Siasa Safi ni kuwasaidia wananchi kutoka katika umaskini unaowasumbua Wananchi

kubenafrank

Member
Aug 14, 2011
82
22
Siasa katika Tanganyika imekuwa kama mtaji wa maisha mazuri kwa wanasiasa wengi.Kwa upeo wa kawaida tu, wengi wao baada ya kupewa kura na wananchi huhama katika makazi husika na kuwasahau kabisa waliowachagua.Hali imeacha maswali mengi kwa wapiga kura wengi wa vijijini ambao maisha yao ni magumu mno.
Mfano mzuri ni baadhi ya wabunge na madiwani wengi wa chama tawala.
Iko sababu kubwa ya kubadili mfumo wa siasa zetu hapa tanganyika ili watu hawa waweze kuwajibika moja kwa moja kwa wananchi waliowachagua na si kwa vyama vyao.Wengi walitoa ahadi zisizotekelezeka.Ifike mahali wananchi wasikubali kuchagua kiongozi kwa sababu ya kanga, suruali, kofia au pesa aliyopewa bali tuangalie mtu mwenye dhamira safi ambaye atatuongoza kufikia malengo yetu.
 
Back
Top Bottom