Siasa ni nini?

Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
4,171
2,000
Kwanini wewe unachangia jukwaa la siasa?

Siasa kwako ina maana gani, hasaa; na upo tayari kusimamia msimamo wako muda wowote na kwa gharama yoyote.

Siasa kwako ni utu?

Siasa kwako ni sheria na mipaka ya kutaka kuongozwa (katiba).

Siasa kwako ni sera zenye kuinua jamii?

Siasa kwako ni njia za kumuwezesha kila mtu; huku ukiwa na njia za kufanikisha ilo zoezi.

Kwa kifupi siasa ni somo pana.

Kujiunga na chama gani cha siasa ni utashi wa mtu. Muhimu ni kuelewa chama husika kinasimamia nini.

Usigombane na kupambana kwa sababu ya kuntetea mtu au taasisi isiyo na muelekeo ilimradi tu ujionyshe unasimamia upande hizo siasa.

Either wewe kijana ni CCM, CDM, ACT wazalendo, CUF; jiunge kwenye chama cha siasa kwa sababu ya itikadi ya nini hiko chama kinataka kufanya na wewe ni muumini wa njia zake.

Siasa ni taasisi na itikadi unayojisimamia yenyewe, siasa sio mtu.

Unajiuliza kwanini mtu yupo tayari kujilipua sio kwa sababu ya misimamo yake bali mtu mwingine hizo ndio sababu za kuwa mwanasiasa kweli.

Unasoma JF asilimia kubwa ya wachangiaji ni ushambenga hizo ndio siasa kweli.

Tuache kuwa watumwa wa wengine kama tunataka kuwa wanasiasa.

Unatakiwa kufanya siasa kwa sababu ya namna ambayo una amini jamii inatakiwa kuongozwa (huo ndio msimamo wako sio mtu).
 
Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
4,171
2,000
Kwa wenye akili siasa ni msingi mzuri wa kujenga taifa lenye ustawi na weledi kwa kuzingatia misingi ya sheria na kanuni zilizopo kwa wajinga siasa ni chaka la wizi,rushwa,tamaa ya madaraka,ubinafsi,nk
Kabisa the latter is a problem in our society.

Watu wanavutiwa kwenye siasa kama chaka la wizi, rushwaa........

Hapo ndio shida ilipo ilipo upendwe lazima uridhishe watu wenye tabia hizo serikalini.

Mpaka lini?
 
Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
4,171
2,000
Ndio siasa za leo ni furaha tele.

Serikalini ni kupishana angani.

Mwezi uliopita walikuwa Dubai sijui wizara gani na JK.

Majuzi wizara ya afya walikuwa Dubai kundi kubwa tu.

Wiki ijayo kuanzia tarehe 26 wapo Glasgow na mama anaenda huko tarehe 30 usitishike na picha atakayo piga mama na watu 20 atakao ongozana nao. Kuna la watu kibao kila mtu anaenda na ndege yake ndio siasa tunazotaka hizi.

Mkutano wenyewe nchi 20 zenye uchumi mkubwa ndio zinazochafua asilimia 80 ya mazingira, hivi kweli huo ni mkutano wa sisi kupeleka zaidi ya watu hamsini au wa kusikiliza upuuzi wao.

Ndio unapojiuliza ili kama jukwaa la siasa tukiacha unazi wa siasa ni kitu gani hasa watu wanasimamia.
 
kurlzawa

JF-Expert Member
Jan 23, 2018
16,336
2,000
"Lugha ya mficho yenye maana uongo uliotawala fitina, chuki na laana"
 
Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
4,171
2,000
"Lugha ya mficho yenye maana uongo uliotawala fitina, chuki na laana"
Pamoja na laana za watu.

Achana na nani raisi; nani mpinzani, na democracy ni kitu gani.

Kama wewe maendeleo gani ungependa kuona watanzania wanapata na kwa njia zipi.
 
WALOLA VUNZYA

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
784
1,000
Kwanini wewe unachangia jukwaa la siasa?

Siasa kwako ina maana gani, hasaa; na upo tayari kusimamia msimamo wako muda wowote na kwa gharama yoyote.

Siasa kwako ni utu?

Siasa kwako ni sheria na mipaka ya kutaka kuongozwa (katiba).

Siasa kwako ni sera zenye kuinua jamii?

Siasa kwako ni njia za kumuwezesha kila mtu; huku ukiwa na njia za kufanikisha ilo zoezi.

Kwa kifupi siasa ni somo pana.

Kujiunga na chama gani cha siasa ni utashi wa mtu. Muhimu ni kuelewa chama husika kinasimamia nini.

Usigombane na kupambana kwa sababu ya kuntetea mtu au taasisi isiyo na muelekeo ilimradi tu ujionyshe unasimamia upande hizo siasa.

Either wewe kijana ni CCM, CDM, ACT wazalendo, CUF; jiunge kwenye chama cha siasa kwa sababu ya itikadi ya nini hiko chama kinataka kufanya na wewe ni muumini wa njia zake.

Siasa ni taasisi na itikadi unayojisimamia yenyewe, siasa sio mtu.

Unajiuliza kwanini mtu yupo tayari kujilipua sio kwa sababu ya misimamo yake bali mtu mwingine hizo ndio sababu za kuwa mwanasiasa kweli.

Unasoma JF asilimia kubwa ya wachangiaji ni ushambenga hizo ndio siasa kweli.

Tuache kuwa watumwa wa wengine kama tunataka kuwa wanasiasa.

Unatakiwa kufanya siasa kwa sababu ya namna ambayo una amini jamii inatakiwa kuongozwa (huo ndio msimamo wako sio mtu).
Siasa ni maisha ya mwanadamu anayoyaishi hapa duniani kuanzia kuzaliwa kwake,kusoma kwake,kukua kwake mpaka siku ya kufa kwake kijamii,kiutamaduni,kiuchumi na kielimu,ili mtu afurahie maisha lazima apambane na maadui endelevu kama umaskini,ujinga,maradhi na utumwa.Mapambano haya humfanya mtu kuwa mwanasiasa bila kujua kwa sababu anataka kuboresha maisha yake.
Tumeona na tumesoma kuwa tangu enzi za zama za mawe binadamu amepita kwenye changamoto nyingi na alikabiliana nazo kwa namna tofauti tofauti kufuatana na jiografia ya mahali husika.Yaani bila mapambano hakuna maendeleo,bila mapambano hakuna umoja,bila mapambano hakuna mshikamano,bila mapambano hakuna maisha bora,bila mapambano hakuna haki,bila mapambano hakuna amani na bila mapambano hakuna utu pia.
Mwanadamu kama mwanadamu ni mwumbaji kwa sababu alipewa nguvu hizo au mamlaka hayo na Mungu mwenyezi,kumkatisha mtu tamaa asipambane na mazingira ili uendelee kumnyonya ni dhambi,na ni kosa kiuhalisia.Ikumbukwe kuwa bila siasa Tanzania isingekuwepo,Kiswahili kisingewaunganisha Watanzania,bila siasa tusingekuwa na rais tungeendelea kutawaliwa na machifu,waarabu au wazungu.
Ukiona mtu anakatisha watu tamaa kusema watu wasipende siasa ujue huyo ni dikteta,mchoyo,mlafi na mchawi kwa sababu yeye yuko kwenye siasa anakula mema ya nchi hataki wengine wale kama yeye.Fuata nyuki ule asali,hivyo siasa ni asali,na ili ule asali kubali kung'atwa na nyuki na uvumilie utakula sali kiulaini na utapelekea familia watafurahi na hawatajiuliza maumivu uliyoyapitia mpaka kupata asli hiyo.Tusikatishane tamaa kwa sababu uwezo wetu unatufanya tuwe wachoyo na walafi.Mungu ibariki Afrika,Mungu ibariki Tanzania na watu wake,kazi iendelee.
 
Nakubaliana na tafsiri yako ila nimegawanya kwa pande mbili.

Paragraph yako ya kwanza hiyo ndio maana ya siasa (kwa uelewa wangu).

Paragraph ya pili malalamiko yako kwa viongozi hayo mamlaka tunatoa sisi wananchi kwa watawala kwa mujibu wa katiba na chaguzi (kwa ivyo hapo kuna constitutional issues na sio lengo la post).

Tukirudi kwenye swali asili je tunawapa mamlaka watu sahihi kututawala kutokana na tafsiri yako ya siasa kama ulivyoelezea kwenye paragraph yako ya kwanza. Kwa lugha nyingine agenda zao ndio vipaumbele vyako kama ulivyoelezea?

Ndipo swali langu lilipo kama ujaridhika na unachofanyiwa na serikali yako ya sasa kutokana na tafsiri yako ya siasa ni kipi ungetaka kufanya kusaidia jamii kama agenda yako; kabla ya kuchagua chama.

Je chama ni agenda ya kutatua shida za watu (itikadi) au kumuabudu kiongozi kama siasa za vyama vyetu zinapoelekea.
 
Pamoja sana.Kwanza nikupongeze kwa kuisoma na kuichambua hoja yangu vizuri,asante.Pili niseme siasa yetu ya kiitikadi siyo siasa bali ni uhuni na uzandiki.Kama unavyojua historia ya nchi yetu tulikotokea tangu enzi za ukoloni hadi uhuru,uhuru mfumo wa vyama vingi hadi mfumo wa chama kimoja kushika hatamu,chama kimoja hadi mfumo wa vyama vingi kidemokrasia na kutoka mfumo wa vyama vingi kwenda kwenye mfumo wa uwezo wa kiongozi tangu 2015 hadi sasa hivi unaozingatia itikadi za chama chake,hiyo imepelekea tuwe na siasa mbaya kuwahi kutokea na tunakoelekea hata kipofu anajua.
Pia napenda nikulaumu kwa kauli yako ya kusema nalaumu,neno hili siyo zuri nalaumu nini?? Mwenyewe unajua shida ni nini ndiyo maana umetuletea nyimbo hiii ya SIASA NI NINI ukiwa na majibu unayoyataka wewe.Amani haijengwi kwa maneno ila kwa ncha ya upanga wahenga walisema.Nyerere angeendelea kuabudu Wazungu mpaka sasa nchi ingekuwa mikononi mwa Wazungu kwa sababu sheria tunazotumia hadi leo zilitungwa na wazungu na bado tunaendelea kuzitumia hizo hizo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom