Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,282
Siasa kwa mwanasiasa ni kazi, kama ilivyo biashara kwa mfanyabiashara na kilimo kwa mkulima. Zitto Z Kabwe akikaa mahabusu kwa makosa ya kisiasa ni sawa sababu ni kiongozi wa chama na siasa kwake ni kazi. Hii haina tafauti kwa mkulima kugongwa na nyoka shambani au kwa malaya kupata HIV, naam, imethibiti ajali kazini.
Mwanachama wa chama cha siasa ambaye si mwanasiasa kuwekwa rumande au gerezani kwa sababu ya siasa na kuumia na hata kufa sababu ya siasa ni ujinga ambao anatakiwa kujivua na kukaa nawo mbali, nao uwe mbali naye.
Kwa mimi mwanachama nikiwekwa ndani kwasababu ya chama ni ujinga. Kwanini nasema hivyo???
Mosi, siasa kwangu si kazi ni dhahiri nikiwekwa ndani kazi zangu zitasimama na wanaonitegemea watalala njaa. Nitawezaje kulima au kufanya biashara nikiwa rumande??? Hivi mimi nikiwekwa Rumande, Zitto au chama changu kitalisha na kutatua changamoto za familia yangu??? Kama hilo haliwezekani, kwanini sasa nifanye mambo ya kuwagharimu wanaonitegemea????
Lakini Zitto na Mbowe akiwekwa rumande au gerezani, kazi yao, ambayo ni siasa, haisimami, sababu wakiwa ndani kwa makosa ya siasa, kazi yao(siasa), ndiyo inanoga. Full kiki!!!
Pili.
Kuwa mwanachama wa chama cha siasa hakunifanyi hata kidogo niwe radhi kuweka rehani maisha yangu na wanaonitegemea.
Naweza kuweka maisha yangu rehani sababu ya siasa endapo tu:
Mosi nchi yangu ikivamiwa na nchi nyingine na uhuru wake wa kujiamulia mambo yake kuwa hatarini. Hapo sitakubali, nitapambana hadi tone la mwisho la damu yangu.
Pili, ikitokea serikali ikaninyima haki yangu ya kuchagua mtu wa kuniongoza kila kipindi cha miaka mitano au miaka ambayo tumekubaliana kama taifa kwa njia ya uwazi na ukweli, au bunge likavunjwa kinyume cha katiba, na au serikali ikikithirisha kukakaidi hukumu na maagizo ya mahakama hususani juu ya mambo yanayogusa haki za msingi za raia.
Hapa namaanisha mahakama na bunge zikiingiliwa na serikali kwa kiwango cha kuvunjwa vipengele vya katiba vilivyounda bunge na mahakama, ni dhahiri serikali hiyo inapoteza uhalali wa kisiasa na kisheria wa kuheshimiwa na kufuatwa na kila mwananchi wa nchi hii.
Serikali ya namna hiyo niko tayari kuitoa kwa jasho na damu yangu. Serikali ya CCM, kama mpinzani, nitapambana kuitoa kwa kura yangu, sababu haina sifa ya kutolewa kwa jasho na damu yangu Tukumbuke CCM haikujipeleka ikulu yenyewe, bali ni wananchi walio wengi ndiyo waliyoipeleka ikulu kwa kutumia sanduku la kura. Hata kama sikupigia kura, lakini hakufanyi wengi waliopigia kuwe si kitu na kwa kubezwa ikiwa uchaguzi huo ulifata sheria.
TANBIHI.
Niliposema kwa wanasiasa sawa kuwekwa ndani sababu ya siasa, siku maanisha ni sawa serikali kuwashikilia wanasiasa kinyume cha sheria, nilicho maanisha wao kuwekwa ndani ni suala la kawaida lakini kwa mimu nikiwekwa ndani kudhulumiwa na kujidhulumu sababu si mwanasiasa.
Kila muomba chumvi, huombea chungu chake,
Hata mtandika jamvi, hulenga ubavu wake,
Aliyeuchonga mvi, alijua windo lake,
Dotto Rangimoto
Jini Kinyonga
+255762845394 Morogoro.