Siasa sio uadui kama kiongozi ni mchapa kazi hata kama upo chama cha upinzani huna budi kumsifia.

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
New Mv victoria Hapa kazi tu na Mv Butiama zimeshamilika na sasa zinasubiribiri tu commissioning ili zianze kufanya kazi.

Hii ni hatua kubwa sana katika sekta ya usafirishaji hasa katika ziwa victoria
Wafanyabiashara kati ya mkoa wa Kagera na Mwanza sasa wataenda kunufaika baada meli hizi kuanza kufanya kazi hii ni kwa sababu usafirishaji wa mizigo kwa njia ya gari unagharama kubwa mara tatu zaidi ya ile gharama unapotumia meli.

Hii ni moja ya miradi ambayo ni lazima serikali ya awamu ya tano ipongezwe kwa kuitekeleza tena kwa haraka sana,sababu hizi meli zilikuwa zimeshachoka na sasa zimekarabatiwa na kuwa kama mpya.
Huu ni mmoja wa mfano tu wa namna serikali ya awamu ya tano imejaribu kuleta madiliko mafupi katika sekta ya usafilishaji huku ikiwa inatekeleza ilani yake ya uchaguzi kwa umakini.

Na sio katika ziwa victoria tu ukienda hata ziwa Nyasa kuna meli mbili kubwa zimekamilika na zinafanya kazi na wananchi wanafaidika na matunda ya uchapa kazi wa JPM.

Hii ndio sababu hasa ya vyama vya upinzani hasa Chadema kuishiwa hoja za kuikosoa serikali maana imefanya mambo makubwa kwa Muda mfupi.

Hivyo wapinzani wawe wazalendo na wampongeze rais John Pombe Magufuli.
 
Back
Top Bottom