Siasa ya Mafuta na Gesi: Kuibadili gesi asilia kuwa mafuta ya petroli inaweza punguza gharama tunazotumia kuagiza mafuta hayo kutoka mataifa ya nje

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
1,486
2,000
Petroli ni moja ya mafuta ambayo huagizwa kutoka katika mataifa ya nje kwa ajili ya kutumiwa katika magari madogo na ya kati.

Mafuta ya petroli ambayo yanaigizwa kutoka mataifa ya nje yanachukua karibia robo (1/4) ya bidhaa za mafuta ambayo huagizwa kutoka mataifa ya nje kama ilivyo ripotiwa na EWURA mwaka 2014.

Sasa kwakuwa mafuta ya Petroli ya gredi ya juu kabisa yanaweza kuzalishwa kwa kutumia gesi asilia. Mradi huu unaweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambazo zinatumika kuagiza mafuta kutoka mataifa ya nje kila mwaka.

Kama tukijenga kiwanda chenye uwezo wa 0.23MTPA kinaweza kutoka mapipa 6350 ya Petroli kwa siku (6350bpd).

Mapipa hayo yataweza kupunguza asilimia 27 za Petroli na 36 za gesi ya LPG ambazo huwa tunaziagiza kutoka katika mataifa ya nje.

Hapa chini ni prosesi nzima inayo onyesha hatua zaa kuibadirisha gesi asilia kuwa petroli (gasoline).

Kwenye gesi asilia kuna kampaundi yenye kabon atom moja (C1) ambayo ni methane kwa jina la kitaalamu hivyo tutafanya miungano ya kikemikali ili kutengeneza kampaundi zenye kaboni atom kuanzia tano (C5) hadi kaboni atom kumi na mbili (C12) ambayo ndio petroli yenyewe.

Pia wakati wa kufanya miungano tutapata na kampaundi zingine zenye kaboni tatu (C3) na kaboni nne (4) ambayo ndio LPG yenyewe hiyo gesi inayouzwa kwa kina Mihani, Oryx, Lake Gas n.k.

Ukitaka kujua zaidi unaweza kunitafuta nitakuelewesha vizuri na kukuelewesha zaidi.

IMG_20210510_182016.jpg
 

andoza

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
2,265
2,000
Tuna wataalamu wa Mafuta na Gas wazuri sana tatizo siasa mingi.If the project is viable and profitable look for investors.Otherwise
 

Kikiwo

JF-Expert Member
Nov 30, 2017
1,776
2,000
Mku ni wazo zuri umebeba maono katika nyanja ya mambo ya mafuta. Sasa ungetusaidia na kwaupande wa costing. Nachojua ni kwamba hizo process zote GAS inakopitia mpaka stage ya mwisho igeuke mafuta ya Petrol lazima kuna gharama .

Tusaidie tuzijue hizo cost kwa kila Lita moja ya Petroli ili tulinganishe na bei ya Petroli kwa sasa tuone kama inalipa au itakuwa very expensive.
 

Chipukizi

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
2,978
2,000
Hiki kiwanda kinazalisha pipa laki 6 kwa siku ubia kati ya Msouz Africa Sasol na Serikali ya Qatar walikijenga kwa dola millioni 600.
 

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
1,486
2,000
Mku ni wazo zuri umebeba maono katika nyanja ya mambo ya mafuta. Sasa ungetusaidia na kwaupande wa costing. Nachojua ni kwamba hizo process zote GAS inakopitia mpaka stage ya mwisho igeuke mafuta ya Petrol lazima kuna gharama...
Ninazo cost za process nzima nitaanda uzi mwingine tena ambao utaelezea cost zote alafu nitalinganisha na gharama tunazotumia kuagiza.
 

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
1,486
2,000
Hiki kiwanda kinazalisha pipa laki 6 kwa siku ubia kati ya Msouz Africa Sasol na Serikali ya Qatar walikijenga kwa dola millioni 600.
Hii kampuni naijua wako vizuri sana
 

taylor9119

JF-Expert Member
Nov 4, 2012
278
500
HAPANA.. Tunapozungumzia SUSTAINABLE DEVELOPMENT huwezi wekeza Kwenye reversal reactions za Gas to Petroleum(liquid) while those resources are limited, non renewables and environmental pollutants.

Kwa akili hizi za kumeza tu madesa hatuwezi produce kina ELON MUSK..Dunia ishabadilika magari yanaweza kua powered hata Na wind/Solar pia bado ya umeme, megawatts 2115 zinakuja be excited.
 

Kiduila

Senior Member
Jun 22, 2017
158
250
Kwenye hilo mimi nina swali, kwanini tuingie gharama kubwa ya kubadilisha gas kuwa petrol ilhali gas yenyewe hutumika kwenye mashine moja kwa moja?

Mfano kwa sasa hapa nchini kuna magari kadhaa yanayotumia nishati hiyo. Mtoa mada unaonekana ni mtaalam wa mambo haya, naomba ufafanuzi tafadhali.
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
41,563
2,000
Gari zijazo ni za umeme! Mi naona tungeanzidha assembly plant ya magari ya umeme nafikiri yako cheap kutengeneza kuliko yale ya combustion engine! Motor haina mbwembwe nyingi kama ma piston
 

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
1,486
2,000
Kwenye hilo mimi nina swali, kwanini tuingie gharama kubwa ya kubadilisha gas kuwa petrol ilhali gas yenyewe hutumika kwenye mashine moja kwa moja?, Mfano kwa sasa hapa nchini kuna magari kadhaa yanayotumia nishati hiyo. Mtoa mada unaonekana ni mtaalam wa mambo haya, naomba ufafanuzi tafadhali.
Gesi asilia inaweza kutumika kwenye magari moja kwa moja katika mfumo wa gesi iliyo shindiliwa au compressed natural gas (CNG).

Ili gesi hii iweze kutumika kwenye magari ya watanzia wote tunahitaji vitu viwili muhimu katika nchi yetu

1. Magari yetu inabidi yaboreshwe kwenye mfumo wa injini ili yaweze kutumia hiyo gesi. Hapo sasa kuna gharama za kubadirisha gari ili liweze kutumia gesi. Hapa kwenye kubadirisha sasa tunahitaji tujenge vituo vya kuboresha hizo injini ili zitumie gesi.

2. Tunatakiwa tujenge vituo vipya vya kushindilia gesi kwenye mitungi itakayobeba hiyo gesi kwenye hayo magari (CNG filling stations). Tunatakiwa tujenge vituo hivyo kila wilaya Tanzania nzima. Kujenga tu vituo itatuchukua muda mrefu sana. Na tunaweza kuingia hasara kama biashara haitokwenda vizuri.

Lakini kama tukiibadili gesi kuwa petroli hatutohitaji kuboresha injini za magari yetu. Pia hatutohitaji kujenga vitu vipya vya kujaza hayo mafuta maana tunavyo tayari vituo Tanzania nzima.

Na pia sio rahisi kukosa wateja wa petroli Tanzania. Kwasababu magari mengi yanatumia petroli. Hivyo ni biashara ambayo itarudisha faida mapema.
 

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
1,486
2,000
Gari zijazo ni za umeme! Mi naona tungeanzidha assembly plant ya magari ya umeme nafikiri yako cheap kutengeneza kuliko yale ya combustion engine! Motor haina mbwembwe nyingi kama ma piston
Tatizo la gari zinazotumia umeme ni energy storage. Mpaka sasa element iliyogunduliwa Kustore energy kwenye battery ni lithium, lakini inauwezo wa kustore energy kidogo sana ukilinganisha na mafuta.

Pack moja ya lithium-ion battery ina energy storage density ya 0.3 MJ kwa kila kg moja na energy density ya 0.4 MJ kwa kila lita moja.

Wakati petroli ina energy storage density mara 100 ya energy storage ya lithium-ion battery.

Kwa uwiano wa 5, a battery yenye energy storage density 1/5 ya hiyo petroli ndio itakua sawa na gari ambalo linaendeshwa kwa petroli.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom