Siasa ya Mwalimu ilivyowaathiri Waislamu Tanganyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa ya Mwalimu ilivyowaathiri Waislamu Tanganyika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mstahiki, Dec 27, 2010.

 1. m

  mstahiki JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2010
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Sijui kwanini lakini awamu hii udini umezungumziwa sana kuliko awamu yeyote iliyopita.
   
 3. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Huenda ikatokana na mporomoko wa miiko katika uongozi, ya kwamba muingiliano kimadaraka na kukosa MKEMEAJI wa dhati ndio chanzo.
  Azimio la Arusha lilitustahili saaana sisi Watanganyika kwa leo yetu. Nchi haina mkemeaji na akasikilizwa, wote ni wajuzi & wababe.
   
 4. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mjomba anaishiwa sera na nchi inazidi kudidimia....hapa ndio anatafuta gia ya kutokea, tatizo ni kwamba itatugharimu vibaya sana!
   
 5. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  usishangae.kila anapokuwepo rais muislamu kadhia hii ya udini hupamba moto,rejea kipindi cha mwinyi mabucha ya kitimoto yalichomwa moto.
  Tatizo la nchi hii hatuna wanasiasa wenye idealogy fulani kwa mfano J.k.Nyerere aliamini katika siasa za kijamaa na alitumia mbinu zote kuhakikisha analitetea hilo.
  Tanzania ya leo haijitambui kama ni ya kibepari,kisoshalizimu au kijamaa kama katiba inavyosema.the leaders have no vision!!yaani mtu anaibuka na kutaka kuwa kiongozi basi,baada ya hapo hajui nini cha kufanya kwa sababu hakujiandaa kifikra na kimkakati.kwa ukweli huu hatuwezi kuwa na mawazo mengine zaidi ya UDINI,MAJUNGU,VIJEMBE na NGONO kwa sana.
  "Hatufiki mpaka tuchapane" those who will be fit to survive wataheshimiana.
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Dec 27, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,610
  Likes Received: 3,913
  Trophy Points: 280
  hamna udini Tanzania watu wanapoteza muda kujadili kitu ambacho hakipo!! wakristo na waislamu wenye ku-mind udini mwisho wao ni aibu!!! watanzania hawa ninaowafahamu hawana huo udini!
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kama Mwalimu Nyerere angekuwa mdini asingethubutu kufanya yafuatayo:

  1. Kuunganisha Zanzibar ya Waislamu wengi na Tanganyika kuwa nchi moja ya Tanzania. Kitendo cha kuunganisha nchi hizi mbili kiliongeza namba ya waislamu katika utawala wa mwalimu. kama angekuwa ni mdini angependa kupunguza idadi ya waislamu nchini na katika utawala wake badala ya kuwaongeza.


  2. Nyerere ndiye Rais pekee Afrika aliyethubutu kuvunja Ubalozi wa Israel hapa nchini na kuwafukuza kutokana na kuitambua Palestina kama taifa huru. Palestina ni taifa la Kiislamu.

  3. Mwalimu, alianzisha siasa ya ujamaa iliyokuwa na mlengo wa ukomunisti wa iliyokuwa Urusi taifa ambalo lilikuwa linakataa kuwepo kwa Mungu na kujitenga mbali na Marekani ambao walikuwa mabepari na wananchi wake wengi wafuasi wa dini ya kikristo. kama mwalimu angekuwa mdini angefuata siasa za MAREKANI kuliko za Urusi.

  4. Nyerere alihusika sana katika ukombozi wa nchi za Afrika bila kujali kwamba ndani ya nchi hizo alikuwa pia anawakomboa Waislamu ambao sio wa dini yake. Hii inaonyesha kwamba mwalimu alikuwa anajali zaidi utu wa binadamu kuliko matakwa ya dini.

  5. Nyerere alitaifisha shule za dini nyingi zikiwa ni pamoja na za wakristo na kuzifanya za wote.

  6. Wakati Nyerere anaondoka madarakani nchi aliikabidhi kwa Ally hassan Mwinyi ambaye ni mwislamu. kama mwalimu angekuwa mdini kwa nafasi yake angeweza kumpigia debe mkristo mwenzake ili kupunguza nguvu ya Waislamu kujijenga kuwa imara zaidi.

  7. Msikiti wa kisasa wa butiama ulijengwa kwa msaada wa Rais Gadaff wa Libya baada ya mwalimu kumuamba msaada. Ombi hilo lilifuatia tabu waliokuwa wanapata waislamu baada ya kukosa mahala pa kuabudu. Msikiti huu umejengwa kwenye himaya ya asili ya mwalimu nyerere, kama angekuwa na chuki na waislamu asingethubutu kuwaeneza katika himaya ya butiama.

  8. Nyerere aliwapa Waislamu uwanja mkubwa pale chang'ombe, Dar es salaam kwa ajili ya kuanzisha chuo kikuu cha waislamu. Kiwanja hiki kimeuzwa na BAKWATA. Ni nani alikuwa anawapenda Waislamu katika suala hili la kiwanja, Nyerere au BAKWATA?

  9. Mfanyakazi wa ndani/Mpishi mkuu wa chakula cha mwalimu kwa miaka karibu yote alikuwa mwislamu na baadhi ya wapishi wake walikuwa ni pamoja na waislamu kwa wakristo. Hii inaonyesha kuwa mwalimu alimuamini mwislamu kuandaa chakula chake.

  10. Katika watoto yatima aliochukua kuwalea mwalimu nyumbani kwake ni pamoja na Waislamu ambao waliendelea na dini zao wakienda msikitini bila kuwazuia kufuata imani yao hadi leo.

  Kwa kifupi, sayansi inakataa kumuonyesha mwalimu kuwa alikuwa mdini ingawa kama binadamu hawezi kukosa kasoro za utawala wake kama itakavyokuwa kwa Rais yeyote ama mkristo, mwislamu, mpagani au dini yoyote. Kama tungekuwa na maabara ya kisayansi ili kuthibitisha kama Nyerere alikuwa mdini basi kuna mambo ambayo Nyerere aliyafanya hayaonyeshi kama alikuwa mdini au mtu ambaye ni mdini angefanya kwa watu wa dini nyingine.
   
 8. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  JK ndiye mtu wa kulaumiwa kwa kupandikiza hoja ya udini wakati wa kampeni na kisha kuanza kuinyweshea maji mbegu yake hii.Kama kuna kitu JK atakumbukwa katika nchi hii ni kuasisi siasa za udini, kusema kweli jambo hili ni la kufikirika zaidi lakini kwa jinsi juhudi zinazofanywa na genge la JK hii nchi itakuja lipuka tu .
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Dec 27, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,610
  Likes Received: 3,913
  Trophy Points: 280
  alitaifisha shule za seminari na kuwa za serikali

  Tatizo la Nyerere ni kutaka sana ukubwa na kuabudiwa na hili kweli kabisa alilifanikisha,pamoja na kuwa athari zake ni hali ya sasa ya kisiasa lakini uzuri wake ni kuwa waliwacontrol waislamu ambao huwa inafika wakati huwa hawatumii akili zao za kuzaliwa bali emotion na uongo ulioandikwa kwenye vitabu vya kidini!

  sipati picha kama rais wa kwanza nchi hii angekuwa mwislamu, mimi mkristo ningekuwa wapi sijui. NYERERE HAKUWA MDINI YET UWEPO WAKE PALE TU UMEWAFAVOUR SANA WAKRISTO
   
 10. N

  Nancy Tweed Senior Member

  #10
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kwasababu tuu ukweli unaweza kufichwa kwa muda, lakini huwezi kuuficha milele.
   
 11. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mimi sioni sababu ya kupaniki na udini huu ambao ilikuwa ni janja ya jamaa tu. CCM ndiyo itakayoamua nchi hii kuwa na udini au la? Udini umetumika tu kwenye uchaguzi wa mwaka huu kwa sababu jamaa aliona mambo yalikuwa yanenda kombo.Tumeuona uswahiba wa CCM na CUF ndiyo uliofanikisha jambo hili, kwa mwaka huu, CUF wakidhani watapata kitu huku bara. Mimi sijui labda mahakama ya kadhi ambayo hatahivyo hii si ngoma ya mchiriku ambayo Jk anaweza kuicheza kama ananawaaaaaaa, ngoma hii hakuna anayeweza kuicheza labda asiyekuwa na akili. Piga ua galagaza ndoa ya CCM na CUF huku bara haiwezi kuwepo baada 2015 na ndiyo itakuwa mwisho wa agenda ya udini. Agenda hii yaweza kurudi tu ikiwa atateuliwa kugombea jamaa mwenye mtazamo sawa na wa huyu jamaa. Lakini nachelea kusema haitatokea tena maana wamejifunza. Tusubiri kama mtaiona agenda hii tena 2015 maana haitakuwa dili tena maana wanauangalia upepo na wameshajua unakoelekea, japo hawataweza kuufuata kwa hiari yao bali utawakumbakumba hata kama hawataki. Itabidi wachukuliwe na upepo huu na pengine wataondoka bila kubeba kitu chochote wakaishi maisha mapya yasiyo na kitu kama wengi wetu tunavyoishi hii leo. Tusubiri tuone!

  Mungu ibariki Tanzania, Mungu tupiganie Watanzania wanyonge tunaonyonywa na watawala!
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Dec 27, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nina bahati ya kuwa katikati ya Waislamu, kwa maana kwamba nimejenga nyumba kwa kuzungukwa na jamii ya waislamu. Hawa ni ndugu zangu hata kuliko wakristo wenzangu. kuna jambo la kushangaza la heri kubwa sana kwa nchi yetu limenitokea xmas hii. Mbali na kupata zawadi nyingi za xmas kutoka kwa waislamu hawa lakini wengine walinitembelea nyumbani kunipa mkono wa heri kama wafanyavyo miaka yote.

  Mmoja wa waislamu hao akajitolea kwamba, safari hii Kristimas kitafanyika kinyumenyume nyumbani kwake hivyo sisi wakristo tusiandae chochote. Pamoja na majirani wengine na familia yangu yote tulikwenda katika boma la waislamu kula xmas.

  Nimejifunza jambo hapa kwamba, Udini haupo Tanzania bali kuna watu wanaukuza kwa maslahi yao.
   
 13. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2010
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Mbu sugu, KULA TANO!

  Ila kubali kuwa kuna waTZ wachache wenye hisia za kidini, na hawa ndio wanajaribu kuzikuza. Imefikia kiasi kuwa unaweza ukawa mathalani, unai-criticise TANESCO kwa mgao wa umeme. Ukitaja tu jina la mtu ndani ya TANESCO basi watu fulani watasema unamsema kwasababu ni wa dini yao. Surely, kuna watu wachache wenye mitazamo ya namna hii, mitizamo ambayo ni unhealthy to our Nation.
   
 14. l

  limited JF-Expert Member

  #14
  Dec 27, 2010
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ni kweli hii hoja ya udini inaletwa tu kutaka kuvuruga watanzania huku viongozi wakiendelea kuboronga na kuiba mali za watanzania it is not right !!!!
   
Loading...