Siasa vs education; elimu ya juu tutafika? tazama hapa na kwa wenzetu ulaya

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,776
2,000
1. UDSM
-Jakaya Mrisho Kikwete (66 yrs)
-Raisi mtaafu wa Tanzania
-Kateuliwa na Raisi Magufuli

2. UDOM
-Benjamin William Mkapa (78 yrs)
-Raisi mstaafu wa Tanzania
-Aliteuliwa na Kikwete

3. MUHIMBILI
-Ali Hassan Mwinyi (91 yrs)
-Raisi mstaafu wa Zanzibar

4. State University of Zanzibar
-Dr Ali M. Shein (68 yrs)
-Raisi wa Zanzibar

5. SUA
-Joseph Warioba (76 yrs)
-Makamu wa Rais mstaafu na Waziri mkuu mstaafu

6. Nelson Mandela
-Dr. G. Bilal (71 yrs)
-Makamu wa Raisi mstaafu

7. CHUO KIKUU HURIA (OUT)
-Mizengo Pinda (68 yrs)
-Waziri Mkuu mstaafu

8. Hubert Kairuki
-Dr. Salim Ahmed Salim (74 yrs)
-Waziri Mkuu mstaafu na
-Secretary General mstaafu wa ilyokuwa OAU na baadae AU

9. Ardhi University
-Cleopa Msuya (85 yrs)
-Waziri Mkuu mstaafu

10. Mzumbe University
-Barnabas Samatta (76 yrs)
-Jaji Mkuu mstaafu

11. MUST
-Prof Mark Mwandosya (67 yrs)
-Waziri Mstaafu

Ama kwel aliyenacho ataongezewa na asie nacho akajiajiri !!!!!

A] Katka hii list Kikwete ndo mdogo kiumri
Hivi hii nafasi inaangalia umri, hata kama, Je hakuna watu wenye cv zilizotukuka wenye 50 to 60 au 65 yrs hivi
Hii nafas ina uzito kias gan mbona kuna wakuu wa nchi wenye umri chini ya miaka 50
1. John Kennedy (USA)
-alkuwa raisi akiwa 43 yrs
2. Atifete Jahjaga (KOSOVO)
-She was 36 yrs
3. Kabila (Congo)
- was 29yrs, now 45
4. Barack Obama USA
-was 47yrs, now 55
5. Andrzej Duda (POLAND)
-was 44yrs, now 45

Uraisi ni taasisi kubwa zaid ya ukuu wa chuo, so sidhan kama umri mkubwa kias hcho ndo kigezo

B] Nikadhan pia labda inabd uwe public figure au uwe na political experience
Sasa ngoja tuone hali ipoje kwa vyuo vitambulikavyo kidunia Chancellors wao :
1. HARVARD UNIVERSITY
- Drew Gilpin Faust
-Professor of History in Harvard's Faculty of Arts and Science

2. MASSACHUSETTS
-Kumble R. Subbaswamy
-Professor, Department of Physics and Astronomy

3. STANFORD UNIVERSITY
-Marc tessier Lavigne
-alkuwa chancellor wa Rockefeller university na
-Head of the Laboratory of Brain Development and Repair

Kazi kwel kwel, wateuzi na wateuliwa ni wale wale, duuu

Aliye na mtaji anateuliwa na asie na mtaji anaambiwa ajiari
Sio kwamba vijana wa 20s ndo wateuliwa la hasha, lakin akiteuliwa wa 50s, wa 40s atapanda kuziba nafasi na 30s atapanda hali kadhalika 20s atapata nafasi huku chini

Wastaafu wana nafas kubwa sana ya kuwashaur viongoz wa juu, wana access, tena hata kwa kumpigia simu tofaut na raia wengine KWANN WASIBAK KAMA WASHAUR TU, na wapate mda wa kuwa na familia zao baada ya majukumu mazito ya kulitumikia taifa hili kama alvosema Mzee Kikwete wakat anaaga ile mwaka jana???

Chancellor ni ceremonial leader, labda kuna vigezo vya kuteuliwa,
wana jamvi tusaidiane tafadhal
NB:
marekebisho yanaruhusiwa
ASANTENI NA KARIBUNI

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 

Batale

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
1,113
2,000
Hilo nalo neno.... naamini hao wana ukwasi hivo badala ya kuwapa majukumu mengine baada ya kustaafu, tuwaache wawekeze ili vijana wa Kitanzania wapate ajira.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom