Siasa Tanzania na utajiri wa kufikirisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa Tanzania na utajiri wa kufikirisha

Discussion in 'Great Thinkers' started by Candid Scope, Aug 12, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kiongozi wa umma anapoonekana kuwa tajiri katika kipindi cha utumishi katika umma tofauti na alivyokuwa kabla ya kuajiriwa utumishi wa umma ni jambo lisilo la kawaida na linafikirisha sana. Hata matajiri duniani wanautajiri ambao vyanzo vyake ni dhahiri na jinsi walivyochangia serikali kwa kodi kutokana na mapato yao. Hii ya kiasi kikubwa cha pesa kuhifadhiwa nje ya nchi asikokuwa na shughuli za biashara wakati akiwa mtumishi wa umma ni kitendo chenye wajibu wa vyombo vya dolla na sheria kufanya utafiti wa kuridhisha umma. Kwani mchumi wa kweli huweka pesa kwenye mzunguko lakini pesa isiyopatikana kwa njia halali hapo hutafutwa njia mbadala ya kuificha nje ya nchi ili mambo yasijulikane.

  Serikali ina utajiri mkubwa sana wa kupata pesa kutokana na tozo la kodi kwa kila raia, makampuni na kila uwezekano wa kutoza kodi. Inashangaza mtu binafsi kuwa na pesa kiasi cha kupita bajeti ya wizara ya serikali na kabisa pesa hizo ni taslim si katika mali ya kuhamishika au kutohamishika. Ni jambo zito sana linalohitaji uwazi kwa mtu binafsi kupatikana na kiasi kikubwa cha pesa taslim nje ya nchi kupita kiasi cha pesa taslim ambacho hata matajiri duniani hawadiriki kuwa nacho. Hali hiyo inaibua maswali mengi mtu binafsi amewezaje kupata kiasi kikubwa hivyo wakati hana vyanzo au biashara inayomwezesha kupata kiasi kama hicho. Pesa ukiziendekeza hupofusha macho usione uendako, ndio maana hata katika ngano za kufikirika nilisoma shule ya msingi zasema "kadiri mtu apatavyo ndivyo atamanivyo."

  Matajiri wakubwa duniani hawana pesa taslim kiasi kama wanachopatikana watu binafsi kuwa nacho, ila kinachofanyiwa tathmini ya utajiri wao ni mali walizo nazo zinazohamishika na zisizohamishika pamoja na pesa taslim walizo nazo ndio zinazotamkwa kwamba ni mabilionea wa kiasi walicho nacho. Hii hali ya mapesa kujilimbikizia nje watu binafsi naona kitendawili kinavyotegua hatua kwa hatua na ukweli ipo siku utawekwa wazi na kuwaumbua watu.

  Hapa usanii mkubwa unaofanyika ni kutumiwa kwa mtu fulani ambaye pengine hawezi kufikiriwa kuwa na pesa nje ya nchi, akatumika kufungua acoount nje ya nchi kwa maslahi ya kikundi au chama fulani cha siasa. Pesa hizo zikawa ni mali ya kikundi fulani au chama fulani ambazo zinachotwa kutoka vyanzo mbalimbali vya umma na serikali kuu. Vyombo vya dola kama usalama wa taifa inashangazo kutojua mchezo unaoendelea kwani wapo kwa usalama wa Taifa la Tanzania si kwa usalama wa mtu, kikundi au chama fulani tu ila Taifa.

  Mpaka mataifa ya nje yaibue uozo ndani ya nchi yetu na serikali kutochukulia uzito na kuona kama hakujatokea kitu kama yalivyotokea haya ya kashfa ya rada, watu binafsi kukutwa na pesa nyingi kama akina Chenge, mwanasheria wa Arusha nk. Hata hivyo serikali imefanya kila jitihada kuwatetea na kuwasafisha watu hao isivyo kawaida. Viongozi waandamizi wako makini kuhudhuria matukio na maziko ya watu lakini hawako makini yatokeapo maafa kwa wananchi na matatizo yanayosababisha kero kubwa kwa wananchi kama umeme, maji, petro nk.

  Katu haki haitatendeka wakati pesa za walipa kodi zikitumiwa na kikundi cha watu, chama fulani bila kujali mambo ya msingi yaliyokusudiwa kwa umma. Sidhani kama jitihada za vyama vya siasa kugawia nguo na kanga za bure kwa wananchi zinaondoa kero ya umeme, mahospitali, mashule, barabara nk. badala yake inaamsha ari zaidi kwa wananchi kukutafuta na kudai haki zao za msingi, kwani pesa za walipa kodi si kwa ajili ya watu fulani nchini au chama fulani ila kwa wananchi wote na tunatazamia hayo yatendeke hivyo.

  Hatujachelewa, wenye uchungu na nchi yao ndio wananchi, na serikali inapaswa kuliona hili, maana mchelea mwana mwisho hulia.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Swali ninalojiuliza je ni lini serikali yetu inachukua umakini katika kushughulikia kero hizi za kuhujumu mali ya umma? Nani atamnyooshea kidole mhujua mali ya umma kama viongozi wa juu wamebaki na hali ya kutofungamana upande wo wote huku mali ikizidi kuporwa?
   
Loading...