FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,026
- 122,647
Nilijibu uzi fulani humu JF kwa haya:
Ni mengi sana yanaongelewa lakini ni wachache sana wenye uelewa wa mambo ya uchumi mkubwa na teknolojia za kuzalisha uchumi mkubwa yanavyoendeshwa na hao wenye teknolojia hiyo, ambao ndiyo hao hao wenye uchumi mkubwa.
Kama hiyo haitoshi, ndiyo hao hao wenye kuwekeza kwenye sekta za uchumi mkubwa.
Yatupasa kufikiri kwenye mambo madogo madogo ya uwekezaji na mizengwe yake kabla ya kujitosa kwenye uwekezaji mkubwa ambao utahitaji teknolojia kutoka kwa hao hao wenye hiyo teknolojia na kama hiyo haitoshi utahitaji uendeshaji wa hiyo teknolojia kutoka kwao hao hao.
Si rahisi leo hii, ukurupuke ukamyang'anye mtu tonge mdomoni na ilhali unamuhitaji yeye huyo akutengenezee njia ya kumnyang'anya hilo tonge.
Wenye teknolojia ya kiwango cha kuweka smelter kubwa ya dhahabu yenye kiwango cha kuwakosesha au kuwapunguzia kipato bila wao kufaidika hawatakupa teknolojia hiyo, ukilazimisha watakukubalia, watakula fedha yako ya kusimika ji tembo jeupe (white elephant) ambalo halitakuwa na faida yoyote ya muda mrefu kwako.
Ntaendeleza mada hii kwenye uzi maalum kwa faida ya wengi.
Chini hapa ni uendelezo wa mada kama nilivyoahidi. Napenda tu ifahamike kuwa hii mada ipo "very deep" na nnajitahidi kuifanya "shallow" ili iwe faida kwa wengi. Nikisema niiandike kwa ukamilifu wake, itachukuwa zaidi ya kurasa elfu na haitaisha kwani inagusia mambo mengi sana.
Mada hii ni elimu kwa wanasiasa, wachumi, raia na wapenda maendeleo wote.
Baada ya kuisoma, unaweza kuuliza chochote ambacho unahisi kinahitaji ufafanuzi zaidi.
Laana za Siasa
Siasa, hata pale mwenye madaraka ya nchi, kama tulivyomsikia Rais Magufuli anaposema "mimi siyo mwanasiasa", ukweli ni kuwa hata hilo nalo ni siasa. Kimantiki, anachotueleza Rais wetu ni kuwa, hataki ukiritimba wa kisiasa katika maamuzi yake.
Laana moja wapo ya siasa ni ukiritimba. Kwa ufupi, ukiritimba ni vigumu kuuepuka kwenye siasa na ukiritimba hauna zaidi ya kuchelewesha maamuzi. Maamuzi ya nani? Maamuzi ya yeyote anaetegemea maamuzi ya viongozi au watendaji hususan wa nyanja zote za kiserikali, ambao wengi wao ni wanasiasa au wamejiingiza kwenye mtego wa wanasiasa amma kwa kujijuwa au kwa kutokujijuwa.
Na kama tujuavyo, hakuna awezae kufanya lolote bila kuwemo mkono wa serikali. Maamuzi yetu ya kila siku amma ya kimaisha amma ya kibiashara amma ya kilimo, yoyote yawayo, basi hutegemea maamuzi ya kisiasa. Wanasiasa ndiyo wanaotupangia maisha yetu ya kila siku kwenye nchi tunazoishi. Iwe isiwe hatuwezi kuepukana na hilo.
Tunapowachagua wanasiasa wakati wa kupiga kura huwa tuna mategemeo kuwa huyu atafanya mambo yetu kuwa mepesi au kwa lugha nyingine ataondoa ukiritimba.
Mwanasiasa amma anatuahidi kwa nia njema kabisa amma anatuahidi tu ili tumpe kura ajineemeshe mwenyewe kwanza, ni vigumu kulielewa mpaka atapokuwa madarakani.
Laana hii ya ukiritimba kwenye siasa inaweza ikasababishwa na mwanasiasa aliyepo madarakani kama hana maamuzi thabiti na au ana utawala (administration) wenye mlolongo /milolongo ya ukiritimba. Pia kwa kiasi kikubwa sana inaweza ikasababishwa na upinzani, amma kwa makusudi kabisa amma kwa kutokujuwa walifanyalo.
Nimeelezea juu mojawapo tu ya laana za kisiasa na zipo nyingi zaidi ila kwa kufupisha mada sitozigusia.
Ntarudi kuendelea na mada ya Neema za Siasa, kisha tutaanza mada ya Uchumi na kwa kumalizia itakuwa Dhahabu ili kukamilisha kichwa cha habari Siasa, Uchumi, Dhahabu, Neema na laana zake.
Itaendelea.
Tuendelee:
Neema za siasa.
Nalo hili ntaligusia kwa ufupi tu ili nisiwachoshe wasomaji na wachambuzi wa hii mada:
Neema za siasa ni kuwa na tija njema ya uongozi na utawala kutoka kwa wanasiasa wanaochaguliwa, kuleta tija kwa wananchi wao waliowachagua kuwaongoza wakati walipowapiga siasa. Kati ya tija hizo ni pamoja na kuuwa ukiritimba (kama inawezekana) au kuupunguza kwa kiasi kikubwa (inawezekana), kuwa na mipango thabiti ya kuwapatia wananchi wakitakacho.
Wenye mahitaji ya maji wapate maji, wenye shida ya elimu wapate elimu, wenye shida ya biashara wafanye biashara, wenye shida ya kulima walime, wenye shida ya kuibiwa wawache kuibiwa, wenye mahitaji ya wake wapate wake, wenye mahitaji ya waume wapate waume, wenye mahitaji ya kufuga wafuge, wenye mahitaji ya haki wapewe haki yao, wenye mahitaji ya kuvaa wavae, wenye mahitaji ya kuabudu waabudu. Kwa kifupi, yote hayo na mengi mengineyo ya kihalali yapatikane kwa wakati muafaka (timely manner) na vigezo vyenye ubora (quality) wenye kukubalika bila manung'uniko.
Mwanasiasa bila kutimiza mahitaji ya waliokuchaguwa ulipowapiga siasa inakuwa hakuna Neema ya Siasa bali kutabaki kuwa na usanii wa kisiasa, kila kukicha itabidi upige siasa na mwishowe utaonekana ni wa porojo tu na ulicheza bahati nasibu (opportunist) uliyetaka uchaguliwe ujineemeshe wewe na walio karibu yako (chama chako?).
Chanzo: Criminal politicians face easier future in US - Global Times
Ili kutimiza mahitaji ya wananchi wako waliokuchagua kufikia Neema za Siasa inabidi uwe na uchumi wa uhakika na usioyumba-yumba. Ndipo tunapoingia kwenye Uchumi...
Ntarudi kuendelea na mada ya Uchumi, kisha kwa kumalizia itakuwa Dhahabu ili kukamilisha kichwa cha habari Siasa, Uchumi, Dhahabu, Neema na laana zake.