Siasa ya nchi yetu ni ipi?

Mzee wa Jando

Member
Feb 7, 2019
7
5
Siasa ya TANU ni Ujamaa ambayo ilijenga imani ya wana TANU. Naamini CCM nayo iliamua kuitumia na kuisimamia hadi sasa.

Baba wa Taifa alitangaza siasa ya KUJITEGEMEA kuwa ya taifa (rejea Azimio la Arusha 1967).

Enzi za Chama kushika hatamu tukaunganisha siasa ya taifa letu kuwa SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA. Tafsiri fupi ya Siasa yetu hiyo ilikuwa Kuamini binadamu wote ni sawa na kila mwenye uwezo afanye kazi kwa bidii ili kukidhi mahitaji yake, ya jamii na taifa letu ili kujimudu bila kuhitaji msaada toka kwa mabeberu!

Leo siasa yetu ni ipi? Msajili wa vyama vya siasa anasimamia siaaa ipi? Ili kila kikundi kinachohitaji kusajili chama cha siasa kiambiwe na Msajili kwamba lazima kisimamie siasa yetu.

Siasa ambayo haitakuwa ya kikundi chochote bali ya taifa letu. Iwe CCM, CUF, CHADEMA, ACT- Wazalendo nk zitalazimika kuisimamia siasa ya taifa letu
 
Mkuu. Swali ulilouliza na hasa ukilihusisha na majukumu ya Msajili wa Vyama ni sahihi kabisa. Hizi “Hapa kazi tu”, “Haki Sawa kwa Wote” na kadhali ni sera tu na sio mrengo!! Ni vema tukaambiwa sasa kama siasa zetu ni za kijamaa au kibepari.

Nimeuliza swali hili siku nyingi katika kuchangia nyuzi zenye mada tofauti, leo nitapata kusikia majibu nadhani.
 
Katiba yetu mpaka sasa (Ibara ya 9) inatamka wazi kuwa tunafuata siasa ya ujamaa na kujitegemea. Ila kila rais aliyepata kututawala ame-define alivyoweza huo ujamaa na kujitegemea. Hata huyu wa sasa haelekei kutuelewesha huo ujamaa unafananaje.
 
Back
Top Bottom