Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 6,293
- 8,204
Petroli ni moja ya mafuta ambayo huagizwa kutoka katika mataifa ya nje kwa ajili ya kutumiwa katika magari madogo na ya kati.
Mafuta ya petroli ambayo yanaigizwa kutoka mataifa ya nje yanachukua karibia robo (1/4) ya bidhaa za mafuta ambayo huagizwa kutoka mataifa ya nje kama ilivyo ripotiwa na EWURA mwaka 2014.
Sasa kwakuwa mafuta ya Petroli ya gredi ya juu kabisa yanaweza kuzalishwa kwa kutumia gesi asilia. Mradi huu unaweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambazo zinatumika kuagiza mafuta kutoka mataifa ya nje kila mwaka.
Kama tukijenga kiwanda chenye uwezo wa 0.23MTPA kinaweza kutoka mapipa 6350 ya Petroli kwa siku (6350bpd).
Mapipa hayo yataweza kupunguza asilimia 27 za Petroli na 36 za gesi ya LPG ambazo huwa tunaziagiza kutoka katika mataifa ya nje.
Hapa chini ni prosesi nzima inayo onyesha hatua zaa kuibadirisha gesi asilia kuwa petroli (gasoline).
Kwenye gesi asilia kuna kampaundi yenye kabon atom moja (C1) ambayo ni methane kwa jina la kitaalamu hivyo tutafanya miungano ya kikemikali ili kutengeneza kampaundi zenye kaboni atom kuanzia tano (C5) hadi kaboni atom kumi na mbili (C12) ambayo ndio petroli yenyewe.
Pia wakati wa kufanya miungano tutapata na kampaundi zingine zenye kaboni tatu (C3) na kaboni nne (4) ambayo ndio LPG yenyewe hiyo gesi inayouzwa kwa kina Mihani, Oryx, Lake Gas n.k.
Ukitaka kujua zaidi unaweza kunitafuta nitakuelewesha vizuri na kukuelewesha zaidi.