa serikali inatambua fika na bwana ushirika wa wilaya na mkoa wanayafumbia macho, hatujui kwanini? ( mjiongoze)

Turudi kwenye ili la uvunaji wa dharula hii:

sisi wengine ni wasomi wa kiwango cha degree tumekosa kazi, tumewekeza kwenye kilimo icho matokeo yake leo napoteza zaidi ya million 20 tena kwa kusubiri kwa mwaka mzima.

Tafakuri: Kwanini serikali ikataze tusivune na tusivunie wakati wewe hawatumii hata chembe ya gharama yao?

Muwekezaji yuko tayali kutusaidi iweje serikali kupitia mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa wanakataaa tusivunie wana agenda gani binafsi hawa watu?

Hawa viongozi wana mchafulia mheshimiwa John pombe magufuli katika sera zake za kilimo na hapa kazi tu.
Wananchi wa kilombero TUMEKUFA.
 
Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
2,325
2,000
Amemkataza mzungu asivune/ nunue au amewakataza nyinyi wakulima msivune! Ingekuwa ni mikoa Fulani hio miwa ingevunwa ili hao wanaozuia waje wazuie.Watu wa morogoro mmwzidi sana upole.Hebu vuneni miwa hio kieleweke kwenye field Kwani hamba majambia ya kuvunia miwa.
Mjomba wangu aliwahu niamvia "Ukiona mtu anazuia riziki yako anadhamiria ufe hivyi unatakiwa umzue yeye".
 
EMG1

Member
Oct 7, 2020
72
150
Michango yetu halali NSSF/PSSSF hatupewi,Kahawa zetu tunapangiwa mnunuzi,korosho zetu ndio hivyo tena, pamba yetu nayo ni balaa ,sasa zamu ya miwa imeanza ,huku kwwnye mahindi ,mpunga ,maharage bei nayo siyo rafiki duh! October 28 siyo ya kukosea
 
Shambaboy jogoli

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
1,080
2,000
Kwanza niseme wazi, mimi ni kijana na mmoja wa waathirika wa siasa kwenye uvunaji wa miwa msimu huu, bonde la mto kilombero.

Week moja imepita tangu ekari zaidi ya 2000 za wakulima wa nje wa miwa ziungue kwa dharula katika maeneo ya Matambiko, ilundo, msindazi na ruhembe na kusababisha hasara ya zaidi ya Tsh 3billions.

Kawaida miwa ikiungua kwa dharula kuna mkataba baina ya muwekezaji ambaye ni Illovo sugar group na wakulima wa nje, kuwa wakulima watavuna miwa yao ila watakatwa asilimia 5% ya pato lao na muwekezaji mara nyingi kutokana na kuwa na vifaa vya kisasa usaidia wakulima kuvuna miwa na miwa ufikishwa kiwandani na tatizo husika umalizwa ka aina iyo.

Cha ajabu? Miwa imeungua this time, anakuja mkuu wa wilaya anasema miwa isivunwe na atakayevuna na kujaribu kupeleka kiwandani akamatwe, anakuja tena mkuu wa mkoa anakazia umo umo kwa kauli ya mkuu wa wilaya.
Kumbuka: jimbo husika lenye uo mgogoro ni la mikumi ambalo mbunge wake ni Proffesor jay.

Watu tunahoji: iweje mkuu wa wilaya na mkoa (serikali) iingilie zoezi ili la uvunaji wakati wao hawausiki?

2) Iweje serikali ikatae kusaidia wananchi wake masikini kuvuna na kupeleka kiwandani ili hali muwekezaji yuko tayali kusaidia wakulima? ( mzungu yuko tayali kusaidia mtu mweusi, serikali, mtu mweusi anakataaa mtu mweusi mwenzake asisaidiwe????)

3) Serikali iko kwa manufaaa ya nani?

Hoja ya serikali: Ni kwamba wananchi wanajichomea makusudi, inawezekana mwananchi mmoja amechoma makusudi, sawa lakini mtoto wako mmoja akikojolea mboga nyumbani kwako, wewe baba utanyima chakula nyumba nzima?

Kwanini wakulima wanajichomea moto: wakulima wanajichomea moto kwakuwa kwenye vyama vya wakulima kuna rushwa mno ya kuchomewa ili uchomewe kwa wakati lazima utoe rushwa, sasa wengine masikini hawana rushwa kwa ghadhabu uchoma ili wavuniwe sasa madhara yake ekari nyingi zaidi ambazo hazikukusudiwa kuungua zinaunguwa. Na ili sio tatizo la leo ili tatizo la miwa kuungua limekuwepo since miaka ya 1980 na kiwanda kusaidiana na wakulima upambana kulitatua tatizo husika.

Rushwa: ni kweli kwenye vyama vya wakulima wa miwa wa nje kumekuwa na rushwa sana kikiongozwa na RCGA chini ya mwenyekiti wake Madenyeka. Iki chama kimekuwa kikilamikiwa mno na wakulima cha ajabu aya matatizo ya rushwa serikali inatambua fika na bwana ushirika wa wilaya na mkoa wanayafumbia macho, hatujui kwanini? ( mjiongoze)

Turudi kwenye ili la uvunaji wa dharula hii:

sisi wengine ni wasomi wa kiwango cha degree tumekosa kazi, tumewekeza kwenye kilimo icho matokeo yake leo napoteza zaidi ya million 20 tena kwa kusubiri kwa mwaka mzima.

Tafakuri: Kwanini serikali ikataze tusivune na tusivunie wakati wewe hawatumii hata chembe ya gharama yao?

Muwekezaji yuko tayali kutusaidi iweje serikali kupitia mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa wanakataaa tusivunie wana agenda gani binafsi hawa watu?

Hawa viongozi wana mchafulia mheshimiwa John pombe magufuli katika sera zake za kilimo na hapa kazi tu.
Wananchi wa kilombero TUMEKUFA.
Sijaelewa! Wachome kwa makusudi ili wavune kwa dhalura, tatizo lipo toka miaka ya 1980, serikali ichukue hatua afu siasa iingie
 
tozi25

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
6,039
2,000
Wananchi wapo 1.5 million Mkuu wa Wilaya 1, Mkuu wa Mkoa 1 polisi + jeshi 1 million hawafiki lakini tunawaogopa hatariii. Ifike muda umafia ufanyike kwa wazuia maendeleo

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
darubin ya mbao

JF-Expert Member
Aug 3, 2016
1,508
2,000
Fanyeni Kama alivyofanya mkukima Mwandindi kule Iringa. Piga Mkuu wa Mkoa na ua. Yeye pia kwa kuzuia kuvuna miwa yenu ameshawaua kiuchumi. Nanyi mfanyizieni. Hana maana.
Naunga mkono hoja, kuna haja raia tuanze kumiliki bunduki Bila longo longo ili tuwe tunaheshimiana

Miwa imeshaungua, kiwanda kipo tayari kuvuna anatokea RC na DC wanazuia watu wasivune aisee Watanzania tunaonewa sana.
 
Mmea Jr

JF-Expert Member
May 20, 2016
311
500
Nchi imeshakuwa ya ovyo hii , mambo mengi yanaenda ovyo ovyo hakuna mipango , sijui ni wapi hawa viongozi wetu wanatupeleka .
Inafika mahari mtu unakaa unafikiriiiaaa mbaka machozi yanakulenga ukifikiria juu ya mambo yanayoendelea ndani ya hii nchi .
Eehh !! Mwenyenzi mungu muumba wa mbingu na na ardhi naomba wapiganie wananchi wamikumi wapiganie watanzania wapate kile wanachoitaji futa wotee wanaoyumbisha haki na amani ndani ya taifa hili amen.
 
konyola

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
2,133
2,000
Ningekuwa huko ningeingia shamba na sebo sasa nione pumbav lolote lije linikoromee ni mwendo wa kumwaga mtu uhalo haijalishi ni Nani ni mwendo wa kumdidimiza sime kwenye antlog kama siyo log inverse ya mouth
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom