Siasa ni Maisha; ni uhai! Ona jinsi gani siasa ilivosababisha wafaransa kuuwa waingereza na Lugha yao ya kiingereza!

Fyafyafya

Member
Nov 30, 2017
53
150
Bonjour! bonjour! bonjour!!

Hello! hello! hello!!

Ndugu; Kwa wale wanaozungumza au kutumia Lugha ya Kiingereza mtakubaliana na mimi kuwa ni ukweli ulotukuka kuwa lugha ya kiingereza imesheheni maneno Lukuki ya Kifaransa.

Pengine kwa kuwa sifa moja wapo za Lugha ni kukua na katika ukuaji wa lugha michakato kama: Kugundua maneno mapya ( misemo) ; Kuazima maneno ya Lugha fulani na luyatumia; Utohoaji wa maneno ya lugha fulani n.k huhusika basi kwa Lugha ya kiingereza si hivo tu! Bali ni zaidi ya hapo. Kunahusishwa na maswala ya kihistoria kwa upande wa utawala.

Ukweli wa mambo yote ni Siasa!!

Katika karne ya 10 toka mwaka ( 1066) hadi karne ya 13 yaani mwaka ( 1272)
takribani miaka 200 taifa la wingereza lilikuwa chini ya Himaya ya wafaransa. ( french conquerors) wakiongozwa na the norman WILLIAM THE CONQUEROR au WILLIAM THE BASTARD) mwaka 1066. Kuanzia mwaka huo (1066) hadi mwaka 1272 uingereza ilikuwa ikitawaliwa na ma king wa jamii ya kifaransa ( Norman Kings in england) kwa miaka 200. Wafalme wa kifaransa walotawala uingereza walikuwa kama

1. 1066- 1087: William the Conqueror
2. 1087 - 1100 : William II
3. 1100 - 1135 : Nenry I
4. 1135 - 1154 : Stephen
5. 1154 - 1184 : Henry II
6. 1184 - 1199 : Richard I
7. 1199 - 1216 : John
8. 1216 - 1272 : Henry III

Hao wafalme wote nane walikuwa wa jamii ya kifaransa na walikuwa wavaamizi ambao walifanikiwa kuiongonza nchi ya Uingereza kwa kipindi hicho.

Sasa turudi kwenye maada yetu inayosema " Ona ni kwa nini Maneno ya lugha ya Kiingereza zaid ya 45% yana asili ya lugha ya Kifaransa."

Sababu moja kuu ni hii:

 • Wingereza kutawaliwa na ufaransa kwa miaka 200.
Inchi kutawaliwa kwa miaka hiyo yote si lele mama. Na kumbuka inchi nyingi zilizotawala nyingine zililazimika kuacha utamaduni wao na hasa swala la Lugha. Kwa hiyo wafaransa nao hawakufanya kosa walifanya vivo hivo nchini wingereza na hata kwenye makoloni mengine walotawara kwa mfano barani Afrika. Walitimia mfumo wao wa Assimilation! ( French Assimilation)

Maelezo hayo yanaweza yasitoshe kwako wewe na uweze kuelewa hii sababu. Historia inasema kuwa wafalme hao wakifaransa hawakuona haja ya kujifunza kiingereza kwa maana hiyo basi Lugha ya mawasiliano head quaters na maeneo mengi sana ya kiutawala ilikuwa ni kifaransa. Kifaransa ilikuwa ni lugha ya mawasiliano kwenye huduma za jamii zote. Upper class na middle class wote walikuwa wakitumia kifaransa kuwasiliana. Hivo basi hata jamiii za chini iliwabidi waaanze kujifunza kifaransa ili waweze kupata huduma.

 • Kuoana.
Viongozi na wanajeshi wa kifaransa waliwaoa wanawake waingereza na l
pengine kupelekea jamii kubwa ya waingereza kuishi ufaransa. Kuooana huko kulizidi kuimarisha lugha ya kifaransa nchini wingereza.

 • UTHIBITISHO. ( Proof)
Kuna msemo maarufu usemao :"No data no reaserch! na wengine huenda mbali na kusema : " No Data no wright to speak!"

Kwa kuthibitisha haya yote nilokwambieni; basi hembu tuone baadhi ya viielelezo vya maneno ya Kiingereza yanayofana na maneno ya Kifaransa.

 • Maneno yote yanayoishia na : - Tion; - Ssion - ; Sion ; - Ion.
Maneno yote ya kiingereza yanayoishia na -tion -ssion - sion na - ion ni ya lugha ya kifaransa. Asili yake ni Lugha ya kifaransa.

Kwa kifaransa hivo viambishi ( morphem) - tion na - ssion hutamkika - Siyo.
Kwa mfano neno : action hutamkika: akisio na neno Mission hutamkika misio. Na kama kawaida - tion na - ssion hutamkika - sheni. kwa kiingereza.

Kwa kifaransa kiambishi - sion hutamkika zio kwa mf. vision hutamkika vizio na kiambishi ion hutamkika -io kwa mfano : opinion hutamkika opinio.
NB. Kugha ya kifaransa hutumia sana pua na koo kutamka herufi . Basi hizo - io zote huwa - iõ maana yake hiyo o yenye ka kofia juu hutamkika puani.

Kwa hiyo maneni yote ama
 • Attention
 • option
 • collection
 • addition
 • permission
 • discussion
 • collusion
 • division
 • n.k yapo hivo hivo pengine mengine yakiwa na tualama ( accents è é ç ê ï )Kenye maneno kama préparation ; élection ; forêt; hôpital n.k maneno hayo yana maana hiyo hiyo ya kiingereza ila matamshi ndo hutofautiana.

 • Maneno yote yanayoishia na - MENT yana asili ya kifaransa.
Siyo siri kingereza kina maneno lukuki ambayo yanaishia na - ment. Maneno hayo yote yana asili ya Lugha ya kifaransa. Maana yake ni hiyo hiyo kwa lugha zote mbili.

Kwenye Lugha ya kifaransa hiyo - ment hutamkika - ma ( ma hutamkiwa puani) yaani :
kwa mf:

Kiingereza kifaransa
jugement jugement
development dévélopement
document document
element élément
environment enveronnement

 • Maneno ya kiingereza yanayoishia na - Ty.
Maneno yote ya kiingereza yanayoishia na - ty yana asili ya lugha ya kifaransa na kwa kifaransa maneno hayo huishiwa na-té badala ya -ty. Maana yake utohohoaji ulifanika kama na sisi waswahili tulivyotohoa baadhi ya maneno ya kiingereza kama Shati toka neno Shirt, Sketi toka neno skirt; baisikeli toka neno bicycle n.k Maana yamaneno hayo inabaki kuwa hiyo hiyo kwenye hizo lugha zote mbili.

Ona mfano hapa.
Kiingereza: Kifaransa
Capacity capacité
unity unité
university université
ntionality nationalité
n.k

 • Vivumishi na maneno yanayoishia na - ent/ ant
Vivumishi na Maneno ya kiingereza yanayishoa na - ent au - ant yana asili ya Lugha ya Kifaransa.
Kwa lugha ya kifaransa hizo mofimu - ent na - ant hutamkika - ã yaani a ya puani na kolomeo.
kwa mfano:

Kiingereza kifaransa
excellent excellent
ignorant ignorant
extent extent
confident confident
innocent innocent
vicent vincent
n.k

 • Majina ya magonjwa
Kiingereza kifaransa
malaria malaria
typhod typhoïde
kwashiorkor kwashiorkor
marasmas marasme
HIV AIDS VIH SIDA
diarrhea diarhée
cholera cholera
n.k

 • Majina ya masomo
kiingereza kifarans
mathematics mathématique
physics physique
chemistry chimie
biology biologie
geography géographie
civics civisme
history histoire
n.k

 • Majina ya michezo
kiingereza kifaransa
football football
tennis tennis
rugby rugby
basketball basket
n.k


 • Vitenzi ( verbs)
kiingereza kifaransa
arrive arriver
correct correcter
collect collecter
introduce introduire
commit commettre
ommit ommettre
transmit transmettre
construct construire
produce produire
elect élire

etc
 • Maneno mengine
Kiingereza kifaransa
table table
route route
verb verbe
abverb adverbe
adjective adjectif
pronoun pronom
present présent
past passé
future future
conditionnal conditionnel
conjunction conjonction
grammar grammaire
usage usage
continent continent
ball ballon
match matche
positive positif
bible bible
coran coran
negative négatif
christian chrétien
muslim musulan
page page
poem poème
radio radio
Tv Tv
television télévision
elephant élephant
train tain
bus bus
ok ok
autobus autobus
vehicle véhicule
person personne
baby bébé
voice voix
salary salaire
electricity électricité
president président
Tanzania Tanzanie
somalia somalie
Colombia colombie
hotel hôtel
lake lac
river rivière
ocean océan

n.k

Nb: Kuna baadhi ya maneno ya kifaransa yanafanana na maneno ya kiingereza ila hayana maana sawa. Maana zake ni tofauti kwenye hizo lugha mbili. Kwa mf.

 • face
 • coin
 • hasard
 • figure
 • n.k
a) face
Kama kawaida; neno 'face' kwa kiingereza humaanisha uso ila kwa kifaransa halimaanishi hivo. Sio uso! Kwa kifaransa neno "face" humaanisha sehemu' yaani place' kijisehemu.

b) coin
Kwa kawaida neno coin' kwakiingereza humaanisha koini au siliva ( pesa) ila kwa kifaransa neno coin liko hivo hivo ila halimaanishi siliva ila linamaanisha kona. Kwenye kona fulani. Au coin! at the corner.

c) hasard
Kwa kiingereza neno hasard humanisha hatari; yaani danger. Kwa kifaransa liko hivo hivo ila halina maana hiyo. Hasard kwa kifaransa humaanisha bahati ( chance)

d) figure
Kwa kiingereza, neno figure humaanisha umbile la kitu. stracture yake. Maumbile ya kitu au mtu. Kwa kifaransa neno hilo liko hivo hivo ila halina maana hiyo. kwa kifaransa figure' humaanisha uso! Yaani usoni ambayo sasa kwa kiingereza huitwa face!!!

Haha hahah haha!!!!!

Jua pia kuwa kwa lugha ya kifaransa Kitenzi kudondoka au kuanguka huitwa : Tomber!
Hapo sasa ndo waswahili wanaojifunza kifaransa huona aibu wanapokuwa wakikonjigeti verbu hii au wakiongea.

Kwa kifaransa maana ya Kufanya malenzi yaani ku~mba huitwa Faire l'amour / Sexer


Hitimisho!

1. Kifaransa ni Lugha ya pili ya kimataifa baada ya kiingereza. Huongelewa katika mataifa mbali mbali na kwenye maswala ya kidiplomasia ni cha pili baada ya kiingereza. Siku hizi watu wengi hapa nchini wamekuwa na hulka na shauku kubwa sana kujifunza na kujua kuongea hii Lugha tamu zaidi kwani ina fursa nyingi sana pia ni vema kujua lugha za kimataifa zaidi ya moja kwa mafanikio zaidi.

Kwa uchambuzi huu hapa nilowapeni; basi bila shaka mmejionea ni jinsi gani kifaransa ni chepesi ilhali tu unajuwa kiungereza. Niseme tu kingereza na kifaransa are two sides of the same coin!

2. Pia kifaransa kinatumia alphabet zile zile kaa za kiingereza A B C B D E D G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z. Na kwa 80% ya matamshi ya hizo herufi ni sawasawa na matamshi ya kiswahili.

3. Neno Bastard la kiingereza linalofanana pi na neno Batârd la kifaransa humaanisha Mtoto wa nje ya Ndoa! Mtoto aliyezaliwa nje ya familiya ya ndoa. Ama, baba kamzaa kwa mchepuko kabla ya kuona hata baada ya kuoa pia ama, Mama kamzaa kwa mchepuko kabla na baada ya kuolewa. Basi mtoto huo huitwa kwa Lugha ya kiigereza Bastard au Bâtard kwa lugha ya kifaransa.

Kama tulivoona hapo mwanzo; mfalme wa kwanza wa uingereza kutoka Ufaransa ndugu William the Conqueror au kwa jina lake la utani William the Bastard (1066-1085) alikuwa mtoto wa nje ya ndoa na yeye ndo aliefungua njia kwa utawala wa wafaransa pale uingereza kipindi hicho.

Hapa tunajifunza yakuwa watoto nje ya ndoa au watoto wa kambo ndio wenye chance kubwa ya kureta mafanukio na mapinduzi katika nchi na familiya kwa ujumla. Hebu fikilia jamaa ( William the Bastard) toka kuwa mtoto wa nje ya ndoa hadi kuwa mfalme tena kwenye nchi jirani! Toka kuwa bastard hadi kuleta mchango mkubwa kwa kukuza lugha yake ( kifaransa) kwa kukipandikiza na kumeza lugha ya nchi jirani ( wingereza)! Huu kweli ni mchango mkubwa sana.

Kutokana na William the Conqueror; Lugha ya kiingereza ilijikuta ikimezwa na lugha ya kifaransa as why mpaka sasa maneno 45% ya kiingereza yana Asili ya Lugha ya Kifaransa.

Kama ulikuwa hujui; Msemo huu :" From zero to Hero." Huwa una be proved na watoto wenye mazingira magumu; watoto mayatima; watoto wa kambo n.k. Watoto hawa kuishi kwa shida na baadae huja kuwa watu wakubwa sana kisiasa ; kiuchumi na kijamii. Kwa mfano Ona Raisi wa nchi hii Mh. Magufuli

 

crocodile

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,056
2,000
Hivi Wafaransa wanatumia nini kunajisi fikra za Waafrika wenzetu kama huyu mjuba hapo juu???
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom