mirindimo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2009
- 892
- 1,709
Tukiwa tunashangalia kufutwa kwa service charge kwa shirika la umeme Tanzania imefahamika kuwa shirika hilo sasa linavujia damu ndani kwa ndani huku likiponzwa kiutendaji kwa kuingiliwa kisiasa.
Siku mbili hizi umeme umekua ukikatika kwa baadhi ya maeneo ya jiji bila taarifa rasmi lakini ukweli ni kwamba mitambo ya kuzalisha umeme ya Songas ilizimwa na kusababisha uzalishaji umeme kupungua kufuatia deni kubwa inalodaiwa TANESCO.Baada ya serikali kuona hivyo vikao vikali vya ndani kwa ndani vilianza huku Songas wakipewa shinikizo kutoka juu kuwasha mitambo hiyo ili vikao vya makubaliano namna watakavyolipwa viendelee.
Baada ya mvutano mkali Songas walilegeza uzi na kuwasha mitambo hiyo na hata hivyo mda ulikua umekwenda na kikao kuahirishwa mpaka siku kitakapotajwa.Taarifa za ndani kutoka EWURA zinasema hawakuikubalia Tanesco kushusha bei ama kufuta service charge kwani shirika hilo halitaweza kujiendesha kutokana na kudaiwa madeni makubwa.Taasisi hiyo ilipokea shinikizo kutoka juu na kusababisha kuforce mambo ili itangazwe kua Tanesco imefuta service charge na itamudu gharama za kujiendesha.
Wakati huo huo taarifa za ndani za Tanesco zinasema kua haikua tayari kufuta/kupunguza gharama hizo kutokana na ukweli kua ina madeni mengi na makubwa na yanazidi kukua,siasa iliingilia kati na ikatolewa amri kua gharama hizo ziondelewe haraka iwezekanavyo na watendaji waangalie namna ya shirika hilo kujiendesha la hawana kazi.Umeme utaendelea kukatika kadri Songas na serikali watakavyokua wanatofautiana katika terms za kulipana ama mpaka hapo serikali itakapoliwezesha shirika hili kusimama na kujiendesha.
Maagizo kama haya ya kisiasa yameendelea kuyakumba mashirika kadhaa ya umma na mamlaka zingine za serikali kama mamlaka ya mapato Tanzania.Je unafikiri huduma kama hizi za kijamii zikiendeshwa kisiasa wakati huo huo kiuhalisia haiwezekani ni sahihi ???